Kutoka 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 10 (Swahili) Exodus 10 (English)

Bwana akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao; kwa kuwa mimi nimeufanya moyo wake mzito, nipate kuzionyesha ishara zangu hizi kati yao; Kutoka 10:1

Yahweh said to Moses, "Go in to Pharaoh, for I have hardened his heart, and the heart of his servants, that I may show these my signs in the midst of them,

nawe upate kusema masikioni mwa mwanao, na masikioni mwa mjukuu wako, ni mambo gani niliyotenda juu ya Misri, na ishara zangu nilizozifanya kati yao; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Kutoka 10:2

and that you may tell in the hearing of your son, and of your son's son, what things I have done to Egypt, and my signs which I have done among them; that you may know that I am Yahweh."

Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, Bwana, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie. Kutoka 10:3

Moses and Aaron went in to Pharaoh, and said to him, "This is what Yahweh, the God of the Hebrews, says: 'How long will you refuse to humble yourself before me? Let my people go, that they may serve me.

Au, kwamba wakataa kuwapa hao watu wangu ruhusa waende zao, tazama, kesho nitaleta nzige waingie ndani ya mipaka yako; Kutoka 10:4

Or else, if you refuse to let my people go, behold, tomorrow I will bring locusts into your country,

nao wataufunika uso wa nchi, mtu asipate kuona hiyo nchi; nao watakula mabaki ya hayo yaliyopona yaliyowasalia baada ya ile mvua ya mawe, watakula kila mti umeao kwa ajili yenu mashambani; Kutoka 10:5

and they shall cover the surface of the earth, so that one won't be able to see the earth. They shall eat the residue of that which has escaped, which remains to you from the hail, and shall eat every tree which grows for you out of the field.

na nyumba zako, na nyumba za watumishi wako, na nyumba za Wamisri wote zitajawa na nzige; mfano wake baba zako wala baba za baba zako hawakuona, tangu siku walipoanza kuwapo juu ya nchi hata hivi leo. Basi akageuka na kutoka kwa Farao. Kutoka 10:6

Your houses shall be filled, and the houses of all your servants, and the houses of all the Egyptians; as neither your fathers nor your fathers' fathers have seen, since the day that they were on the earth to this day.'" He turned, and went out from Pharaoh.

Ndipo watumishi wa Farao wakamwambia, Mtu huyu atakuwa tanzi kwetu sisi hata lini? Wape hawa watu ruhusa waende zao, wamtumikie Bwana, Mungu wao; hujatambua bado ya kuwa Misri imekwisha haribika? Kutoka 10:7

Pharaoh's servants said to him, "How long will this man be a snare to us? Let the men go, that they may serve Yahweh, their God. Don't you yet know that Egypt is destroyed?"

Musa na Haruni wakaletwa tena kwa Farao; naye akawaambia, Nendeni, mkamtumikie Bwana, Mungu wenu; lakini ni kina nani watakaokwenda? Kutoka 10:8

Moses and Aaron were brought again to Pharaoh, and he said to them, "Go, serve Yahweh your God; but who are those who will go?"

Musa akamjibu, Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu, tutakwenda na kondoo zetu na ng'ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia Bwana sikukuu. Kutoka 10:9

Moses said, "We will go with our young and with our old; with our sons and with our daughters, with our flocks and with our herds will we go; for we must hold a feast to Yahweh."

Lakini akawaambia, Ehe, Bwana na awe pamoja nanyi, kama nitakavyowapa ruhusa kwenda zenu pamoja na watoto wenu; angalieni, kwa kuwa pana uovu huko mbele yenu. Kutoka 10:10

He said to them, "Yahweh be with you if I will let you go with your little ones! See, evil is clearly before your faces.

Sivyo; endeni ninyi mlio watu wazima, mkamtumikie Bwana; kwa kuwa ndilo jambo mtakalo. Nao walifukuzwa usoni pa Farao. Kutoka 10:11

Not so! Go now you who are men, and serve Yahweh; for that is what you desire!" They were driven out from Pharaoh's presence.

Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya nchi ya Misri kwa hao nzige, ili wakwee juu ya nchi ya Misri, waile mimea yote ya nchi, yaani, vyote vilivyosazwa na ile mvua ya mawe. Kutoka 10:12

Yahweh said to Moses, "Stretch out your hand over the land of Egypt for the locusts, that they may come up on the land of Egypt, and eat every herb of the land, even all that the hail has left."

Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na Bwana akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige. Kutoka 10:13

Moses stretched forth his rod over the land of Egypt, and Yahweh brought an east wind on the land all that day, and all the night; and when it was morning, the east wind brought the locusts.

Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya Misri, walikuwa wabaya mno; hawajakuwapo nzige kama hao majira yo yote, wala baada yao hawatakuwa wengine jinsi hiyo. Kutoka 10:14

The locusts went up over all the land of Egypt, and rested in all the borders of Egypt. They were very grievous. Before them there were no such locusts as they, neither after them shall be such.

Kwa kuwa waliufunika uso wote wa nchi, hata nchi iliingia giza; wakala mimea yote ya nchi, na matunda yote ya miti yaliyosazwa na ile mvua ya mawe; hapakusalia hata jani moja, mti wala mmea wa mashamba, katika nchi yote ya Misri. Kutoka 10:15

For they covered the surface of the whole earth, so that the land was darkened, and they ate every herb of the land, and all the fruit of the trees which the hail had left. There remained nothing green, either tree or herb of the field, through all the land of Egypt.

Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni haraka; akasema, Nimemfanyia dhambi Bwana, Mungu wenu na ninyi pia. Kutoka 10:16

Then Pharaoh called for Moses and Aaron in haste, and he said, "I have sinned against Yahweh your God, and against you.

Basi sasa, nawasihi, nisameheni dhambi yangu mara hii moja tu, mkamwombe Bwana, Mungu wenu, aniondolee kifo hiki tu. Kutoka 10:17

Now therefore please forgive my sin again, and pray to Yahweh your God, that he may also take away from me this death."

Akatoka kwa Farao, na kumwomba Bwana. Kutoka 10:18

He went out from Pharaoh, and prayed to Yahweh.

Bwana akaugeuza upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka katika Bahari ya Shamu; hakusalia hata nzige mmoja ndani ya mipaka yote ya Misri. Kutoka 10:19

Yahweh turned an exceeding strong west wind, which took up the locusts, and drove them into the Red Sea. There remained not one locust in all the borders of Egypt.

Lakini Bwana akaufanya ule moyo wa Farao uwe mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa waende zao. Kutoka 10:20

But Yahweh hardened Pharaoh's heart, and he didn't let the children of Israel go.

Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, kuwe giza juu ya nchi ya Misri, watu wapapase-papase gizani. Kutoka 10:21

Yahweh said to Moses, "Stretch out your hand toward the sky, that there may be darkness over the land of Egypt, even darkness which may be felt."

Basi Musa akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; kukawa na giza nene katika nchi yote ya Misri muda wa siku tatu; Kutoka 10:22

Moses stretched forth his hand toward the sky, and there was a thick darkness in all the land of Egypt three days.

hawakupata kuonana mtu na mwenziwe, wala hakuondoka mtu mahali alipokuwa muda wa siku tatu; lakini wana wa Israeli wote walikuwa na mwanga makaoni mwao. Kutoka 10:23

They didn't see one another, neither did anyone rise from his place for three days; but all the children of Israel had light in their dwellings.

Farao akamwita Musa, na kumwambia, Haya, nendeni, mkamtumikie Bwana; kondoo zenu na ng'ombe zenu tu na waachwe; watoto wenu nao na waende pamoja nanyi. Kutoka 10:24

Pharaoh called to Moses, and said, "Go, serve Yahweh. Only let your flocks and your herds stay behind. Let your little ones also go with you."

Musa akasema, Ni lazima utupe mikononi mwetu na wanyama wa dhabihu na wa sadaka za kuteketezwa, ili tupate kumchinjia Bwana Mungu wetu dhabihu. Kutoka 10:25

Moses said, "You must also give into our hand sacrifices and burnt-offerings, that we may sacrifice to Yahweh our God.

Makundi yetu pia watakwenda pamoja nasi; hautasalia nyuma hata ukwato mmoja; kwa maana inampasa kutwaa katika hao tupate kumtumikia Bwana, Mungu wetu; nasi hatujui, hata tutakapofika huko, ni kitu gani ambacho kwa hicho inatupasa kumtumikia Bwana. Kutoka 10:26

Our cattle also shall go with us. There shall not a hoof be left behind, for of it we must take to serve Yahweh our God; and we don't know with what we must serve Yahweh, until we come there."

Lakini Bwana akaufanya kuwa mgumu moyo wa Farao, asikubali kuwapa ruhusa waende zao. Kutoka 10:27

But Yahweh hardened Pharaoh's heart, and he wouldn't let them go.

Farao akamwambia Musa, Nenda zako, ujiangalie, usinione uso tena; kwani siku hiyo utakayoniangalia uso wangu utakufa. Kutoka 10:28

Pharaoh said to him, "Get away from me! Be careful to see my face no more; for in the day you see my face you shall die!"

Musa akasema, Umenena vema; mimi sitakuangalia uso wako tena. Kutoka 10:29

Moses said, "You have spoken well. I will see your face again no more."