Kutoka 23 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 23 (Swahili) Exodus 23 (English)

Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu. Kutoka 23:1

"You shall not spread a false report. Don't join your hand with the wicked to be a malicious witness.

Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu; Kutoka 23:2

You shall not follow a crowd to do evil; neither shall you testify in court to side with a multitude to pervert justice;

wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake. Kutoka 23:3

neither shall you favor a poor man in his cause.

Ukimwona ng'ombe wa adui wako, au punda wake, amepotea, sharti umrudishie mwenyewe tena. Kutoka 23:4

"If you meet your enemy's ox or his donkey going astray, you shall surely bring it back to him again.

Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye hali ameanguka chini ya mzigo wake, nawe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie. Kutoka 23:5

If you see the donkey of him who hates you fallen down under his burden, don't leave him, you shall surely help him with it.

Usipotoe hukumu ya mtu maskini katika neno lake. Kutoka 23:6

"You shall not deny justice to your poor people in their lawsuits.

Jitenge mbali na neno uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu. Kutoka 23:7

"Keep far from a false charge, and don't kill the innocent and righteous: for I will not justify the wicked.

Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki. Kutoka 23:8

You shall take no bribe, for a bribe blinds those who have sight and perverts the words of the righteous.

Usimwonee mgeni; maana, ninyi mwajua moyo wa mgeni ulivyo, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. Kutoka 23:9

"You shall not oppress an alien, for you know the heart of an alien, seeing you were aliens in the land of Egypt.

Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake; Kutoka 23:10

"For six years you shall sow your land, and shall gather in its increase,

lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni. Kutoka 23:11

but the seventh year you shall let it rest and lie fallow, that the poor of your people may eat; and what they leave the animal of the field shall eat. In like manner you shall deal with your vineyard and with your olive grove.

Siku sita utafanya kazi yako, na siku ya saba utapumzika; ili kwamba ng'ombe wako na punda wako wapate kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako na mgeni wapate kuburudika. Kutoka 23:12

"Six days you shall do your work, and on the seventh day you shall rest, that your ox and your donkey may have rest, and the son of your handmaid, and the alien may be refreshed.

Yaangalieni hayo yote niliyowaambia; wala msitaje kabisa majina ya miungu mingine, wala yasisikizwe kutoka kinywani mwako. Kutoka 23:13

"Be careful to do all things that I have said to you; and don't invoke the name of other gods, neither let them be heard out of your mouth.

Mara tatu kila mwaka utaniwekea sikukuu. Kutoka 23:14

"You shall observe a feast to me three times a year.

Utaiweka sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu; utakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba kama nilivyokuagiza, kwa wakati uliowekwa, mwezi wa Abibu (kwa maana ndio mwezi uliotoka Misri); wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu; Kutoka 23:15

You shall observe the feast of unleavened bread. Seven days you shall eat unleavened bread, as I commanded you, at the time appointed in the month Abib (for in it you came out from Egypt), and no one shall appear before me empty.

tena, sikukuu ya mavuno, hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani. Kutoka 23:16

And the feast of harvest, the first fruits of your labors, which you sow in the field: and the feast of harvest, at the end of the year, when you gather in your labors out of the field.

Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU. Kutoka 23:17

Three times in the year all your males shall appear before the Lord Yahweh.

Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi. Kutoka 23:18

"You shall not offer the blood of my sacrifice with leavened bread, neither shall the fat of my feast remain all night until the morning.

Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake. Kutoka 23:19

The first of the first fruits of your ground you shall bring into the house of Yahweh your God. "You shall not boil a kid in its mother's milk.

Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Kutoka 23:20

"Behold, I send an angel before you, to keep you by the way, and to bring you into the place which I have prepared.

Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. Kutoka 23:21

Pay attention to him, and listen to his voice. Don't provoke him, for he will not pardon your disobedience, for my name is in him.

Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao. Kutoka 23:22

But if you indeed listen to his voice, and do all that I speak, then I will be an enemy to your enemies, and an adversary to your adversaries.

Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali. Kutoka 23:23

For my angel shall go before you, and bring you in to the Amorite, the Hittite, the Perizzite, the Canaanite, the Hivite, and the Jebusite; and I will cut them off.

Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande. Kutoka 23:24

You shall not bow down to their gods, nor serve them, nor follow their practices, but you shall utterly overthrow them and demolish their pillars.

Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Kutoka 23:25

You shall serve Yahweh your God, and he will bless your bread and your water, and I will take sickness away from your midst.

Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. Kutoka 23:26

No one will miscarry or be barren in your land. I will fulfill the number of your days.

Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao. Kutoka 23:27

I will send my terror before you, and will confuse all the people to whom you come, and I will make all your enemies turn their backs to you.

Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako. Kutoka 23:28

I will send the hornet before you, which will drive out the Hivite, the Canaanite, and the Hittite, from before you.

Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. Kutoka 23:29

I will not drive them out from before you in one year, lest the land become desolate, and the animals of the field multiply against you.

Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi. Kutoka 23:30

Little by little I will drive them out from before you, until you have increased and inherit the land.

Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hata bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako. Kutoka 23:31

I will set your border from the Red Sea even to the sea of the Philistines, and from the wilderness to the River; for I will deliver the inhabitants of the land into your hand, and you shall drive them out before you.

Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao. Kutoka 23:32

You shall make no covenant with them, nor with their gods.

Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni tanzi kwako.

Kutoka 23:33

They shall not dwell in your land, lest they make you sin against me, for if you serve their gods, it will surely be a snare to you."