Kutoka 27 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 27 (Swahili) Exodus 27 (English)

Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita; urefu wake utakuwa ni dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano; hiyo madhabahu itakuwa mraba; na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu. Kutoka 27:1

"You shall make the altar of acacia wood, five cubits long, and five cubits broad; the altar shall be foursquare: and its height shall be three cubits.

Nawe fanya pembe nne katika pembe zake nne; hizo pembe zitakuwa za kitu kimoja na madhabahu; nawe utayafunika shaba. Kutoka 27:2

You shall make its horns on its four corners; its horns shall be of one piece with it; and you shall overlay it with brass.

Na vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake; vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba. Kutoka 27:3

You shall make its pots to take away its ashes, its shovels, its basins, its flesh hooks, and its fire pans: all its vessels you shall make of brass.

Nawe uifanyie hiyo madhabahu wavu wa shaba; kisha utie pete nne za shaba katika hizo pembe nne za ule wavu. Kutoka 27:4

You shall make a grating for it of network of brass: and on the net you shall make four brazen rings in its four corners.

Nawe tia huo wavu chini ya kizingo kiizungukacho madhabahu upande wa chini, ili huo wavu ufikilie katikati ya hiyo madhabahu. Kutoka 27:5

You shall put it under the ledge around the altar beneath, that the net may reach halfway up the altar.

Nawe fanya miti kwa ajili ya madhabahu, miti ya mshita, na kuifunika shaba. Kutoka 27:6

You shall make poles for the altar, poles of acacia wood, and overlay them with brass.

Na hiyo miti itatiwa katika pete, na ile miti itakuwa katika pande mbili za madhabahu, wakati wa kuichukua. Kutoka 27:7

Its poles shall be put into the rings, and the poles shall be on the two sides of the altar, when carrying it.

Uifanye ya mbao, yenye mvungu ndani yake; kama ulivyoonyeshwa mlimani, ndivyo watakavyoifanya. Kutoka 27:8

Hollow with planks shall you make it: as it has been shown you on the mountain, so shall they make it.

Nawe fanya ua wa maskani; upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia; Kutoka 27:9

"You shall make the court of the tent: for the south side southward there shall be hangings for the court of fine twined linen one hundred cubits long for one side:

na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na matako yake ishirini, matako yake yatakuwa ya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha. Kutoka 27:10

and the pillars of it shall be twenty, and their sockets twenty, of brass; the hooks of the pillars and their fillets shall be of silver.

Ni vivyo upande wa kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia, na nguzo zake ishirini, na matako yake ishirini yatakuwa ya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha. Kutoka 27:11

Likewise for the north side in length there shall be hangings one hundred cubits long, and the pillars of it twenty, and their sockets twenty, of brass; the hooks of the pillars, and their fillets, of silver.

Na upande wa magharibi, upana wa ua kutakuwa na chandarua ya dhiraa hamsini; nguzo zake kumi, na matako yake kumi. Kutoka 27:12

For the breadth of the court on the west side shall be hangings of fifty cubits; their pillars ten, and their sockets ten.

Na upana wa ule ua upande wa mashariki kuelekea mashariki utakuwa ni dhiraa hamsini. Kutoka 27:13

The breadth of the court on the east side eastward shall be fifty cubits.

Chandarua upande mmoja wa lango itakuwa dhiraa kumi na tano upana wake; nguzo zake zitakuwa tatu na matako yake matatu. Kutoka 27:14

The hangings for the one side of the gate shall be fifteen cubits; their pillars three, and their sockets three.

Upande wa pili ni vivyo chandarua ya dhiraa kumi na tano; nguzo zake tatu, na matako yake matatu. Kutoka 27:15

For the other side shall be hangings of fifteen cubits; their pillars three, and their sockets three.

Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshona taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na matako yake manne. Kutoka 27:16

For the gate of the court shall be a screen of twenty cubits, of blue, and purple, and scarlet, and fine twined linen, the work of the embroiderer; their pillars four, and their sockets four.

Nguzo zote za ule ua ziuzungukazo pande zote zitakuwa na vitanzi vya fedha; kulabu zake za fedha, na matako yake ya shaba. Kutoka 27:17

All the pillars of the court round about shall be filleted with silver; their hooks of silver, and their sockets of brass.

Urefu wa huo ua utakuwa dhiraa mia, na upana wake utakuwa dhiraa hamsini kotekote, na kwenda juu kwake dhiraa tano; yawe ya nguo ya kitani nzuri, na matako yake yatakuwa ya shaba. Kutoka 27:18

The length of the court shall be one hundred cubits, and the breadth fifty every where, and the height five cubits, of fine twined linen, and their sockets of brass.

Vyombo vyote vya maskani vitumiwavyo katika utumishi wake wote, na vigingi vyake vyote, na vigingi vyote vya ule ua, vitakuwa vya shaba. Kutoka 27:19

All the instruments of the tent in all its service, and all the pins of it, and all the pins of the court, shall be of brass.

Nawe waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima. Kutoka 27:20

"You shall command the children of Israel, that they bring to you pure olive oil beaten for the light, to cause a lamp to burn continually.

Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hata asubuhi mbele ya Bwana; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.

Kutoka 27:21

In the tent of meeting, outside the veil which is before the testimony, Aaron and his sons shall keep it in order from evening to morning before Yahweh: it shall be a statute forever throughout their generations on the behalf of the children of Israel.