Kutoka 26 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 26 (Swahili) Exodus 26 (English)

Kisha fanya hiyo maskani iwe na mapazia kumi; ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya samawi, na ya zambarau, na nyekundu, pamoja na makerubi; kazi ya fundi stadi. Kutoka 26:1

"Moreover you shall make the tent with ten curtains; of fine twined linen, and blue, and purple, and scarlet, with cherubim. The work of the skillful workman you shall make them.

Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa ishirini na nane, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne; mapazia yote yatakuwa ya kipimo kimoja. Kutoka 26:2

The length of each curtain shall be twenty-eight cubits, and the breadth of each curtain four cubits: all the curtains shall have one measure.

Mapazia matano yataungwa pamoja, hili na hili; na mapazia matano mengine yataungwa pamoja, hili na hili. Kutoka 26:3

Five curtains shall be coupled together one to another; and the other five curtains shall be coupled one to another.

Kisha utafanya tanzi za rangi ya samawi upande wa mwisho wa pazia moja katika ule upindo wa fungu lake, vivyo utafanya upande wa mwisho wa ile pazia iliyo, katika fungu la pili. Kutoka 26:4

You shall make loops of blue on the edge of the one curtain from the edge in the coupling; and likewise shall you make in the edge of the curtain that is outmost in the second coupling.

Fanya matanzi hamsini katika pazia moja, na matanzi hamsini katika upande wa mwisho wa ile pazia iliyo katika kuungana kwa pili; hizo tanzi zitaelekeana. Kutoka 26:5

You shall make fifty loops in the one curtain, and you shall make fifty loops in the edge of the curtain that is in the second coupling. The loops shall be opposite one to another.

Kisha ufanye vifungo hamsini vya dhahabu, na kuunganya hayo mapazia pamoja kwa vile vifungo; na hiyo maskani itakuwa ni moja. Kutoka 26:6

You shall make fifty clasps of gold, and couple the curtains one to another with the clasps: and the tent shall be a unit.

Nawe fanya mapazia ya singa za mbuzi yawe hema juu ya maskani; fanya mapazia kumi na moja. Kutoka 26:7

"You shall make curtains of goats' hair for a covering over the tent: eleven curtains shall you make them.

Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa thelathini, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne; hayo mapazia kumi na moja yatakuwa ya kipimo kimoja. Kutoka 26:8

The length of each curtain shall be thirty cubits, and the breadth of each curtain four cubits: the eleven curtains shall have one measure.

Kisha utaunganya mapazia matano mbali, na mapazia sita mbali, na lile pazia la sita utalipeta hapo upande wa mbele wa ile hema. Kutoka 26:9

You shall couple five curtains by themselves, and six curtains by themselves, and shall double over the sixth curtain in the forefront of the tent.

Fanya tanzi hamsini upande wa mwisho wa pazia lile lililo la mwisho katika hayo yaliyounganywa pamoja, na tanzi hamsini upande wa mwisho wa lile pazia lililo nje katika hayo ya pili yaliyounganywa pamoja. Kutoka 26:10

You shall make fifty loops on the edge of the one curtain that is outmost in the coupling, and fifty loops on the edge of the curtain which is outmost in the second coupling.

Tena ufanye vifungo hamsini vya shaba, na kuvitia vile vifungo katika zile tanzi, na kuiunganya ile hema pamoja, ili iwe hema moja. Kutoka 26:11

You shall make fifty clasps of brass, and put the clasps into the loops, and couple the tent together, that it may be one.

Na kipande kile kilichosalia, kile kiangukacho, cha yale mapazia ya hema, ile nusu ya pazia iliyosalia, itaanguka huko upande wa nyuma wa maskani. Kutoka 26:12

The overhanging part that remains of the curtains of the tent, the half curtain that remains, shall hang over the back of the tent.

Na hiyo dhiraa moja upande mmoja, na ile dhiraa moja upande wa pili, ya urefu wa mapazia ya hema uliosalia, zitaanguka katika ubavu wa maskani upande huu na upande huu, ili kuifunika. Kutoka 26:13

The cubit on the one side, and the cubit on the other side, of that which remains in the length of the curtains of the tent, shall hang over the sides of the tent on this side and on that side, to cover it.

Nawe fanya kifuniko cha ile hema, cha ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo. Kutoka 26:14

You shall make a covering for the tent of rams' skins dyed red, and a covering of sea cow hides above.

Nawe fanya hizo mbao za maskani za mti wa mshita, zenye kusimama. Kutoka 26:15

"You shall make the boards for the tent of acacia wood, standing up.

Kila ubao utakuwa na urefu wa dhiraa kumi, na upana wake kila ubao utakuwa dhiraa moja na nusu. Kutoka 26:16

Ten cubits shall be the length of a board, and one and a half cubits the breadth of each board.

Kila ubao utakuwa na ndimi mbili, zenye kuunganywa huu na huu; ndivyo utakavyozifanya mbao zote za maskani. Kutoka 26:17

There shall be two tenons in each board, joined to one another: thus shall you make for all the boards of the tent.

Kisha ufanye zile mbao za maskani, mbao ishirini kwa upande wa kusini kuelekea kusini. Kutoka 26:18

You shall make the boards for the tent, twenty boards for the south side southward.

Nawe ufanye matako arobaini ya fedha chini ya zile mbao ishirini, matako mawili chini ya ubao mmoja, kupokea zile ndimi zake mbili, na matako mawili chini ya ubao mwingine kupokea zile ndimi zake mbili; Kutoka 26:19

You shall make forty sockets of silver under the twenty boards; two sockets under one board for its two tenons, and two sockets under another board for its two tenons.

na upande wa pili wa maskani, upande wa kaskazini, mbao ishirini; Kutoka 26:20

For the second side of the tent, on the north side, twenty boards,

na matako yake ya fedha arobaini; matako mawili chini ya ubao mmoja, na matako mawili chini ya ubao mwingine. Kutoka 26:21

and their forty sockets of silver; two sockets under one board, and two sockets under another board.

Kisha ufanye mbao sita kwa ajili ya upande wa nyuma wa maskani kuelekea magharibi. Kutoka 26:22

For the far part of the tent westward you shall make six boards.

Tena ufanye mbao mbili kwa ajili ya hizo pembe za maskani zilizo upande wa nyuma. Kutoka 26:23

Two boards shall you make for the corners of the tent in the far part.

Upande wa chini zitakuwa ni mbili mbili; vivyo zitaungwa pamoja mbao pacha hata ncha ya juu katika pete ya kwanza; zote mbili ndivyo zitakavyokuwa; zitakuwa kwa ajili ya hizo pembe mbili. Kutoka 26:24

They shall be double beneath, and in like manner they shall be entire to the top of it to one ring: thus shall it be for them both; they shall be for the two corners.

Mbao zitakuwa ni nane, na matako yake ya fedha, matako kumi na sita; matako mawili chini ya ubao mmoja, na matako mawili chini ya ubao wa pili. Kutoka 26:25

There shall be eight boards, and their sockets of silver, sixteen sockets; two sockets under one board, and two sockets under another board.

Nawe fanya mataruma ya mti wa mshita; mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande mmoja wa maskani, Kutoka 26:26

"You shall make bars of acacia wood: five for the boards of the one side of the tent,

na mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande wa pili wa maskani, na mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande wa maskani ulio nyuma kuelekea magharibi. Kutoka 26:27

and five bars for the boards of the other side of the tent, and five bars for the boards of the side of the tent, for the far part westward.

Na hilo taruma la katikati, lililo katikati ya zile mbao litapenya toka mwisho huu hata mwisho huu. Kutoka 26:28

The middle bar in the midst of the boards shall pass through from end to end.

Na hizo mbao utazifunika dhahabu, na pete zake za kutilia yale mataruma utazifanya za dhahabu; na hayo mataruma utayafunika dhahabu. Kutoka 26:29

You shall overlay the boards with gold, and make their rings of gold for places for the bars: and you shall overlay the bars with gold.

Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake ulioonyeshwa mlimani. Kutoka 26:30

You shall set up the tent according to the way that it was shown to you on the mountain.

Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi; Kutoka 26:31

"You shall make a veil of blue, and purple, and scarlet, and fine twined linen, with cherubim. The work of the skillful workman shall it be made.

kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika matako ya fedha manne. Kutoka 26:32

You shall hang it on four pillars of acacia overlaid with gold; their hooks shall be of gold, on four sockets of silver.

Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana. Kutoka 26:33

You shall hang up the veil under the clasps, and shall bring the ark of the testimony in there within the veil: and the veil shall separate the holy place from the most holy for you.

Nawe utaweka kiti cha rehema juu ya lile sanduku la ushuhuda ndani ya mahali pale patakatifu sana. Kutoka 26:34

You shall put the mercy seat on the ark of the testimony in the most holy place.

Na ile meza utaiweka nje ya pazia, na kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini; na ile meza utaiweka upande wa kaskazini. Kutoka 26:35

You shall set the table outside the veil, and the lampstand over against the table on the side of the tent toward the south: and you shall put the table on the north side.

Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa Hema, cha nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshona taraza. Kutoka 26:36

"You shall make a screen for the door of the Tent, of blue, and purple, and scarlet, and fine twined linen, the work of the embroiderer.

Nawe fanya nguzo tano za mti wa mshita kwa kile kisitiri, na kuzifunika dhahabu; kulabu zake zitakuwa za dhahabu; nawe utasubu matako ya shaba matano kwa ajili yake.

Kutoka 26:37

You shall make for the screen five pillars of acacia, and overlay them with gold: their hooks shall be of gold: and you shall cast five sockets of brass for them.