Matendo ya Mitume 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 16 (Swahili) Acts 16 (English)

Basi akafika Derbe na Listra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Myunani. Matendo ya Mitume 16:1

He came to Derbe and Lystra: and behold, a certain disciple was there, named Timothy, the son of a Jewess who believed; but his father was a Greek.

Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio. Matendo ya Mitume 16:2

The brothers who were at Lystra and Iconium gave a good testimony about him.

Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani. Matendo ya Mitume 16:3

Paul wanted to have him go out with him, and he took and circumcised him because of the Jews who were in those parts; for they all knew that his father was a Greek.

Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike. Matendo ya Mitume 16:4

As they went on their way through the cities, they delivered the decrees to them to keep which had been ordained by the apostles and elders who were at Jerusalem.

Makanisa yakatiwa nguvu katika ile Imani, hesabu yao ikaongezeka kila siku. Matendo ya Mitume 16:5

So the assemblies were strengthened in the faith, and increased in number daily.

Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. Matendo ya Mitume 16:6

When they had gone through the region of Phrygia and Galatia, they were forbidden by the Holy Spirit to speak the word in Asia.

Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, Matendo ya Mitume 16:7

When they had come opposite Mysia, they tried to go into Bithynia, but the Spirit didn't allow them.

wakapita Misia wakatelemkia Troa. Matendo ya Mitume 16:8

Passing by Mysia, they came down to Troas.

Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. Matendo ya Mitume 16:9

A vision appeared to Paul in the night. There was a man of Macedonia standing, begging him, and saying, "Come over into Macedonia and help us."

Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema. Matendo ya Mitume 16:10

When he had seen the vision, immediately we sought to go out to Macedonia, concluding that the Lord had called us to preach the Gospel to them.

Basi tukang'oa nanga kutoka Troa, tukafika Samothrake kwa tanga moja, na siku ya pili tukafika Neapoli; Matendo ya Mitume 16:11

Setting sail therefore from Troas, we made a straight course to Samothrace, and the day following to Neapolis;

na kutoka hapo tukafika Filipi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika jimbo lile, mahali walipohamia Warumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha. Matendo ya Mitume 16:12

and from there to Philippi, which is a city of Macedonia, the foremost of the district, a Roman colony. We were staying some days in this city.

Hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale. Matendo ya Mitume 16:13

On the Sabbath day we went forth outside of the city by a riverside, where we supposed there was a place of prayer, and we sat down, and spoke to the women who had come together.

Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo. Matendo ya Mitume 16:14

A certain woman named Lydia, a seller of purple, of the city of Thyatira, one who worshiped God, heard us; whose heart the Lord opened to listen to the things which were spoken by Paul.

Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatushurutisha. Matendo ya Mitume 16:15

When she and her household were baptized, she begged us, saying, "If you have judged me to be faithful to the Lord, come into my house, and stay." So she persuaded us.

Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Matendo ya Mitume 16:16

It happened, as we were going to prayer, that a certain girl having a spirit of divination met us, who brought her masters much gain by fortune telling.

Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. Matendo ya Mitume 16:17

Following Paul and us, she cried out, "These men are servants of the Most High God, who proclaim to us the way of salvation!"

Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. Matendo ya Mitume 16:18

She was doing this for many days. But Paul, becoming greatly annoyed, turned and said to the spirit, "I charge you in the name of Jesus Christ to come out of her!" It came out that very hour.

Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji; Matendo ya Mitume 16:19

But when her masters saw that the hope of their gain was gone, they seized Paul and Silas, and dragged them into the marketplace before the rulers.

wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanachafua sana mji wetu, nao ni Wayahudi; Matendo ya Mitume 16:20

When they had brought them to the magistrates, they said, "These men, being Jews, are agitating our city,

tena wanatangaza habari ya desturi zisizokuwa halali kwetu kuzipokea wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi. Matendo ya Mitume 16:21

and set forth customs which it is not lawful for us to accept or to observe, being Romans."

Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora. Matendo ya Mitume 16:22

The multitude rose up together against them, and the magistrates tore their clothes off of them, and commanded them to be beaten with rods.

Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. Matendo ya Mitume 16:23

When they had laid many stripes on them, they threw them into prison, charging the jailer to keep them safely,

Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. Matendo ya Mitume 16:24

who, having received such a charge, threw them into the inner prison, and secured their feet in the stocks.

Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Matendo ya Mitume 16:25

But about midnight Paul and Silas were praying and singing hymns to God, and the prisoners were listening to them.

Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. Matendo ya Mitume 16:26

Suddenly there was a great earthquake, so that the foundations of the prison were shaken; and immediately all the doors were opened, and everyone's bonds were loosened.

Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia. Matendo ya Mitume 16:27

The jailer, being roused out of sleep and seeing the prison doors open, drew his sword and was about to kill himself, supposing that the prisoners had escaped.

Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa. Matendo ya Mitume 16:28

But Paul cried with a loud voice, saying, "Don't harm yourself, for we are all here!"

Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; Matendo ya Mitume 16:29

He called for lights and sprang in, and, fell down trembling before Paul and Silas,

kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Matendo ya Mitume 16:30

and brought them out and said, "Sirs, what must I do to be saved?"

Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. Matendo ya Mitume 16:31

They said, "Believe in the Lord Jesus Christ, and you will be saved, you and your household."

Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. Matendo ya Mitume 16:32

They spoke the word of the Lord to him, and to all who were in his house.

Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo. Matendo ya Mitume 16:33

He took them the same hour of the night, and washed their stripes, and was immediately baptized, he and all his household.

Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu. Matendo ya Mitume 16:34

He brought them up into his house, and set food before them, and rejoiced greatly, with all his household, having believed in God.

Kulipopambauka makadhi wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao. Matendo ya Mitume 16:35

But when it was day, the magistrates sent the sergeants, saying, "Let those men go."

Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paulo maneno haya akisema, Makadhi wametuma watu ili mfunguliwe; basi, sasa tokeni nje, enendeni zenu kwa amani. Matendo ya Mitume 16:36

The jailer reported these words to Paul, saying, "The magistrates have sent to let you go; now therefore come out, and go in peace."

Paulo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, tena wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? Sivyo, lakini na waje wenyewe wakatutoe. Matendo ya Mitume 16:37

But Paul said to them, "They have beaten us publicly, without a trial, men who are Romans, and have cast us into prison! Do they now release us secretly? No, most assuredly, but let them come themselves and bring us out!"

Wakubwa wa askari wakawapasha makadhi habari za maneno haya; nao wakaogopa, waliposikia ya kwamba hao ni Warumi. Matendo ya Mitume 16:38

The sergeants reported these words to the magistrates, and they were afraid when they heard that they were Romans,

Wakaja wakawasihi; na walipokwisha kuwatoa nje, wakawaomba watoke katika mji ule. Matendo ya Mitume 16:39

and they came and begged them. When they had brought them out, they asked them to depart from the city.

Nao wakatoka gerezani wakaingia nyumbani mwa Lidia; na walipokwisha kuonana na ndugu wakawafariji, wakaenda zao. Matendo ya Mitume 16:40

They went out of the prison, and entered into Lydia's house. When they had seen the brothers, they encouraged them, and departed.