Matendo ya Mitume 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 3 (Swahili) Acts 3 (English)

Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa. Matendo ya Mitume 3:1

Peter and John were going up into the temple at the hour of prayer, the ninth hour{3:00 PM}.

Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu. Matendo ya Mitume 3:2

A certain man who was lame from his mother's womb was being carried, whom they laid daily at the door of the temple which is called Beautiful, to ask gifts for the needy of those who entered into the temple.

Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. Matendo ya Mitume 3:3

Seeing Peter and John about to go into the temple, he asked to receive gifts for the needy.

Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. Matendo ya Mitume 3:4

Peter, fastening his eyes on him, with John, said, "Look at us."

Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao. Matendo ya Mitume 3:5

He listened to them, expecting to receive something from them.

Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende. Matendo ya Mitume 3:6

But Peter said, "Silver and gold have I none, but what I have, that I give you. In the name of Jesus Christ of Nazareth, get up and walk!"

Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Matendo ya Mitume 3:7

He took him by the right hand, and raised him up. Immediately his feet and his ankle bones received strength.

Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu. Matendo ya Mitume 3:8

Leaping up, he stood, and began to walk. He entered with them into the temple, walking, leaping, and praising God.

Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu. Matendo ya Mitume 3:9

All the people saw him walking and praising God.

Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango Mzuri wa hekalu; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata. Matendo ya Mitume 3:10

They recognized him, that it was he who used to sit begging for gifts for the needy at the Beautiful Gate of the temple. They were filled with wonder and amazement at what had happened to him.

Basi alipokuwa akiwashika Petro na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika tao lile lililoitwa tao la Sulemani, wakishangaa sana. Matendo ya Mitume 3:11

As the lame man who was healed held on to Peter and John, all the people ran together to them in the porch that is called Solomon's, greatly wondering.

Hata Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi? Matendo ya Mitume 3:12

When Peter saw it, he responded to the people, "You men of Israel, why do you marvel at this man? Why do you fasten your eyes on us, as though by our own power or godliness we had made him walk?

Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe. Matendo ya Mitume 3:13

The God of Abraham, Isaac, and Jacob, the God of our fathers, has glorified his Servant Jesus, whom you delivered up, and denied in the presence of Pilate, when he had determined to release him.

Bali ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe mwuaji; Matendo ya Mitume 3:14

But you denied the Holy and Righteous One, and asked for a murderer to be granted to you,

mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu; na sisi tu mashahidi wake. Matendo ya Mitume 3:15

and killed the Prince of life, whom God raised from the dead, to which we are witnesses.

Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote. Matendo ya Mitume 3:16

By faith in his name has his name made this man strong, whom you see and know. Yes, the faith which is through him has given him this perfect soundness in the presence of you all.

Basi sasa, ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda. Matendo ya Mitume 3:17

"Now, brothers{The word for "brothers" here may be also correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."}, I know that you did this in ignorance, as did also your rulers.

Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo. Matendo ya Mitume 3:18

But the things which God announced by the mouth of all his prophets, that Christ should suffer, he thus fulfilled.

Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; Matendo ya Mitume 3:19

"Repent therefore, and turn again, that your sins may be blotted out, so that there may come times of refreshing from the presence of the Lord,

apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani; Matendo ya Mitume 3:20

and that he may send Christ Jesus, who was ordained for you before,

ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu. Matendo ya Mitume 3:21

whom heaven must receive until the times of restoration of all things, which God spoke long ago by the mouth of his holy prophets.

Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi. Matendo ya Mitume 3:22

For Moses indeed said to the fathers, 'The Lord God will raise up a prophet for you from among your brothers, like me. You shall listen to him in all things whatever he says to you.

Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake. Matendo ya Mitume 3:23

It will be, that every soul that will not listen to that prophet will be utterly destroyed from among the people.'

Naam, na manabii wote tangu Samweli na wale waliokuja baada yake, wote walionena, walihubiri habari za siku hizi. Matendo ya Mitume 3:24

Yes, and all the prophets from Samuel and those who followed after, as many as have spoken, they also told of these days.

Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa. Matendo ya Mitume 3:25

You are the children of the prophets, and of the covenant which God made with our fathers, saying to Abraham, 'In your seed will all the families of the earth be blessed.'

Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake. Matendo ya Mitume 3:26

God, having raised up his servant, Jesus, sent him to you first, to bless you, in turning away everyone of you from your wickedness."