Matendo ya Mitume 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 15 (Swahili) Acts 15 (English)

Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka. Matendo ya Mitume 15:1

Some men came down from Judea and taught the brothers, "Unless you are circumcised after the custom of Moses, you can't be saved."

Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo. Matendo ya Mitume 15:2

Therefore when Paul and Barnabas had no small discord and discussion with them, they appointed Paul and Barnabas, and some others of them, to go up to Jerusalem to the apostles and elders about this question.

Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana. Matendo ya Mitume 15:3

They, being sent on their way by the assembly, passed through both Phoenicia and Samaria, declaring the conversion of the Gentiles. They caused great joy to all the brothers.{The word for "brothers" here and where the context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."}

Walipofika Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao. Matendo ya Mitume 15:4

When they had come to Jerusalem, they were received by the assembly and the apostles and the elders, and they reported all things that God had done with them.

Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa. Matendo ya Mitume 15:5

But some of the sect of the Pharisees who believed rose up, saying, "It is necessary to circumcise them, and to charge them to keep the law of Moses."

Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo. Matendo ya Mitume 15:6

The apostles and the elders were gathered together to see about this matter.

Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini. Matendo ya Mitume 15:7

When there had been much discussion, Peter rose up and said to them, "Brothers, you know that a good while ago God made choice among you, that by my mouth the Gentiles should hear the word of the Gospel, and believe.

Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi; Matendo ya Mitume 15:8

God, who knows the heart, testified about them, giving them the Holy Spirit, just like he did to us.

wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani. Matendo ya Mitume 15:9

He made no distinction between us and them, cleansing their hearts by faith.

Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua. Matendo ya Mitume 15:10

Now therefore why do you tempt God, that you should put a yoke on the neck of the disciples which neither our fathers nor we were able to bear?

Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao. Matendo ya Mitume 15:11

But we believe that we are saved through the grace of the Lord Jesus,{TR adds "Christ"} just as they are."

Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa. Matendo ya Mitume 15:12

All the multitude kept silence, and they listened to Barnabas and Paul reporting what signs and wonders God had done among the Gentiles through them.

Na hao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akisema, Ndugu zangu, nisikilizeni. Matendo ya Mitume 15:13

After they were silent, James answered, "Brothers, listen to me.

Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake. Matendo ya Mitume 15:14

Simeon has reported how God first visited the Gentiles, to take out of them a people for his name.

Na maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa, Matendo ya Mitume 15:15

This agrees with the words of the prophets. As it is written,

Baada ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha; Matendo ya Mitume 15:16

'After these things I will return. I will again build the tent of David, which has fallen. I will again build its ruins. I will set it up,

Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao; Matendo ya Mitume 15:17

That the rest of men may seek after the Lord; All the Gentiles who are called by my name, Says the Lord, who does all these things.

Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele. Matendo ya Mitume 15:18

All his works are known to God from eternity.'

Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa; Matendo ya Mitume 15:19

"Therefore my judgment is that we don't trouble those from among the Gentiles who turn to God,

bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu. Matendo ya Mitume 15:20

but that we write to them that they abstain from the pollution of idols, from sexual immorality, from what is strangled, and from blood.

Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi. Matendo ya Mitume 15:21

For Moses from generations of old has in every city those who preach him, being read in the synagogues every Sabbath."

Basi ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na kupeleka kwa mikono yao, Matendo ya Mitume 15:22

Then it seemed good to the apostles and the elders, with the whole assembly, to choose men out of their company, and send them to Antioch with Paul and Barnabas: Judas called Barsabbas, and Silas, chief men among the brothers.{The word for "brothers" here and where the context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."}

Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu. Matendo ya Mitume 15:23

They wrote these things by their hand: "The apostles, the elders, and the brothers, to the brothers who are of the Gentiles in Antioch, Syria, and Cilicia: greetings.

Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbua kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, ambao sisi hatukuwaagiza; Matendo ya Mitume 15:24

Because we have heard that some who went out from us have troubled you with words, unsettling your souls, saying, 'You must be circumcised and keep the law,' to whom we gave no commandment;

sisi tumeona vema, hali tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo, Matendo ya Mitume 15:25

it seemed good to us, having come to one accord, to choose out men and send them to you with our beloved Barnabas and Paul,

watu waliohatirisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Matendo ya Mitume 15:26

men who have risked their lives for the name of our Lord Jesus Christ.

Basi tumewatuma Yuda na Sila, watakaowaambia wenyewe maneno yayo hayo kwa vinywa vyao. Matendo ya Mitume 15:27

We have sent therefore Judas and Silas, who themselves will also tell you the same things by word of mouth.

Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, Matendo ya Mitume 15:28

For it seemed good to the Holy Spirit, and to us, to lay no greater burden on you than these necessary things:

yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu. Matendo ya Mitume 15:29

that you abstain from things sacrificed to idols, from blood, from things strangled, and from sexual immorality, from which if you keep yourselves, it will be well with you. Farewell."

Hata hao wakiisha kupewa ruhusa wakatelemkia Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii yote wakawapa ile barua. Matendo ya Mitume 15:30

So, when they were sent off, they came to Antioch. Having gathered the multitude together, they delivered the letter.

Nao walipokwisha kuisoma wakafurahi kwa ajili ya faraja ile. Matendo ya Mitume 15:31

When they had read it, they rejoiced over the encouragement.

Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathibitisha. Matendo ya Mitume 15:32

Judas and Silas, also being prophets themselves, encouraged the brothers with many words, and strengthened them.

Na wakiisha kukaa huko muda, wakaruhusiwa na ndugu waende kwa amani kwa hao waliowatuma. [ Matendo ya Mitume 15:33

After they had spent some time there, they were sent back with greetings from the brothers to the apostles.

Lakini Sila akaona vema kukaa huko.] Matendo ya Mitume 15:34

{Some manuscripts add: But it seemed good to Silas to stay there.}

Na Paulo na Barnaba wakakaa huko Antiokia, wakifundisha na kulihubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi. Matendo ya Mitume 15:35

But Paul and Barnabas stayed in Antioch, teaching and preaching the word of the Lord, with many others also.

Baada ya siku kadha wa kadha Paulo akamwambia Barnaba, Haya! Mrejee sasa tukawaangalie hao ndugu katika kila mji tulipolihubiri neno la Bwana, wa hali gani. Matendo ya Mitume 15:36

After some days Paul said to Barnabas, "Let's return now and visit our brothers in every city in which we proclaimed the word of the Lord, to see how they are doing."

Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao. Matendo ya Mitume 15:37

Barnabas planned to take John, who was called Mark, with them also.

Bali Paulo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfilia, asiende nao kazini. Matendo ya Mitume 15:38

But Paul didn't think that it was a good idea to take with them someone who had withdrawn from them in Pamphylia, and didn't go with them to do the work.

Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kipro. Matendo ya Mitume 15:39

Then the contention grew so sharp that they separated from each other. Barnabas took Mark with him, and sailed away to Cyprus,

Lakini Paulo akamchagua Sila, akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana. Matendo ya Mitume 15:40

but Paul chose Silas, and went out, being commended by the brothers to the grace of God.

Akapita katika Shamu na Kilikia akiyathibitisha makanisa. Matendo ya Mitume 15:41

He went through Syria and Cilicia, strengthening the assemblies.