Matendo ya Mitume 27 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 27 (Swahili) Acts 27 (English)

Basi ilipoamriwa tuabiri hata Italia, wakamtia Paulo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto. Matendo ya Mitume 27:1

When it was determined that we should sail for Italy, they delivered Paul and certain other prisoners to a centurion named Julius, of the Augustan band.

Tukapanda katika merikebu ya Adramitio iliyokuwa tayari kusafiri mpaka miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedonia wa Thesalonike, akiwa pamoja nasi. Matendo ya Mitume 27:2

Embarking in a ship of Adramyttium, which was about to sail to places on the coast of Asia, we put to sea; Aristarchus, a Macedonian of Thessalonica, being with us.

Siku ya pili tukawasili Sidoni; Yulio akamfadhili sana Paulo akampa ruhusa kwenda kwa rafiki zake, apate kutunzwa. Matendo ya Mitume 27:3

The next day, we touched at Sidon. Julius treated Paul kindly, and gave him permission to go to his friends and refresh himself.

Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kipro ili kuukinga upepo, kwa maana pepo zilikuwa za mbisho. Matendo ya Mitume 27:4

Putting to sea from there, we sailed under the lee of Cyprus, because the winds were contrary.

Tulipopita bahari ya upande wa Kilikia na Pamfilia, tukafika Mira, mji wa Likia. Matendo ya Mitume 27:5

When we had sailed across the sea which is off Cilicia and Pamphylia, we came to Myra, a city of Lycia.

Na huko yule akida akakuta merikebu ya Iskanderia, tayari kusafiri kwenda Italia, akatupandisha humo. Matendo ya Mitume 27:6

There the centurion found a ship of Alexandria sailing for Italy, and he put us on board.

Tukasafiri polepole kwa muda wa siku nyingi, tukafika mpaka Nido kwa shida; na kwa sababu upepo ulikuwa ukituzuia tukapita chini ya Krete, tukaikabili Salmone. Matendo ya Mitume 27:7

When we had sailed slowly many days, and had come with difficulty opposite Cnidus, the wind not allowing us further, we sailed under the lee of Crete, opposite Salmone.

Tukaipita kwa shida, pwani kwa pwani, tukafika mahali paitwapo Bandari Nzuri. Karibu na hapo pana mji uitwao Lasea. Matendo ya Mitume 27:8

With difficulty sailing along it we came to a certain place called Fair Havens, near the city of Lasea.

Na wakati mwingi ulipokwisha kupita, na safari ikiwa ina hatari sasa, kwa sababu siku za kufunga zilikuwa zimekwisha kupita, Paulo akawaonya, Matendo ya Mitume 27:9

When much time had passed and the voyage was now dangerous, because the Fast had now already gone by, Paul admonished them,

akawaambia, Wanaume, naona kwamba safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia. Matendo ya Mitume 27:10

and said to them, "Sirs, I perceive that the voyage will be with injury and much loss, not only of the cargo and the ship, but also of our lives."

Lakini yule akida akawasikiliza nahodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyoyasema Paulo. Matendo ya Mitume 27:11

But the centurion gave more heed to the master and to the owner of the ship than to those things which were spoken by Paul.

Na kwa sababu bandari ile ilikuwa haifai kukaa wakati wa baridi, wengi wao wakatoa shauri la kutweka kutoka huko ili wapate kufika Foinike, kama ikiwezekana, na kukaa huko wakati wa baridi; nayo ni bandari ya Krete, inaelekea kaskazini-mashariki na kusini-mashariki. Matendo ya Mitume 27:12

Because the haven was not suitable to winter in, the majority advised going to sea from there, if by any means they could reach Phoenix, and winter there, which is a port of Crete, looking northeast and southeast.

Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata waliyoazimu kupata, wakang'oa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani. Matendo ya Mitume 27:13

When the south wind blew softly, supposing that they had obtained their purpose, they weighed anchor and sailed along Crete, close to shore.

Baada ya muda mchache ukavuma upepo wa nguvu wa namna ya tufani, uitwao Eurakilo, Matendo ya Mitume 27:14

But before long, a tempestuous wind beat down from shore, which is called Euroclydon.{Or, "a northeaster."}

merikebu iliposhikwa, na kutoweza kushindana na upepo, tukaiacha tukachukuliwa. Matendo ya Mitume 27:15

When the ship was caught, and couldn't face the wind, we gave way to it, and were driven along.

Na tukipita upesi karibu na kisiwa kidogo kiitwacho Kauda tukadiriki kuikweza mashua; lakini kwa shida. Matendo ya Mitume 27:16

Running under the lee of a small island called Clauda, we were able, with difficulty, to secure the boat.

Walipokwisha kuikweza wakatumia misaada, wakaikaza merikebu kwa kupitisha kamba chini yake, nao wakiogopa wasije wakakwama katika fungu liitwalo Sirti, wakatua matanga wakachukuliwa vivi hivi. Matendo ya Mitume 27:17

After they had hoisted it up, they used cables to help reinforce the ship. Fearing that they would run aground on the Syrtis sand bars, they lowered the sea anchor, and so were driven along.

Na kwa maana tulikuwa tukipigwa sana na ile tufani, siku ya pili yake wakaanza kuitupa shehena baharini. Matendo ya Mitume 27:18

As we labored exceedingly with the storm, the next day they began to throw things overboard.

Siku ya tatu wakatupa vyombo vya merikebu kwa mikono yao wenyewe. Matendo ya Mitume 27:19

On the third day, they threw out the ship's tackle with their own hands.

Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka. Matendo ya Mitume 27:20

When neither sun nor stars shone on us for many days, and no small tempest pressed on us, all hope that we would be saved was now taken away.

Na walipokuwa wamekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paulo akasimama katikati yao, akasema, Wanaume, iliwapasa kunisikiliza mimi na kutokung'oa nanga huko Krete, na kupata madhara haya na hasara hii. Matendo ya Mitume 27:21

When they had been long without food, Paul stood up in the middle of them, and said, "Sirs, you should have listened to me, and not have set sail from Crete, and have gotten this injury and loss.

Sasa nawapeni shauri, iweni na moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu atakayepotea, ila merikebu tu. Matendo ya Mitume 27:22

Now I exhort you to cheer up, for there will be no loss of life among you, but only of the ship.

Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, Matendo ya Mitume 27:23

For there stood by me this night an angel, belonging to the God whose I am and whom I serve,

akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Matendo ya Mitume 27:24

saying, 'Don't be afraid, Paul. You must stand before Caesar. Behold, God has granted you all those who sail with you.'

Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa. Matendo ya Mitume 27:25

Therefore, sirs, cheer up! For I believe God, that it will be just as it has been spoken to me.

Lakini hatuna budi kupwelewa katika kisiwa kimoja. Matendo ya Mitume 27:26

But we must run aground on a certain island."

Hata usiku wa kumi na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, kama usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu. Matendo ya Mitume 27:27

But when the fourteenth night had come, as we were driven back and forth in the Adriatic Sea, about midnight the sailors surmised that they were drawing near to some land.

Wakatupa bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata pima kumi na tano. Matendo ya Mitume 27:28

They took soundings, and found twenty fathoms.{20 fathoms = 120 feet = 36.6 meters} After a little while, they took soundings again, and found fifteen fathoms.{15 fathoms = 90 feet = 27.4 meters}.

Wakachelea tusije tukapwelewa mahali penye miamba, wakatupa nanga nne za tezi, wakaomba kuche. Matendo ya Mitume 27:29

Fearing that we would run aground on rocky ground, they let go four anchors from the stern, and wished for daylight.

Na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha merikebu, wakiishusha mashua baharini kana kwamba wanataka kutupa nanga za omo, Matendo ya Mitume 27:30

As the sailors were trying to flee out of the ship, and had lowered the boat into the sea, pretending that they would lay out anchors from the bow,

Paulo akawaambia akida na askari, Hawa wasipokaa ndani ya merikebu hamtaweza kuokoka. Matendo ya Mitume 27:31

Paul said to the centurion and to the soldiers, "Unless these stay in the ship, you can't be saved."

Basi askari wakazikata kamba za mashua, wakaiacha ianguke. Matendo ya Mitume 27:32

Then the soldiers cut away the ropes of the boat, and let it fall off.

Na kulipokuwa kukipambauka Paulo akawasihi wote wale chakula, akisema, Leo ni siku ya kumi na nne kungoja na kufunga, hamkula kitu cho chote. Matendo ya Mitume 27:33

While the day was coming on, Paul begged them all to take some food, saying, "This day is the fourteenth day that you wait and continue fasting, having taken nothing.

Basi nawasihi mle chakula, maana itakuwa kwa wokovu wenu; kwa maana hapana hata unywele wa kichwa cha mmoja wenu utakaopotea. Matendo ya Mitume 27:34

Therefore I beg you to take some food, for this is for your safety; for not a hair will perish from any of your heads."

Alipokwisha kusema hayo akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula. Matendo ya Mitume 27:35

When he had said this, and had taken bread, he gave thanks to God in the presence of all, and he broke it, and began to eat.

Ndipo wakachangamka wote, wakala chakula wenyewe. Matendo ya Mitume 27:36

Then they all cheered up, and they also took food.

Na sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu mia mbili na sabini na sita. Matendo ya Mitume 27:37

In all, we were two hundred seventy-six souls on the ship.

Walipokwisha kushiba wakaipunguza shehena ya merikebu, wakiitupa ngano baharini. Matendo ya Mitume 27:38

When they had eaten enough, they lightened the ship, throwing out the wheat into the sea.

Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana. Matendo ya Mitume 27:39

When it was day, they didn't recognize the land, but they noticed a certain bay with a beach, and they decided to try to drive the ship onto it.

Wakazitupilia mbali zile nanga, na kuziacha baharini, pamoja na kuzilegeza kamba za sukani, wakalitweka tanga dogo ili liushike upepo, wakauendea ule ufuo. Matendo ya Mitume 27:40

Casting off the anchors, they left them in the sea, at the same time untying the rudder ropes. Hoisting up the foresail to the wind, they made for the beach.

Lakini wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, omo ikakwama ikakaa isitikiswe, bali tezi ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi. Matendo ya Mitume 27:41

But coming to a place where two seas met, they ran the vessel aground. The bow struck and remained immovable, but the stern began to break up by the violence of the waves.

Shauri la askari lilikuwa kuwaua wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia. Matendo ya Mitume 27:42

The soldiers' counsel was to kill the prisoners, so that none of them would swim out and escape.

Bali akida, akitaka kumponya Paulo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu; Matendo ya Mitume 27:43

But the centurion, desiring to save Paul, stopped them from their purpose, and commanded that those who could swim should throw themselves overboard first to go toward the land;

nao waliosalia, hawa juu ya mbao na hawa juu ya vitu vingine vya merikebu. Na hivyo watu wote wakapata kuifikilia nchi kavu salama. Matendo ya Mitume 27:44

and the rest should follow, some on planks, and some on other things from the ship. So it happened that they all escaped safely to the land.