Matendo ya Mitume 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 6 (Swahili) Acts 6 (English)

Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku. Matendo ya Mitume 6:1

Now in those days, when the number of the disciples was multiplying, a complaint arose from the Grecian Jews against the Hebrews because their widows were neglected in the daily service.

Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani. Matendo ya Mitume 6:2

The twelve summoned the multitude of the disciples and said, "It is not appropriate for us to forsake the word of God and serve tables.

Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; Matendo ya Mitume 6:3

Therefore select from among you, brothers, seven men of good report, full of the Holy Spirit and of wisdom, whom we may appoint over this business.

na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno. Matendo ya Mitume 6:4

But we will continue steadfastly in prayer and in the ministry of the word."

Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; Matendo ya Mitume 6:5

These words pleased the whole multitude. They chose Stephen, a man full of faith and of the Holy Spirit, Philip, Prochorus, Nicanor, Timon, Parmenas, and Nicolaus, a proselyte of Antioch;

ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao. Matendo ya Mitume 6:6

whom they set before the apostles. When they had prayed, they laid their hands on them.

Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani. Matendo ya Mitume 6:7

The word of God increased and the number of the disciples multiplied in Jerusalem exceedingly. A great company of the priests were obedient to the faith.

Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. Matendo ya Mitume 6:8

Stephen, full of faith and power, performed great wonders and signs among the people.

Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano; Matendo ya Mitume 6:9

But some of those who were of the synagogue called "The Libertines," and of the Cyrenians, of the Alexandrians, and of those of Cilicia and Asia arose, disputing with Stephen.

lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye. Matendo ya Mitume 6:10

They weren't able to withstand the wisdom and the Spirit by which he spoke.

Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu. Matendo ya Mitume 6:11

Then they secretly induced men to say, "We have heard him speak blasphemous words against Moses and God."

Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza. Matendo ya Mitume 6:12

They stirred up the people, the elders, and the scribes, and came against him and seized him, and brought him in to the council,

Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati; Matendo ya Mitume 6:13

and set up false witnesses who said, "This man never stops speaking blasphemous words against this holy place and the law.

maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu mahali hapa, na kuzibadili desturi tulizopewa na Musa. Matendo ya Mitume 6:14

For we have heard him say that this Jesus of Nazareth will destroy this place, and will change the customs which Moses delivered to us."

Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika. Matendo ya Mitume 6:15

All who sat in the council, fastening their eyes on him, saw his face like it was the face of an angel.