Matendo ya Mitume 23 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 23 (Swahili) Acts 23 (English)

Paulo akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa dhamiri safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hata leo hivi. Matendo ya Mitume 23:1

Paul, looking steadfastly at the council, said, "Brothers, I have lived before God in all good conscience until this day."

Kuhani Mkuu Anania akawaamuru wale waliosimama karibu naye wampige kinywa chake. Matendo ya Mitume 23:2

The high priest, Ananias, commanded those who stood by him to strike him on the mouth.

Ndipo Paulo akamwambia, Mungu atakupiga wewe, ukuta uliopakwa chokaa. Wewe umeketi kunihukumu sawasawa na sheria, nawe unaamuru nipigwe kinyume cha sheria? Matendo ya Mitume 23:3

Then Paul said to him, "God will strike you, you whitewashed wall! Do you sit to judge me according to the law, and command me to be struck contrary to the law?"

Wale waliosimama karibu wakasema, Je! Unamtukana Kuhani Mkuu wa Mungu? Matendo ya Mitume 23:4

Those who stood by said, "Do you malign God's high priest?"

Paulo akasema, Sikujua, ndugu zangu, ya kuwa yeye ni Kuhani Mkuu; maana imeandikwa, Usimnenee mabaya mkuu wa watu wako. Matendo ya Mitume 23:5

Paul said, "I didn't know, brothers, that he was high priest. For it is written, 'You shall not speak evil of a ruler of your people.'"

Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu. Matendo ya Mitume 23:6

But when Paul perceived that the one part were Sadducees and the other Pharisees, he cried out in the council, "Men and brothers, I am a Pharisee, a son of Pharisees. Concerning the hope and resurrection of the dead I am being judged!"

Alipokwisha kunena hayo palikuwa na mashindano baina ya Mafarisayo na Masadukayo, mkutano ukafarakana. Matendo ya Mitume 23:7

When he had said this, an argument arose between the Pharisees and Sadducees, and the assembly was divided.

Kwa maana Masadukayo husema ya kwamba hakuna kiyama wala malaika wala roho; bali Mafarisayo hukiri yote. Matendo ya Mitume 23:8

For the Sadducees say that there is no resurrection, nor angel, nor spirit; but the Pharisees confess all of these.

Pakawa na makelele mengi. Waandishi wengine wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakateta, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema naye, ni nini? Matendo ya Mitume 23:9

A great clamor arose, and some of the scribes of the Pharisees part stood up, and contended, saying, "We find no evil in this man. But if a spirit or angel has spoken to him, let's not fight against God!"

Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akachelea Paulo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumwondoa kwa nguvu mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome. Matendo ya Mitume 23:10

When a great argument arose, the commanding officer, fearing that Paul would be torn in pieces by them, commanded the soldiers to go down and take him by force from among them, and bring him into the barracks.

Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako. Matendo ya Mitume 23:11

The following night, the Lord stood by him, and said, "Cheer up, Paul, for as you have testified about me at Jerusalem, so you must testify also at Rome."

Kulipopambauka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hata wamwue Paulo. Matendo ya Mitume 23:12

When it was day, some of the Jews banded together, and bound themselves under a curse, saying that they would neither eat nor drink until they had killed Paul.

Na hao walioapiana hivyo walipata zaidi ya watu arobaini. Matendo ya Mitume 23:13

There were more than forty people who had made this conspiracy.

Nao wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo tusionje kitu hata tumwue Paulo. Matendo ya Mitume 23:14

They came to the chief priests and the elders, and said, "We have bound ourselves under a great curse, to taste nothing until we have killed Paul.

Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi tu tayari kumwua kabla hajakaribia. Matendo ya Mitume 23:15

Now therefore, you with the council inform the commanding officer that he should bring him down to you tomorrow, as though you were going to judge his case more exactly. We are ready to kill him before he comes near."

Mjomba wake Paulo akasikia habari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paulo habari. Matendo ya Mitume 23:16

But Paul's sister's son heard of their lying in wait, and he came and entered into the barracks and told Paul.

Paulo akamwita akida mmoja, akasema, Mchukue kijana huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwarifu. Matendo ya Mitume 23:17

Paul summoned one of the centurions, and said, "Bring this young man to the commanding officer, for he has something to tell him."

Basi akamchukua, akampeleka kwa jemadari, akamwambia, Paulo, yule mfungwa, aliniita akataka nikuletee kijana huyu kwa kuwa ana neno la kukuambia. Matendo ya Mitume 23:18

So he took him, and brought him to the commanding officer, and said, "Paul, the prisoner, summoned me and asked me to bring this young man to you, who has something to tell you."

Yule jemadari akamshika mkono akajitenga pamoja naye kando, akamwuliza kwa faragha, Una neno gani utakalo kuniarifu? Matendo ya Mitume 23:19

The commanding officer took him by the hand, and going aside, asked him privately, "What is it that you have to tell me?"

Akasema Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paulo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata habari zake kwa usahihi zaidi. Matendo ya Mitume 23:20

He said, "The Jews have agreed to ask you to bring Paul down to the council tomorrow, as though intending to inquire somewhat more accurately concerning him.

Basi wewe usikubali; kwa maana watu zaidi ya arobaini wanamwotea, wamejifunga kwa kiapo wasile wala wasinywe hata watakapomwua; nao sasa wako tayari, wakiitazamia ahadi kwako. Matendo ya Mitume 23:21

Therefore don't yield to them, for more than forty men lie in wait for him, who have bound themselves under a curse neither to eat nor to drink until they have killed him. Now they are ready, looking for the promise from you."

Basi yule jemadari akamwacha kijana aende zake, akimwagiza, Usimwambie mtu awaye yote ya kwamba umeniarifu haya. Matendo ya Mitume 23:22

So the commanding officer let the young man go, charging him, "Tell no one that you have revealed these things to me."

Akawaita maakida wawili, akasema, Wekeni tayari askari mia mbili kwenda Kaisaria, na askari wapanda farasi sabini, na wenye mikuki mia mbili, kwa saa tatu ya usiku. Matendo ya Mitume 23:23

He called to himself two of the centurions, and said, "Prepare two hundred soldiers to go as far as Caesarea, with seventy horsemen, and two hundred men armed with spears, at the third hour of the night{about 9:00 PM}."

Akawaambia kuweka wanyama tayari wampandishe Paulo, na kumchukua salama kwa Feliki liwali. Matendo ya Mitume 23:24

He asked them to provide animals, that they might set Paul on one, and bring him safely to Felix the governor.

Akaandika barua, kwa namna hii, Matendo ya Mitume 23:25

He wrote a letter like this:

Klaudio Lisia kwa liwali mtukufu Feliki, Salamu! Matendo ya Mitume 23:26

"Claudius Lysias to the most excellent governor Felix: Greetings.

Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi, wakawa karibu kumwua, ndipo nikaenda pamoja na kikosi cha askari nikamwokoa, nilipopata habari ya kuwa yeye ni Mrumi. Matendo ya Mitume 23:27

"This man was seized by the Jews, and was about to be killed by them, when I came with the soldiers and rescued him, having learned that he was a Roman.

Nami nikitaka kulijua lile neno walilomshitakia, nikamtelemsha nikamweka mbele ya baraza; Matendo ya Mitume 23:28

Desiring to know the cause why they accused him, I brought him down to their council.

nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa. Matendo ya Mitume 23:29

I found him to be accused about questions of their law, but to have nothing laid to his charge worthy of death or of bonds.

Hata nilipopewa habari kwamba patakuwa na vitimvi juu ya mtu huyu, mara nikampeleka kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu. Matendo ya Mitume 23:30

When I was told that the Jews lay in wait for the man, I sent him to you immediately, charging his accusers also to bring their accusations against him before you. Farewell."

Basi, wale askari wakamchukua Paulo kama walivyoamriwa, wakampeleka hata Antipatri usiku; Matendo ya Mitume 23:31

So the soldiers, carrying out their orders, took Paul and brought him by night to Antipatris.

hata asubuhi wakawaacha wale wapanda farasi waende pamoja naye, nao wakarudi zao ngomeni. Matendo ya Mitume 23:32

But on the next day they left the horsemen to go with him, and returned to the barracks.

Na wale walipofika Kaisaria, na kumpa liwali ile barua, wakamweka Paulo mbele yake. Matendo ya Mitume 23:33

When they came to Caesarea and delivered the letter to the governor, they also presented Paul to him.

Naye alipokwisha kuisoma, akawauliza, Mtu huyu ni wa jimbo gani? Alipoarifiwa ya kuwa ni mtu wa Kilikia, Matendo ya Mitume 23:34

When the governor had read it, he asked what province he was from. When he understood that he was from Cilicia, he said,

akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya uliwali ya Herode. Matendo ya Mitume 23:35

"I will hear you fully when your accusers also arrive." He commanded that he be kept in Herod's palace.