Matendo ya Mitume 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 13 (Swahili) Acts 13 (English)

Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Matendo ya Mitume 13:1

Now in the assembly that was at Antioch there were some prophets and teachers: Barnabas, Simeon who was called Niger, Lucius of Cyrene, Manaen the foster-brother of Herod the tetrarch, and Saul.

Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Matendo ya Mitume 13:2

As they served the Lord and fasted, the Holy Spirit said, "Separate Barnabas and Saul for me, for the work to which I have called them."

Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao. Matendo ya Mitume 13:3

Then, when they had fasted and prayed and laid their hands on them, they sent them away.

Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro. Matendo ya Mitume 13:4

So, being sent out by the Holy Spirit, they went down to Seleucia. From there they sailed to Cyprus.

Na walipokuwa katika Salami wakalihubiri neno la Mungu katika masinagogi ya Wayahudi, nao walikuwa naye Yohana kuwa mtumishi wao. Matendo ya Mitume 13:5

When they were at Salamis, they proclaimed the word of God in the synagogues of the Jews. They had also John as their attendant.

Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; Matendo ya Mitume 13:6

When they had gone through the island to Paphos, they found a certain sorcerer, a false prophet, a Jew, whose name was Bar Jesus,

mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. Matendo ya Mitume 13:7

who was with the proconsul, Sergius Paulus, a man of understanding. This man summoned Barnabas and Saul, and sought to hear the word of God.

Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Matendo ya Mitume 13:8

But Elymas the sorcerer (for so is his name by interpretation) withstood them, seeking to turn aside the proconsul from the faith.

Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, Matendo ya Mitume 13:9

But Saul, who is also called Paul, filled with the Holy Spirit, fastened his eyes on him,

akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Matendo ya Mitume 13:10

and said, "Full of all deceit and all cunning, you son of the devil, you enemy of all righteousness, will you not cease to pervert the right ways of the Lord?

Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. Matendo ya Mitume 13:11

Now, behold, the hand of the Lord is on you, and you will be blind, not seeing the sun for a season!" Immediately there fell on him a mist and darkness. He went around seeking someone to lead him by the hand.

Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana. Matendo ya Mitume 13:12

Then the proconsul, when he saw what was done, believed, being astonished at the teaching of the Lord.

Kisha Paulo na wenziwe wakang'oa nanga wakasafiri kutoka Pafo, wakafika Perge katika Pamfilia. Yohana akawaacha akarejea Yerusalemu. Matendo ya Mitume 13:13

Now Paul and his company set sail from Paphos, and came to Perga in Pamphylia. John departed from them and returned to Jerusalem.

Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi. Matendo ya Mitume 13:14

But they, passing on from Perga, came to Antioch of Pisidia. They went into the synagogue on the Sabbath day, and sat down.

Kisha, baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sinagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni. Matendo ya Mitume 13:15

After the reading of the law and the prophets, the rulers of the synagogue sent to them, saying, "Brothers, if you have any word of exhortation for the people, speak."

Paulo akasimama, akawapungia mkono, akasema, Enyi waume wa Israeli, nanyi mnaomcha Mungu, sikilizeni. Matendo ya Mitume 13:16

Paul stood up, and beckoning with his hand said, "Men of Israel, and you who fear God, listen.

Mungu wa watu hawa Israeli aliwachagua baba zetu, akawatukuza watu hao, walipokuwa wakikaa kama wageni katika nchi ya Misri, na kwa mkono ulioinuliwa akawatoa, akawaongoza. Matendo ya Mitume 13:17

The God of this people{TR, NU add "Israel"} chose our fathers, and exalted the people when they stayed as aliens in the land of Egypt, and with an uplifted arm, he led them out of it.

Na kwa muda wa miaka kama arobaini akawavumilia katika jangwa. Matendo ya Mitume 13:18

For a period of about forty years he put up with them in the wilderness.

Na alipokwisha kuwaharibu mataifa saba katika nchi ya Kanaani akawapa nchi yao iwe urithi kwa muda wa miaka kama mia nne na hamsini; Matendo ya Mitume 13:19

When he had destroyed seven nations in the land of Canaan, he gave them their land for an inheritance, for about four hundred fifty years.

baada ya hayo akawapa waamuzi hata zamani za nabii Samweli. Matendo ya Mitume 13:20

After these things he gave them judges until Samuel the prophet.

Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka arobaini. Matendo ya Mitume 13:21

Afterward they asked for a king, and God gave to them Saul the son of Kish, a man of the tribe of Benjamin, for forty years.

Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote. Matendo ya Mitume 13:22

When he had removed him, he raised up David to be their king, to whom he also testified, 'I have found David the son of Jesse, a man after my heart, who will do all my will.'

Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi; Matendo ya Mitume 13:23

From this man's seed, God has brought salvation{TR, NU read "a Savior, Jesus" instead of "salvation"} to Israel according to his promise,

Yohana alipokuwa amekwisha kuwahubiri watu wote wa Israeli habari za ubatizo wa toba, kabla ya kuja kwake. Matendo ya Mitume 13:24

before his coming, when John had first preached the baptism of repentance to Israel.{TR, NU read "to all the people of Israel" instead of "to Israel"}

Naye Yohana alipokuwa akimaliza mwendo wake alinena, Mwanidhani mimi kuwa nani? Mimi siye. Lakini, angalieni, anakuja mmoja nyuma yangu ambaye mimi sistahili kumlegezea viatu vya miguu yake. Matendo ya Mitume 13:25

As John was fulfilling his course, he said, 'What do you suppose that I am? I am not he. But behold, one comes after me the sandals of whose feet I am not worthy to untie.'

Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa. Matendo ya Mitume 13:26

Brothers, children of the stock of Abraham, and those among you who fear God, the word of this salvation is sent out to you.

Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu. Matendo ya Mitume 13:27

For those who dwell in Jerusalem, and their rulers, because they didn't know him, nor the voices of the prophets which are read every Sabbath, fulfilled them by condemning him.

Na ijapokuwa hawakuona sababu ya kumfisha wakamwomba Pilato auawe. Matendo ya Mitume 13:28

Though they found no cause for death, they still asked Pilate to have him killed.

Hata walipokwisha kumaliza yote aliyoandikiwa, wakamtelemsha katika ule mti, wakamweka kaburini. Matendo ya Mitume 13:29

When they had fulfilled all things that were written about him, they took him down from the tree, and laid him in a tomb.

Lakini Mungu akamfufua katika wafu; Matendo ya Mitume 13:30

But God raised him from the dead,

akaonekana siku nyingi na wale waliopanda naye kutoka Galilaya hata Yerusalemu, ambao sasa ndio walio mashahidi wake mbele ya watu. Matendo ya Mitume 13:31

and he was seen for many days by those who came up with him from Galilee to Jerusalem, who are his witnesses to the people.

Na sisi tunawahubiri habari njema ya ahadi ile waliyopewa mababa, Matendo ya Mitume 13:32

We bring you good news of the promise made to the fathers,

ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili, Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa. Matendo ya Mitume 13:33

that God has fulfilled the same to us, their children, in that he raised up Jesus. As it is also written in the second psalm, 'You are my Son. Today I have become your father.'

Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi, Nitawapa ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini. Matendo ya Mitume 13:34

"Concerning that he raised him up from the dead, now no more to return to corruption, he has spoken thus: 'I will give you the holy and sure blessings of David.'

Kwa hiyo anena na pengine, Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu, Matendo ya Mitume 13:35

Therefore he says also in another psalm, 'You will not allow your Holy One to see decay.'

Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu. Matendo ya Mitume 13:36

For David, after he had in his own generation served the counsel of God, fell asleep, and was laid with his fathers, and saw decay.

Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona uharibifu. Matendo ya Mitume 13:37

But he whom God raised up saw no decay.

Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi; Matendo ya Mitume 13:38

Be it known to you therefore, brothers{The word for "brothers" here and where the context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."}, that through this man is proclaimed to you remission of sins,

na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa. Matendo ya Mitume 13:39

and by him everyone who believes is justified from all things, from which you could not be justified by the law of Moses.

Angalieni, basi, isiwajilie habari ile iliyonenwa katika manabii. Matendo ya Mitume 13:40

Beware therefore, lest that come on you which is spoken in the prophets:

Tazameni, enyi mnaodharau, kastaajabuni, mkatoweke; kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu, kazi ambayo msingeisadiki kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana. Matendo ya Mitume 13:41

'Behold, you scoffers, and wonder, and perish; For I work a work in your days, A work which you will in no way believe, if one declares it to you.'"

Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili. Matendo ya Mitume 13:42

So when the Jews went out of the synagogue, the Gentiles begged that these words might be preached to them the next Sabbath.

Sinagogi ilipofumukana, Wayahudi na waongofu watauwa wengi wakashikamana na Paulo na Barnaba; ambao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu. Matendo ya Mitume 13:43

Now when the synagogue broke up, many of the Jews and of the devout proselytes followed Paul and Barnabas; who, speaking to them, urged them to continue in the grace of God.

Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. Matendo ya Mitume 13:44

The next Sabbath almost the whole city was gathered together to hear the word of God.

Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana. Matendo ya Mitume 13:45

But when the Jews saw the multitudes, they were filled with jealousy, and contradicted the things which were spoken by Paul, and blasphemed.

Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. Matendo ya Mitume 13:46

Paul and Barnabas spoke out boldly, and said, "It was necessary that God's word should be spoken to you first. Since indeed you thrust it from you, and judge yourselves unworthy of eternal life, behold, we turn to the Gentiles.

Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia. Matendo ya Mitume 13:47

For so has the Lord commanded us, saying, 'I have set you as a light for the Gentiles, That you should bring salvation to the uttermost parts of the earth.'"

Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. Matendo ya Mitume 13:48

As the Gentiles heard this, they were glad, and glorified the word of God. As many as were appointed to eternal life believed.

Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote. Matendo ya Mitume 13:49

The Lord's word was spread abroad throughout all the region.

Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao. Matendo ya Mitume 13:50

But the Jews stirred up the devout and prominent women and the chief men of the city, and stirred up a persecution against Paul and Barnabas, and threw them out of their borders.

Nao wakawakung'utia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio. Matendo ya Mitume 13:51

But they shook off the dust of their feet against them, and came to Iconium.

Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu. Matendo ya Mitume 13:52

The disciples were filled with joy with the Holy Spirit.