Matendo ya Mitume 22 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 22 (Swahili) Acts 22 (English)

Enyi wanaume, ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea mbele yenu sasa. Matendo ya Mitume 22:1

"Brothers and fathers, listen to the defense which I now make to you."

Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza; akasema, Matendo ya Mitume 22:2

When they heard that he spoke to them in the Hebrew language, they were even more quiet. He said,

Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; Matendo ya Mitume 22:3

"I am indeed a Jew, born in Tarsus of Cilicia, but brought up in this city at the feet of Gamaliel, instructed according to the strict manner of the law of our fathers, being zealous for God, even as you all are this day.

nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake. Matendo ya Mitume 22:4

I persecuted this Way to the death, binding and delivering into prisons both men and women.

Kama Kuhani Mkuu naye anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipokea barua kwao kuwapelekea ndugu wale, nikaenda Dameski, ili niwalete wale waliokuwa huko hata Yerusalemu, hali wamefungwa, ili waadhibiwe. Matendo ya Mitume 22:5

As also the high priest and all the council of the elders testify, from whom also I received letters to the brothers, and traveled to Damascus to bring them also who were there to Jerusalem in bonds to be punished.

Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote. Matendo ya Mitume 22:6

It happened that, as I made my journey, and came close to Damascus, about noon, suddenly there shone from the sky a great light around me.

Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi? Matendo ya Mitume 22:7

I fell to the ground, and heard a voice saying to me, 'Saul, Saul, why are you persecuting me?'

Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi. Matendo ya Mitume 22:8

I answered, 'Who are you, Lord?' He said to me, 'I am Jesus of Nazareth, whom you persecute.'

Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami. Matendo ya Mitume 22:9

"Those who were with me indeed saw the light and were afraid, but they didn't understand the voice of him who spoke to me.

Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye. Matendo ya Mitume 22:10

I said, 'What shall I do, Lord?' The Lord said to me, 'Arise, and go into Damascus. There you will be told about all things which are appointed for you to do.'

Na nilipokuwa sioni kwa sababu ya fahari ya nuru ile, nikaongozwa na mikono yao waliokuwa pamoja nami, nikaingia Dameski. Matendo ya Mitume 22:11

When I couldn't see for the glory of that light, being led by the hand of those who were with me, I came into Damascus.

Basi mtu mmoja, Anania, mtauwa kwa kuifuata sheria, aliyeshuhudiwa wema na Wayahudi wote waliokaa huko, Matendo ya Mitume 22:12

One Ananias, a devout man according to the law, well reported of by all the Jews who lived in Damascus,

Akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu yangu Sauli, uone. Nikamwinulia macho yangu saa ile ile. Matendo ya Mitume 22:13

came to me, and standing by me said to me, 'Brother Saul, receive your sight!' In that very hour I looked up at him.

Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, na kumwona yule Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake. Matendo ya Mitume 22:14

He said, 'The God of our fathers has appointed you to know his will, and to see the Righteous One, and to hear a voice from his mouth.

Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia. Matendo ya Mitume 22:15

For you will be a witness for him to all men of what you have seen and heard.

Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake. Matendo ya Mitume 22:16

Now why do you wait? Arise, be baptized, and wash away your sins, calling on the name of the Lord.'

Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemu, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa hali ya kuzimia roho, Matendo ya Mitume 22:17

"It happened that, when I had returned to Jerusalem, and while I prayed in the temple, I fell into a trance,

nikamwona, naye akiniambia, Hima, utoke Yerusalemu upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako katika habari zangu. Matendo ya Mitume 22:18

and saw him saying to me, 'Hurry and get out of Jerusalem quickly, because they will not receive testimony concerning me from you.'

Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikiwafunga gerezani wale wanaokuamini na kuwapiga katika kila sinagogi. Matendo ya Mitume 22:19

I said, 'Lord, they themselves know that I imprisoned and beat in every synagogue those who believed in you.

Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali, na kuzitunza nguo zao waliomwua. Matendo ya Mitume 22:20

When the blood of Stephen, your witness, was shed, I also was standing by, and consenting to his death, and guarding the cloaks of those who killed him.'

Naye akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma uende mbali kwa watu wa Mataifa. Matendo ya Mitume 22:21

"He said to me, 'Depart, for I will send you out far from here to the Gentiles.'"

Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika nchi, kwa maana haifai aishi. Matendo ya Mitume 22:22

They listened to him until he said that; then they lifted up their voice, and said, "Rid the earth of this fellow, for he isn't fit to live!"

Walipokuwa wakipiga kelele na kutupa mavazi yao na kurusha-rusha mavumbi juu, Matendo ya Mitume 22:23

As they cried out, and threw off their cloaks, and threw dust into the air,

yule jemadari akaamuru aletwe ndani ya ngome, akisema aulizwe habari zake kwa kupigwa mijeledi, ili ajue sababu hata wakampigia kelele namna hii. Matendo ya Mitume 22:24

the commanding officer commanded him to be brought into the barracks, ordering him to be examined by scourging, that he might know for what crime they shouted against him like that.

Hata walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliyesimama karibu, Je! Ni halali ninyi kumpiga mtu aliye Mrumi naye hajakuhumiwa bado? Matendo ya Mitume 22:25

When they had tied him up with thongs, Paul asked the centurion who stood by, "Is it lawful for you to scourge a man who is a Roman, and not found guilty?"

Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni Mrumi. Matendo ya Mitume 22:26

When the centurion heard it, he went to the commanding officer and told him, "Watch what you are about to do, for this man is a Roman!"

Jemadari akaja, akamwuliza, Niambie, u Mrumi? Akasema, Ndiyo. Matendo ya Mitume 22:27

The commanding officer came and asked him, "Tell me, are you a Roman?" He said, "Yes."

Jemadari akajibu, Mimi nalipata wenyeji huu kwa mali nyingi. Paulo akasema, Na mimi ni Mrumi wa kuzaliwa. Matendo ya Mitume 22:28

The commanding officer answered, "I bought my citizenship for a great price." Paul said, "But I was born a Roman."

Basi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari naye akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga. Matendo ya Mitume 22:29

Immediately those who were about to examine him departed from him, and the commanding officer also was afraid when he realized that he was a Roman, because he had bound him.

Siku ya pili yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru wakuu wa makuhani na baraza yote wakutane. Akamleta Paulo chini, akamweka mbele yao. Matendo ya Mitume 22:30

But on the next day, desiring to know the truth about why he was accused by the Jews, he freed him from the bonds, and commanded the chief priests and all the council to come together, and brought Paul down and set him before them.