Matendo ya Mitume 28 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 28 (Swahili) Acts 28 (English)

Tulipokwisha kuokoka, ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita. Matendo ya Mitume 28:1

When we had escaped, then they{NU reads "we"} learned that the island was called Malta.

Wenyeji wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana waliwasha moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyonyesha na kwa sababu ya baridi. Matendo ya Mitume 28:2

The natives showed us uncommon kindness; for they kindled a fire, and received us all, because of the present rain, and because of the cold.

Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzonga-zonga mkononi. Matendo ya Mitume 28:3

But when Paul had gathered a bundle of sticks and laid them on the fire, a viper came out because of the heat, and fastened on his hand.

Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewa-lewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi. Matendo ya Mitume 28:4

When the natives saw the creature hanging from his hand, they said one to another, "No doubt this man is a murderer, whom, though he has escaped from the sea, yet Justice has not allowed to live."

Lakini yeye akamtukusia motoni asipate madhara. Matendo ya Mitume 28:5

However he shook off the creature into the fire, and wasn't harmed.

Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu. Matendo ya Mitume 28:6

But they expected that he would have swollen or fallen down dead suddenly, but when they watched for a long time and saw nothing bad happen to him, they changed their minds, and said that he was a god.

Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya mkuu wa kisiwa, jina lake Publio; mtu huyu akatukaribisha kwa moyo wa urafiki, akatufanya wageni wake kwa muda wa siku tatu. Matendo ya Mitume 28:7

Now in the neighborhood of that place were lands belonging to the chief man of the island, named Publius, who received us, and courteously entertained us for three days.

Ikawa babaake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paulo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, na kumpoza. Matendo ya Mitume 28:8

It happened that the father of Publius lay sick of fever and dysentery. Paul entered in to him, prayed, and laying his hands on him, healed him.

Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja wakapozwa; Matendo ya Mitume 28:9

Then when this was done, the rest also who had diseases in the island came, and were cured.

nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi; basi tulipoabiri wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo. Matendo ya Mitume 28:10

They also honored us with many honors, and when we sailed, they put on board the things that we needed.

Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha. Matendo ya Mitume 28:11

After three months, we set sail in a ship of Alexandria which had wintered in the island, whose sign was "The Twin Brothers."

Tukafika Sirakusa, tukakaa siku tatu. Matendo ya Mitume 28:12

Touching at Syracuse, we stayed there three days.

Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio; baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli. Matendo ya Mitume 28:13

From there we circled around and arrived at Rhegium. After one day, a south wind sprang up, and on the second day we came to Puteoli,

Huko tukakuta ndugu, wakatusihi tukae nao siku saba; na hivi tukafika Rumi. Matendo ya Mitume 28:14

where we found brothers,{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} and were entreated to stay with them for seven days. So we came to Rome.

Na kutoka huko ndugu, waliposikia habari zetu, wakaja kutulaki mpaka Soko la Apio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona alimshukuru Mungu, akachangamka. Matendo ya Mitume 28:15

From there the brothers, when they heard of us, came to meet us as far as The Market of Appius and The Three Taverns. When Paul saw them, he thanked God, and took courage.

Tulipoingia Rumi Paulo alipewa ruhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda. Matendo ya Mitume 28:16

When we entered into Rome, the centurion delivered the prisoners to the captain of the guard, but Paul was allowed to stay by himself with the soldier who guarded him.

Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane, hata walipokutanika akawaambia, Ndugu zangu, ningawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, hali nimefungwa, tokea Yerusalemu. Matendo ya Mitume 28:17

It happened that after three days Paul called together those who were the leaders of the Jews. When they had come together, he said to them, "I, brothers, though I had done nothing against the people, or the customs of our fathers, still was delivered prisoner from Jerusalem into the hands of the Romans,

Na hao walipokwisha kuniuliza-uliza walitaka kunifungua, kwa maana hapakuwa na sababu yo yote kwangu ya kuuawa. Matendo ya Mitume 28:18

who, when they had examined me, desired to set me free, because there was no cause of death in me.

Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu. Matendo ya Mitume 28:19

But when the Jews spoke against it, I was constrained to appeal to Caesar, not that I had anything about which to accuse my nation.

Basi kwa ajili ya hayo, nimewaita mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli. Matendo ya Mitume 28:20

For this cause therefore I asked to see you and to speak with you. For because of the hope of Israel I am bound with this chain."

Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye habari zako kutoka Uyahudi, wala hapana ndugu hata mmoja aliyefika hapa na kutupasha habari, au kunena neno baya juu yako. Matendo ya Mitume 28:21

They said to him, "We neither received letters from Judea concerning you, nor did any of the brothers come here and report or speak any evil of you.

Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika habari za madhehebu hiyo imejulikana kwetu kwamba inanenwa vibaya kila mahali. Matendo ya Mitume 28:22

But we desire to hear from you what you think. For, as concerning this sect, it is known to us that everywhere it is spoken against."

Wakiisha kuagana naye siku, wakamjia katika nyumba aliyokaa, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii, tangu asubuhi hata jioni. Matendo ya Mitume 28:23

When they had appointed him a day, many people came to him at his lodging. He explained to them, testifying about the Kingdom of God, and persuading them concerning Jesus, both from the law of Moses and from the prophets, from morning until evening.

Wengine waliamini yale yaliyonenwa, wengine hawakuyaamini. Matendo ya Mitume 28:24

Some believed the things which were spoken, and some disbelieved.

Na walipokuwa hawapatani wao kwa wao, wakaenda zao, Paulo alipokwisha kusema neno hili moja, ya kwamba, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya, Matendo ya Mitume 28:25

When they didn't agree among themselves, they departed after Paul had spoken one word, "The Holy Spirit spoke rightly through Isaiah, the prophet, to our fathers,

akisema, Enenda kwa watu hawa, ukawaambie, Kusikia, mtasikia wala hamtafahamu; Na kuona, mtaona wala hamtatambua; Matendo ya Mitume 28:26

saying, 'Go to this people, and say, In hearing, you will hear, But will in no way understand. In seeing, you will see, But will in no way perceive.

Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni mazito ya kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kubadili nia zao, nikawaponya. Matendo ya Mitume 28:27

For this people's heart has grown callous. Their ears are dull of hearing. Their eyes they have closed. Lest they should see with their eyes, Hear with their ears, Understand with their heart, And would turn again, And I would heal them.'

Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa, nao watasikia! Matendo ya Mitume 28:28

"Be it known therefore to you, that the salvation of God is sent to the Gentiles. They will also listen."

Alipokwisha kusema hayo, Wayahudi wakaenda zao, wakiulizana mengi wao kwa wao.] Matendo ya Mitume 28:29

When he had said these words, the Jews departed, having a great dispute among themselves.

Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, Matendo ya Mitume 28:30

Paul stayed two whole years in his own rented house, and received all who were coming to him,

akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu. Matendo ya Mitume 28:31

preaching the Kingdom of God, and teaching the things concerning the Lord Jesus Christ with all boldness, without hinderance.