Matendo ya Mitume 25 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 25 (Swahili) Acts 25 (English)

Hata Festo alipokwisha kuingia katika uliwali, baada ya siku tatu akapanda kwenda Yerusalemu kutoka Kaisaria. Matendo ya Mitume 25:1

Festus therefore, having come into the province, after three days went up to Jerusalem from Caesarea.

Kuhani Mkuu na wakuu wa Wayahudi wakampasha habari za Paulo, wakamsihi, Matendo ya Mitume 25:2

Then the high priest and the principal men of the Jews informed him against Paul, and they begged him,

na kumwomba fadhili juu yake, kwamba atoe amri aletwe Yerusalemu, wapate kumwotea na kumwua njiani. Matendo ya Mitume 25:3

asking a favor against him, that he would summon him to Jerusalem; plotting to kill him on the way.

Lakini Festo akajibu ya kwamba Paulo analindwa Kaisaria; naye mwenyewe yu tayari kwenda huko karibu. Matendo ya Mitume 25:4

However Festus answered that Paul should be kept in custody at Caesarea, and that he himself was about to depart shortly.

Akasema, Wale walio na mamlaka kwenu na watelemke pamoja nami wakamshitaki, ikiwa liko neno baya katika mtu huyu. Matendo ya Mitume 25:5

"Let them therefore," said he, "that are in power among you go down with me, and if there is anything wrong in the man, let them accuse him."

Alipokwisha kukaa kwao siku nane au kumi si zaidi, akatelemkia Kaisaria; hata siku ya pili akaketi katika kiti cha hukumu akaamuru Paulo aletwe. Matendo ya Mitume 25:6

When he had stayed among them more than ten days, he went down to Caesarea, and on the next day he sat on the judgment seat, and commanded Paul to be brought.

Alipokuja, wale Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasimama karibu yake wakaleta mashitaka mengi mazito juu yake, wasiyoweza kuyayakinisha. Matendo ya Mitume 25:7

When he had come, the Jews who had come down from Jerusalem stood around him, bringing against him many and grievous charges which they could not prove,

Paulo akasema akijitetea, Mimi sikukosa neno juu ya sheria ya Wayahudi, wala juu ya hekalu, wala juu ya Kaisari. Matendo ya Mitume 25:8

while he said in his defense, "Neither against the law of the Jews, nor against the temple, nor against Caesar, have I sinned at all."

Lakini Festo akitaka kujipendekeza kwa Wayahudi akamjibu Paulo, akisema, Je! Wataka kwenda Yerusalemu, ukahukumiwe huko mbele yangu kwa ajili ya mambo hayo? Matendo ya Mitume 25:9

But Festus, desiring to gain favor with the Jews, answered Paul and said, "Are you willing to go up to Jerusalem, and be judged by me there concerning these things?"

Paulo akasema, Mimi ninasimama hapa mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari, ndipo panipasapo kuhukumiwa; sikuwakosa Wayahudi neno, kama wewe ujuavyo sana. Matendo ya Mitume 25:10

But Paul said, "I am standing before Caesar's judgment seat, where I ought to be tried. I have done no wrong to the Jews, as you also know very well.

Basi ikiwa ni mkosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; bali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezaye kunitia mikononi mwao. Nataka rufani kwa Kaisari. Matendo ya Mitume 25:11

For if I have done wrong, and have committed anything worthy of death, I don't refuse to die; but if none of those things is true that they accuse me of, no one can give me up to them. I appeal to Caesar!"

Basi Festo alipokwisha kusema na watu wa baraza, akajibu, Umetaka rufani kwa Kaisari! Basi, utakwenda kwa Kaisari. Matendo ya Mitume 25:12

Then Festus, when he had conferred with the council, answered, "You have appealed to Caesar. To Caesar you shall go."

Siku kadha wa kadha zilipokwisha kupita, Agripa mfalme na Bernike wakafika Kaisaria, wakimwamkia Festo. Matendo ya Mitume 25:13

Now when some days had passed, Agrippa the King and Bernice arrived at Caesarea, and greeted Festus.

Na walipokuwa wakikaa huko siku nyingi, Festo akamweleza mfalme habari za Paulo, akisema, Yupo hapa mtu mmoja aliyeachwa na Feliki kifungoni; Matendo ya Mitume 25:14

As he stayed there many days, Festus laid Paul's case before the king, saying, "There is a certain man left a prisoner by Felix;

ambaye nilipokuwa Yerusalemu wakuu wa makuhani na wazee wa Wayahudi wakaniarifu habari zake, wakinitaka hukumu juu yake. Matendo ya Mitume 25:15

about whom, when I was at Jerusalem, the chief priests and the elders of the Jews informed me, asking for a sentence against him.

Nikawajibu kwamba si desturi ya Warumi kumtoa mtu awaye yote, kabla mtu yule aliyeshitakiwa hajaonana na washitaki wake uso kwa uso, na kupewa nafasi ya kujitetea katika mashitaka yake. Matendo ya Mitume 25:16

To whom I answered that it is not the custom of the Romans to give up any man to destruction, before the accused has met the accusers face to face, and has had opportunity to make his defense concerning the matter laid against him.

Basi walipokutanika hapa sikukawia; bali siku ya pili nikaketi katika kiti cha hukumu nikaamuru mtu huyo aletwe. Matendo ya Mitume 25:17

When therefore they had come together here, I didn't delay, but on the next day sat on the judgment seat, and commanded the man to be brought.

Na wale waliomshitaki waliposimama hawakuleta neno lo lote baya, kama nilivyodhani, Matendo ya Mitume 25:18

Concerning whom, when the accusers stood up, they brought no charge of such things as I supposed;

bali walikuwa na maswali mengine mengine juu yake katika dini yao wenyewe, na katika habari ya mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambaye Paulo alikaza kusema kwamba yu hai. Matendo ya Mitume 25:19

but had certain questions against him about their own religion, and about one Jesus, who was dead, whom Paul affirmed to be alive.

Nami nikaona shaka jinsi ya kutafuta hakika ya habari hii, nikamwuliza kama anataka kwenda Yerusalemu ahukumiwe huko katika mambo haya. Matendo ya Mitume 25:20

Being perplexed how to inquire concerning these things, I asked whether he was willing to go to Jerusalem and there be judged concerning these matters.

Lakini Paulo alipodai kuwekwa ahukumiwe na Kaisari, nikaamuru alindwe hata nitakapompeleka kwa Kaisari. Matendo ya Mitume 25:21

But when Paul had appealed to be kept for the decision of the emperor, I commanded him to be kept until I could send him to Caesar."

Agripa akamwambia Festo, Mimi nami nalikuwa nikitaka kumsikia mtu huyu. Akasema, Utamsikia kesho. Matendo ya Mitume 25:22

Agrippa said to Festus, "I also would like to hear the man myself." "Tomorrow," he said, "you shall hear him."

Hata asubuhi Agripa akaja pamoja na Bernike kwa fahari nyingi, wakaingia mahali pa kusikia maneno, pamoja na maakida wakuu na watu wakuu wa mji; Festo akatoa amri, Paulo akaletwa. Matendo ya Mitume 25:23

So on the next day, when Agrippa and Bernice had come with great pomp, and they had entered into the place of hearing with the commanding officers and principal men of the city, at the command of Festus, Paul was brought in.

Festo akasema, Mfalme Agripa, na ninyi nyote mliopo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu, ambaye jamii yote ya Wayahudi huko Yerusalemu na hapa pia wamenitaka niwasaidie, wakipiga kelele kwamba haimpasi kuishi zaidi. Matendo ya Mitume 25:24

Festus said, "King Agrippa, and all men who are here present with us, you see this man, about whom all the multitude of the Jews petitioned me, both at Jerusalem and here, crying that he ought not to live any longer.

Lakini mimi naliona kwamba hakutenda neno la kustahili kuuawa, na yeye mwenyewe alipotaka kuhukumiwa na Kaisari, nalikusudia kumpeleka kwake. Matendo ya Mitume 25:25

But when I found that he had committed nothing worthy of death, and as he himself appealed to the emperor I determined to send him.

Nami katika habari yake sina neno la hakika la kumwandikia bwana. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu, hasa mbele yako wewe, mfalme Agripa, ili akiisha kuulizwa-ulizwa nipate neno la kuandika. Matendo ya Mitume 25:26

Of whom I have no certain thing to write to my lord. Therefore I have brought him forth before you, and especially before you, King Agrippa, that, after examination, I may have something to write.

Kwa maana naona ni neno lisilo maana kumpeleka mfungwa, bila kuonyesha mashitaka yale aliyoshitakiwa. Matendo ya Mitume 25:27

For it seems to me unreasonable, in sending a prisoner, not to also specify the charges against him."