Matendo ya Mitume 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 8 (Swahili) Acts 8 (English)

Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume. Matendo ya Mitume 8:1

Saul was consenting to his death. A great persecution arose against the assembly which was in Jerusalem in that day. They were all scattered abroad throughout the regions of Judea and Samaria, except for the apostles.

Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu. Matendo ya Mitume 8:2

Devout men buried Stephen, and lamented greatly over him.

Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. Matendo ya Mitume 8:3

But Saul ravaged the assembly, entering into every house, and dragged both men and women off to prison.

Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. Matendo ya Mitume 8:4

Therefore those who were scattered abroad went around preaching the word.

Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo. Matendo ya Mitume 8:5

Philip went down to the city of Samaria, and proclaimed to them the Christ.

Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Matendo ya Mitume 8:6

The multitudes listened with one accord to the things that were spoken by Philip, when they heard and saw the signs which he did.

Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. Matendo ya Mitume 8:7

For unclean spirits came out of many of those who had them. They came out, crying with a loud voice. Many who had been paralyzed and lame were healed.

Ikawa furaha kubwa katika mji ule. Matendo ya Mitume 8:8

There was great joy in that city.

Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. Matendo ya Mitume 8:9

But there was a certain man, Simon by name, who used to practice sorcery in the city, and amazed the people of Samaria, making himself out to be some great one,

Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu. Matendo ya Mitume 8:10

to whom they all listened, from the least to the greatest, saying, "This man is that great power of God."

Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake. Matendo ya Mitume 8:11

They listened to him, because for a long time he had amazed them with his sorceries.

Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. Matendo ya Mitume 8:12

But when they believed Philip preaching good news concerning the Kingdom of God and the name of Jesus Christ, they were baptized, both men and women.

Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka. Matendo ya Mitume 8:13

Simon himself also believed. Being baptized, he continued with Philip. Seeing signs and great miracles occuring, he was amazed.

Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana; Matendo ya Mitume 8:14

Now when the apostles who were at Jerusalem heard that Samaria had received the word of God, they sent Peter and John to them,

ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; Matendo ya Mitume 8:15

who, when they had come down, prayed for them, that they might receive the Holy Spirit;

kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Matendo ya Mitume 8:16

for as yet he had fallen on none of them. They had only been baptized in the name of Christ Jesus.

Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Matendo ya Mitume 8:17

Then they laid their hands on them, and they received the Holy Spirit.

Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, Matendo ya Mitume 8:18

Now when Simon saw that the Holy Spirit was given through the laying on of the apostles' hands, he offered them money,

Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. Matendo ya Mitume 8:19

saying, "Give me also this power, that whoever I lay my hands on may receive the Holy Spirit."

Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Matendo ya Mitume 8:20

But Peter said to him, "May your silver perish with you, because you thought you could obtain the gift of God with money!

Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. Matendo ya Mitume 8:21

You have neither part nor lot in this matter, for your heart isn't right before God.

Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako. Matendo ya Mitume 8:22

Repent therefore of this, your wickedness, and ask God if perhaps the thought of your heart may be forgiven you.

Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu. Matendo ya Mitume 8:23

For I see that you are in the gall of bitterness and in the bondage of iniquity."

Simoni akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Bwana, yasinifikilie mambo haya mliyosema hata moja. Matendo ya Mitume 8:24

Simon answered, "Pray for me to the Lord, that none of the things which you have spoken happen to me."

Nao walipokwisha kushuhudia na kulihubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemu, wakaihubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria. Matendo ya Mitume 8:25

They therefore, when they had testified and spoken the word of the Lord, returned to Jerusalem, and preached the Gospel to many villages of the Samaritans.

Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa. Matendo ya Mitume 8:26

But an angel of the Lord spoke to Philip, saying, "Arise, and go toward the south to the way that goes down from Jerusalem to Gaza. This is a desert."

Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, Matendo ya Mitume 8:27

He arose and went; and behold, there was a man of Ethiopia, a eunuch of great authority under Candace, queen of the Ethiopians, who was over all her treasure, who had come to Jerusalem to worship.

akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. Matendo ya Mitume 8:28

He was returning and sitting in his chariot, and was reading the prophet Isaiah.

Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. Matendo ya Mitume 8:29

The Spirit said to Philip, "Go near, and join yourself to this chariot."

Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? Matendo ya Mitume 8:30

Philip ran to him, and heard him reading Isaiah the prophet, and said, "Do you understand what you are reading?"

Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. Matendo ya Mitume 8:31

He said, "How can I, unless someone explains it to me?" He begged Philip to come up and sit with him.

Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. Matendo ya Mitume 8:32

Now the passage of the Scripture which he was reading was this, "He was led as a sheep to the slaughter. As a lamb before his shearer is silent, So he doesn't open his mouth.

Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi. Matendo ya Mitume 8:33

In his humiliation, his judgment was taken away. Who will declare His generation? For his life is taken from the earth."

Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? Matendo ya Mitume 8:34

The eunuch answered Philip, "Who is the prophet talking about? About himself, or about someone else?"

Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. Matendo ya Mitume 8:35

Philip opened his mouth, and beginning from this Scripture, preached to him Jesus.

Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? Matendo ya Mitume 8:36

As they went on the way, they came to some water, and the eunuch said, "Behold, here is water. What is keeping me from being baptized?"

Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.] Matendo ya Mitume 8:37

{TR adds "Philip said, 'If you believe with all your heart, you may.' He answered, 'I believe that Jesus Christ is the Son of God.'"}

Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. Matendo ya Mitume 8:38

He commanded the chariot to stand still, and they both went down into the water, both Philip and the eunuch, and he baptized him.

Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi. Matendo ya Mitume 8:39

When they came up out of the water, the Spirit of the Lord caught Philip away, and the eunuch didn't see him any more, for he went on his way rejoicing.

Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria. Matendo ya Mitume 8:40

But Philip was found at Azotus. Passing through, he preached the Gospel to all the cities, until he came to Caesarea.