Matendo ya Mitume 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 20 (Swahili) Acts 20 (English)

Kishindo kile kilipokoma, Paulo akatuma kuwaita wanafunzi akawaonya, akaagana nao, kisha akaondoka aende zake mpaka Makedonia. Matendo ya Mitume 20:1

After the uproar had ceased, Paul sent for the disciples, took leave of them, and departed to go into Macedonia.

Naye akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani. Matendo ya Mitume 20:2

When he had gone through those parts, and had encouraged them with many words, he came into Greece.

Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi kumfanyia vitimvi, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia. Matendo ya Mitume 20:3

When he had spent three months there, and a plot was made against him by Jews as he was about to set sail for Syria, he determined to return through Macedonia.

Watu hawa wakafuatana naye, Sopatro Mberoya, mwana wa Piro, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thesalonike; na Gayo mtu wa Derbe, na Timotheo; na Tikiko na Trofimo watu wa Asia. Matendo ya Mitume 20:4

These accompanied him as far as Asia: Sopater of Beroea; Aristarchus and Secundus of the Thessalonians; Gaius of Derbe; Timothy; and Tychicus and Trophimus of Asia.

Ila watu hao wamekwisha kutangulia wakamngojea Troa. Matendo ya Mitume 20:5

But these had gone ahead, and were waiting for us at Troas.

Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba. Matendo ya Mitume 20:6

We sailed away from Philippi after the days of Unleavened Bread, and came to them at Troas in five days, where we stayed seven days.

Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane. Matendo ya Mitume 20:7

On the first day of the week, when the disciples were gathered together to break bread, Paul talked with them, intending to depart on the next day, and continued his speech until midnight.

Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika. Matendo ya Mitume 20:8

There were many lights in the upper chamber where we{TR reads "they" instead of "we"} were gathered together.

Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa. Matendo ya Mitume 20:9

A certain young man named Eutychus sat in the window, weighed down with deep sleep. As Paul spoke still longer, being weighed down by his sleep, he fell down from the third story, and was taken up dead.

Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake. Matendo ya Mitume 20:10

Paul went down, and fell upon him, and embracing him said, "Don't be troubled, for his life is in him."

Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hata alfajiri, ndipo akaenda zake. Matendo ya Mitume 20:11

When he had gone up, and had broken bread, and eaten, and had talked with them a long while, even until break of day, he departed.

Wakamleta yule kijana, yu mzima, wakafarijika faraja kubwa sana. Matendo ya Mitume 20:12

They brought the boy in alive, and were greatly comforted.

Lakini sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukaabiri kwenda Aso, tukikusudia kumpakia Paulo huko; kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe aliazimu kwenda kwa miguu. Matendo ya Mitume 20:13

But we who went ahead to the ship set sail for Assos, intending to take Paul aboard there, for he had so arranged, intending himself to go by land.

Alipotufikia huko Aso, tukampakia, kisha tukafika Mitilene. Matendo ya Mitume 20:14

When he met us at Assos, we took him aboard, and came to Mitylene.

Tukatweka kutoka huko, na siku ya pili tukafika mahali panapokabili Kio; siku ya tatu tukawasili Samo, tukakaa Trogilio, siku ya nne tukafika Mileto. Matendo ya Mitume 20:15

Sailing from there, we came the following day opposite Chios. The next day we touched at Samos and stayed at Trogyllium, and the day after we came to Miletus.

Kwa sababu Paulo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka, akitaka kuwahi Yerusalemu siku ya Pentekoste, kama ikiwezekana. Matendo ya Mitume 20:16

For Paul had determined to sail past Ephesus, that he might not have to spend time in Asia; for he was hastening, if it were possible for him, to be in Jerusalem on the day of Pentecost.

Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa. Matendo ya Mitume 20:17

From Miletus he sent to Ephesus, and called to himself the elders of the assembly.

Walipofika kwake, akawaambia, Ninyi wenyewe mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu wakati wote, Matendo ya Mitume 20:18

When they had come to him, he said to them, "You yourselves know, from the first day that I set foot in Asia, how I was with you all the time,

nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na kwa machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi; Matendo ya Mitume 20:19

serving the Lord with all humility, with many tears, and with trials which happened to me by the plots of the Jews;

ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba, Matendo ya Mitume 20:20

how I didn't shrink from declaring to you anything that was profitable, teaching you publicly and from house to house,

nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo. Matendo ya Mitume 20:21

testifying both to Jews and to Greeks repentance toward God, and faith toward our Lord Jesus.{TR adds "Christ"}

Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko; Matendo ya Mitume 20:22

Now, behold, I go bound by the Spirit to Jerusalem, not knowing what will happen to me there;

isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. Matendo ya Mitume 20:23

except that the Holy Spirit testifies in every city, saying that bonds and afflictions wait for me.

Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu. Matendo ya Mitume 20:24

But these things don't count; nor do I hold my life dear to myself, so that I may finish my race with joy, and the ministry which I received from the Lord Jesus, to fully testify to the Gospel of the grace of God.

Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena. Matendo ya Mitume 20:25

Now, behold, I know that you all, among whom I went about preaching the Kingdom of God, will see my face no more.

Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina hatia kwa damu ya mtu awaye yote. Matendo ya Mitume 20:26

Therefore I testify to you this day that I am clean from the blood of all men,

Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu. Matendo ya Mitume 20:27

for I didn't shrink from declaring to you the whole counsel of God.

Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Matendo ya Mitume 20:28

Take heed, therefore, to yourselves, and to all the flock, in which the Holy Spirit has made you overseers, to shepherd the assembly of the Lord and{TR, NU omit "the Lord and"} God which he purchased with his own blood.

Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; Matendo ya Mitume 20:29

For I know that after my departure, vicious wolves will enter in among you, not sparing the flock.

tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. Matendo ya Mitume 20:30

Men will arise from among your own selves, speaking perverse things, to draw away the disciples after them.

Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi. Matendo ya Mitume 20:31

Therefore watch, remembering that for a period of three years I didn't cease to admonish everyone night and day with tears.

Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa. Matendo ya Mitume 20:32

Now, brothers,{The word for "brothers" here and where the context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} I entrust you to God, and to the word of his grace, which is able to build up, and to give you the inheritance among all those who are sanctified.

Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. Matendo ya Mitume 20:33

I coveted no one's silver, or gold, or clothing.

Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. Matendo ya Mitume 20:34

You yourselves know that these hands ministered to my necessities, and to those who were with me.

Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea. Matendo ya Mitume 20:35

In all things I gave you an example, that so laboring you ought to help the weak, and to remember the words of the Lord Jesus, that he himself said, 'It is more blessed to give than to receive.'"

Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote. Matendo ya Mitume 20:36

When he had spoken these things, he knelt down and prayed with them all.

Wakalia sana wote, wakamwangukia Paulo shingoni, wakambusu-busu, Matendo ya Mitume 20:37

They all wept a lot, and fell on Paul's neck and kissed him,

wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamwona uso tena. Wakamsindikiza hata merikebuni. Matendo ya Mitume 20:38

sorrowing most of all because of the word which he had spoken, that they should see his face no more. And they accompanied him to the ship.