Matendo ya Mitume 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Matendo ya Mitume 12 (Swahili) Acts 12 (English)

Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa. Matendo ya Mitume 12:1

Now about that time, Herod the king stretched out his hands to oppress some of the assembly.

Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga. Matendo ya Mitume 12:2

He killed James, the brother of John, with the sword.

Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa. Matendo ya Mitume 12:3

When he saw that it pleased the Jews, he proceeded to seize Peter also. This was during the days of unleavened bread.

Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu. Matendo ya Mitume 12:4

When he had arrested him, he put him in prison, and delivered him to four squads of four soldiers each to guard him, intending to bring him out to the people after the Passover.

Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. Matendo ya Mitume 12:5

Peter therefore was kept in the prison, but constant prayer was made by the assembly to God for him.

Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. Matendo ya Mitume 12:6

The same night when Herod was about to bring him out, Peter was sleeping between two soldiers, bound with two chains. Guards in front of the door kept the prison.

Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Matendo ya Mitume 12:7

And behold, an angel of the Lord stood by him, and a light shone in the cell. He struck Peter on the side, and woke him up, saying, "Stand up quickly!" His chains fell off from his hands.

Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. Matendo ya Mitume 12:8

The angel said to him, "Get dressed and put on your sandals." He did so. He said to him, "Put on your cloak, and follow me."

Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono. Matendo ya Mitume 12:9

And he went out and followed him. He didn't know that what was being done by the angel was real, but thought he saw a vision.

Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha. Matendo ya Mitume 12:10

When they were past the first and the second guard, they came to the iron gate that leads into the city, which opened to them by itself. They went out, and went down one street, and immediately the angel departed from him.

Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi. Matendo ya Mitume 12:11

When Peter had come to himself, he said, "Now I truly know that the Lord has sent out his angel and delivered me out of the hand of Herod, and from everything the Jewish people were expecting."

Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba. Matendo ya Mitume 12:12

Thinking about that, he came to the house of Mary, the mother of John whose surname was Mark, where many were gathered together and were praying.

Naye alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Roda, akaja kusikiliza. Matendo ya Mitume 12:13

When Peter knocked at the door of the gate, a maid named Rhoda came to answer.

Alipoitambua sauti ya Petro, hakukifungua lango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango. Matendo ya Mitume 12:14

When she recognized Peter's voice, she didn't open the gate for joy, but ran in, and reported that Peter was standing in front of the gate.

Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo hivyo. Wakanena, Ni malaika wake. Matendo ya Mitume 12:15

They said to her, "You are crazy!" But she insisted that it was so. They said, "It is his angel."

Petro akafuliza kugonga, hata walipokwisha kumfungulia wakamwona, wakastaajabu. Matendo ya Mitume 12:16

But Peter continued knocking. When they had opened, they saw him, and were amazed.

Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine. Matendo ya Mitume 12:17

But he, beckoning to them with his hand to be silent, declared to them how the Lord had brought him out of the prison. He said, "Tell these things to James, and to the brothers." Then he departed, and went to another place.

Hata kulipopambauka askari wakaingiwa na fadhaa nyingi, amekuwaje Petro. Matendo ya Mitume 12:18

Now as soon as it was day, there was no small stir among the soldiers about what had become of Peter.

Na Herode alipomtafuta, asimwone, aliwauliza-uliza wale walinzi, akaamuru wauawe. Kisha akatelemkia kutoka Uyahudi kwenda Kaisaria, akakaa huko. Matendo ya Mitume 12:19

When Herod had sought for him, and didn't find him, he examined the guards, and commanded that they should be put to death. He went down from Judea to Caesarea, and stayed there.

Naye Herode alikuwa amewakasirikia sana watu wa Tiro na Sidoni; wakamwendea kwa nia moja, na wakiisha kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulalia, wakataka amani; kwa maana nchi yao ilipata riziki kwa nchi ya mfalme. Matendo ya Mitume 12:20

Now Herod was very angry with the people of Tyre and Sidon. They came with one accord to him, and, having made Blastus, the king's chamberlain, their friend, they asked for peace, because their country depended on the king's country for food.

Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao. Matendo ya Mitume 12:21

On an appointed day, Herod dressed himself in royal clothing, sat on the throne, and gave a speech to them.

Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu. Matendo ya Mitume 12:22

The people shouted, "The voice of a god, and not of a man!"

Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho. Matendo ya Mitume 12:23

Immediately an angel of the Lord struck him, because he didn't give God the glory, and he was eaten by worms and died.

Neno la Bwana likazidi na kuenea. Matendo ya Mitume 12:24

But the word of God grew and multiplied.

Na Barnaba na Sauli, walipokwisha kutimiza huduma yao, wakarejea kutoka Yerusalemu, wakamchukua pamoja nao Yohana aitwaye Marko. Matendo ya Mitume 12:25

Barnabas and Saul returned to{TR reads "from" instead of "to"} Jerusalem, when they had fulfilled their service, also taking with them John whose surname was Mark.