Sifa Lyrics

Bora Kushukuru by Obby Alpha cover art

Obby Alpha - Bora Kushukuru Lyrics

Artist:
Obby Alpha

Lyrics

Verse 1

Bora hata nimshukuru Mungu Kwa hivi nilivyo,
Maana hata Kuna wengine hawajafika nilipo,
Bora hata nimshukuru Mungu Kwa hiki nilichopata,
Maana hata Kuna wengine wamekosa kabisa.

Tabasamu njoo,Nataka nibadiri
Wangu mtazamo niishi kitajiri
Na wewe maumivu njoo,Nataka nibadiri
Wangu msimamo niishi kijasiri,

Ile habari ya kulialia Kila siku nakataa (Nakataaa).
Na kama nilisainiwa mkataba nafuta aah,

Ndugu tulowasaidia wakaficha makucha (Makucha).
Wao walipofanikiwa wakataka kutushusha aah!!!

Bridge

Nafuta zile why me!! Why me!!
Sijapata kwanini ? Kwanini ?
Najawa ujasiri ujasiri
Nitapata na mimi na mimi

Nafuta zile why mimi Why mimi !!
Sijapata kwanini ? Kwanini ?
Najawa ujasiri ujasiri
Nitapata na mimi na mimi

Chorus

Bora hata nimshukuru Mungu Kwa hivi nilivyo,
Maana hata Kuna wengine hawajafika nilipo,
Bora hata nimshukuru Mungu Kwa hiki nilichopata,
Maana hata Kuna wengine wamekosa kabisa.

Verse 2

Na nilipo huenda Kuna wengine wanapatamani,

Zamani huko nilishakataliwa na watu wa nyumbani,

Kile kidogo ninacholalamika lakini nimepata,
Wengine huko wamepambana wamekosa kabisa.

Kumbe ni Bora kuridhika na hiki,
Nilichopata ndio yangu ridhiki,
Mungu ni Bora yeye hatabiriki,
Amekupa hicho mi amenipa hikii.

Video