Obby Alpha - Ananipenda Lyrics
Lyrics
[Verse 1]
Unashangaza Bwana kwa matendo yako ya ajabu
Toka mwaka jana, mwaka juzi na mwaka huu
Yale yote niliyoshindwa uliyafanya we
Na siwezi kuzimaliza sifa zako we, zako we
Baba unajua kupenda, unajua kujali
Hata wengine wakinikataa wewe unanikubali
[Chorus]
Leo niwaambie, waambie Mungu wangu ananipenda
Niwaambie, ambie Mungu wangu ananipenda
Dunia nzima wajue Mungu wangu ananipenda
Na dunia nzima wajue Mungu wangu ananipenda
[Bridge]
Yaani nikifanya kosa nikiomba toba ananisamehe, ananipenda
Huzuni ikinifika ananijaza furaha na amani tele, ananipenda
Ananipenda tu, ananipenda tu pe
Ananipenda tu, ananipenda upe
Ananipenda tu, ananipenda pe
Ananipenda tu, ananipenda
[Verse 2]
Eti saba mara sabini wala si hesabu zake hizo
Nikilaaniwa mimi anageuza baraka hizo
Alinikuta ninachechemea karibu yangu kanisogelea
Aliponiona mimi nalia machozi yangu kayafuta pia
Kwa hili pendo la Mungu kwa shetani nifuate nini hakuna
Na kwa hizi baraka za Mungu wacha leo niwaambie
[Chorus]
Waambie Mungu wangu ananipenda
Niwaambie waambie Mungu wangu ananipenda
Dunia nzima wajue Mungu wangu ananipenda
Na dunia nzima Mungu wangu ananipenda
[Bridge]
Nikifanya kosa nikiomba toba ananisamehe, ananipenda
Huzuni ikilifika ananijaza furaha na amani tele, ananipenda
Ananipenda tu, ananipenda pe
Ananipenda tu, ananipenda pe
Ananipenda tu, ananipenda pe
Ananipenda tu, ananipenda
[Outro]
Leo niwaambie, waambie Mungu wangu ananipenda
Niwaambie Mungu wangu ananipenda
Dunia nzima wajue Mungu wangu ananipenda
Na dunia nzima wajue Mungu wangu ananipenda
Nikifanya kosa nikiomba toba ananisamehe, ananipenda
Huzuni ikinifika ananijaza furaha na amani tele, ananipenda
Ananipenda tu, ananipenda pe...
Video
Ananipenda