Sifa Lyrics

Alikonitoa by Alphanny cover art

Alphanny - Alikonitoa Lyrics

Artist:
Alphanny
Album:
Alikonitoa - Single
Official Release:
24 Aug 2026

Lyrics

(Intro)
(Oweeh!!!)
Ni Alphanny tena
Alphanny


Verse 1
Mungu ni kila kitu kwangu
Na kila kitu kwangu ni bure bila Mungu
Nafasi yake moyoni mwangu ni permanent


Verse 2
Chukua biashara yangu mniache na Mungu
Chukua hata na nyumba yangu mniache na Mungu
Ukitaka chukua marafiki niache na Mungu wangu
Chukua mali yangu mniache na Mungu


Chorus
Maana mi najua alikonitoa Mungu
Mimi ninajua bila Mungu hivyo vyote havingekuwepo kwangu
Alinitoa chini matopeni kanioshaaa
(Kanifuta aibu)
Alinikung'uta mavumbi kanisafishaaa
Alikonitoa Mungu na mahali nimefika
Kweli ni Ebenezer wangu


Bridge
Hakunionyesha njia tu aliniongoza bwana
Hakunispoil na mavitu alinipa kinachonifaa
Maana ushindi wangu (ni neema)
Afya yangu (ni neema)
Na watoto wangu (ni neema)
Ni neema ni neema
Hata maisha yangu (ni neema)
Kicheko kwangu (ni neema)
Kazi yangu (ni neema)
Ni neema ni neema


Chorus
Maana mi najua alikonitoa Mungu
Mimi ninajua bila Mungu hivyo vyote havingekuwepo kwangu
Alinitoa chini matopeni kanioshaaa
(Kanifuta aibu)
Alinikung'uta mavumbi kanisafishaaa
Alikonitoa Mungu na mahali nimefika
Kweli ni Ebenezer wangu


Outro
Alikonitoa Mungu na mahali nimefika
Kweli ni Ebenezer wangu
(Mungu ni Ebenezer wangu)


Video