Sifa Lyrics

Nawakumbuka by Japhet Zabron cover art

Japhet Zabron - Nawakumbuka Lyrics

Artist:
Japhet Zabron
Album:
Nikumbuke
Official Release:
19 Mar 2022

Lyrics

Hebu nisikilizeni sasa niwaambie furaha yangu eeh
Najua kwamba sote ni ndugu na baba yetu mmoja'
Nawakumbuka waliodharauliwa hata kukosa dhamani
Mungu ndiye huinua hushusha mwamini atakuinua


Hata wale masikini, wale watoto wa mitaani
Najua maisha magumu kwenu ipo siku tutafika
Nawakumbuka wale waliochukiwa bure bila sababu
Wengine  vita na mama wa kambo, manyanyaso kila siku


Kuna walo zaa tena, wakawatupa watoto
Kuna wasiojiweza chakula kwao ni shida 
Kuna wanaotamani kutembea hawawezi
Walemavu na vipofu wakitamani kuponywa
Najua haya yote yapo sababu Mungu ndiye hupanga maisha


Katika maombi yangu nawakumbuka sana
Japo maisha ni shida, yasikutenge na Mungu
Endelea mwenzangu anajua nia yako
Ni mponyaji wa kweli ye ndo mgawa riziki
Kilio chako, hakika bwana anajua
Usichoke furaha yetu iko karibu


Katika maombi yangu nawakumbuka sana
Japo maisha ni shida, yasikutenge na Mungu
Endelea mwenzangu anajua nia yako
Ni mponyaji wa kweli ye ndo mgawa riziki
Kilio chako, hakika bwana anajua
Usichoke furaha yetu iko karibu


Nawakumbuka waliokataliwa duniani na wazazi eeh
Mama yako au baba mzazi wako alikukana aah
Najua dunia hii inachosha lakini usichoke ndugu
Ni baba wa wote wamchao Mungu ni mwaminifu eeh


Katika yeye nayaweza yote Mungu wangu hashindi eeh
Ni vyema nawakumbuka sasa tufurahi pamoja aah
Hata kama ni kifo kitutenge tutaishi pamoja eeh
Najua wengi wamepotea tena wawadhamini eeh


Ya nini uhuzunike mfariji wako yupo
Shida tunazopitia malipo yake uzima
Atawafuta machozi hautaona huzuni
Ajua makovu yako, majeraha ya dunia
Nawaombea wote msichoke ahadi yetu iko karibu 


Katika maombi yangu nawakumbuka sana
Japo maisha ni shida, yasikutenge na Mungu
Endelea mwenzangu anajua nia yako
Ni mponyaji wa kweli ye ndo mgawa riziki
Kilio chako, hakika bwana anajua
Usichoke furaha yetu iko karibu


Katika maombi yangu nawakumbuka sana
Japo maisha ni shida, yasikutenge na Mungu
Endelea mwenzangu anajua nia yako
Ni mponyaji wa kweli ye ndo mgawa riziki
Kilio chako, hakika bwana anajua
Usichoke furaha yetu iko karibu


Video