Japhet Zabron - Napungukiwa Nini Lyrics
Lyrics
Ndege, hawavuni Hawapandi wala hawafanyi kitu Mihangaiko, ya dunia sahau wala hawasumbukii Sauti tulivu Asabuhi huimba nakushukuru Wanamjua awapae kuishi kamwe hawahofu kitu Heeh’ ndivyo aishivyo amtumainie, muumba wa mbingu Hahangaiki hahofii dunia na masumbuko yajayo
Napungukiwa nini, Napungukiwa nini Nikiwa naye Yesu Sina kiu ya kitu Napungukiwa nini, Napungukiwa nini Nikiwa naye Yesu Sina kiu ya kitu
Huna tumaini Umekwama na kesho inakutisha Hufika muda Peke yako, njiani waongea na kulia Maisha mzigo Umetengwa wapendwa kukukimbia Nikukumbushe Yupo Yesu rafiki hata usiwaze kitu He he, ndivyo aishivyo Amtumainie muumba wa mbingu Hahangaikii hahofii dunia na masumbuko yajayo
Napungukiwa nini (nakosa nini) Napungukiwa nini (zaidi nini Baba) Nikiwa naye Yesu Sina kiu ya kitu Napungukiwa nini, Napungukiwa nini Nikiwa naye Yesu Sina kiu ya kitu
Mungu yupo upande wetu Nani atakae kaa juu yetu Tulia, tulia, tuliaa kwa Yesu
Video
Napungukiwa Nini by Japhet Zabron