Sifa Lyrics

Salimia Watu by Japhet Zabron cover art

Japhet Zabron - Salimia Watu Lyrics

Artist:
Japhet Zabron
Album:
Salimia Watu
Official Release:
27 Sep 2019

Lyrics

Si kuna Mungu, Mungu wa watu
Ndiye hutuweka pamoja
Huyu ni ndugu, yule rafiki
Wote ni kitu kimoja


Uwe m Israeli, uwe kabila la Yudah
Muumba wetu mmoja
Si tuliumbwa na Mungu, kuishi kwetu ni Mungu
Na uzima huu ni Mungu


Waishi vipi na watu wako wa mtaani
Hapa duniani
Utu kwa watu ndani yake twaona upendo
Uwapo hai duniani
Salimia watu pesa huisha


Salimia watu, utu ni utu, ongea na watu 
Ndio watakuzika kesho 
Salimia watu, utu ni utu, waheshimu watu
Pesa huisha 


Salimia watu, utu ni utu, ongea na watu 
Ndio watakuzika kesho 
Salimia watu, utu ni utu, waheshimu watu


Hakuna jambo lisilo mwisho 
Hata bado tujivune
Chini uhai, vitu na mali
Hivi vyote ni vya Mungu


Dunia hii tunapita na njia yetu ni moja
Kuna kifo na uzima 
Je unatenda ya Mungu, unatimiza ya Mungu
Wamtegemea Mungu


Kwa wema wenu, kwa watu twaona upendo
Upendo wa Mungu
Anatupenda hutuwazia mema kila siku


Tuwapo hai duniani, waheshimu watu
Pesa huisha 


Salimia watu, utu ni utu, ongea na watu 
Ndio watakuzika kesho 
Salimia watu, utu ni utu, waheshimu watu
Pesa huisha 


Salimia watu, utu ni utu, ongea na watu 
Ndio watakuzika kesho 
Salimia watu, utu ni utu, waheshimu watu


Salimia watu, ongea na watu
Salimia watu, waheshimu watu 
Salimia watu, ongea na watu
Salimia watu, waheshimu watu 


(Ishi na watu wapende watu)


Video