Japhet Zabron - Nikumbuke Lyrics
Lyrics
Nilipo waza kuomba Kazikumbuka dhambi zangu Zikanipa mashaka huenda hutojibu Ombeni na mtapewa Moyoni ukanikumbusha Nikapata nguvu za kusujudu tena Nikaanza kwa kuomba Unisamehe dhambi zangu Msamaha sasa wa Baba na mtoto Nikakumbuka nakuita Baba, nikawaza je kuna Baba Anae weza sikia sauti ya mwanae wala asijali Moyoni nikawaza si rahisi, utelekeze ombi langu Kama ni hivyo ombi langu leo Bwana mi naomba kukumbukwa
Nikumbuke, nikumbuke Yesu wangu (nami nikumbuke) Nisisahaulike kwa mazuri na wema wako (bwana nikumbuke) Unikumbuke na uyabebe magumu yangu (nami nikumbuke) Mi sikujua kumbe vita ni kubwa hivi (bwana nikumbuke) Unikumbuke ugawapo Baraka zako (nami nikumbuke) Nisisahaulike niwe mtu kati ya watu (bwana nikumbuke) Unikumbuke unapo ratibu mambo (nami nikumbuke) Yalipo mazuri bwana uweke na tiki zangu (bwana nikumbuke)
Umenifurahisha mungu, kwa hapa mimi nimefika Nakiri umenikumbuka Ni wewe huyu umefanya Matendo yako haya mungu Hayana mwisho kusimuliwa Nakushukuru mungu Baba Milele nitakutukuza Wanifurahisha zaidi Ukisha sema umesema Ni nani alojuu yako, na kama yupo na aseme Kama bahari tumevuka Iweje mito na milima Hakuna kama wewe mungu na hasa ukinikumbuka
Nikumbuke, nikumbuke Yesu wangu (nami nikumbuke) Nisisahaulike kwa mazuri na wema wako (bwana nikumbuke) Nikumbuke na uyabebe magumu yangu (nami nikumbuke) Mi sikujua kumbe vita ni kubwa hivi (bwana nikumbuke) Unikumbuke ugawapo Baraka zako (nami nikumbuke) Nisisahaulike niwe mtu kati ya watu (bwana nikumbuke) Unikumbuke unapo ratibu mambo (nami nikumbuke) Yalipo mazuri bwana uweke na tiki zangu (bwana nikumbuke)
Video
nikumbuke by Japhet Zabron (Official Video)