Sifa Lyrics

Bado Nasimama by Kambua cover art

Kambua - Bado Nasimama Lyrics

Artist:
Kambua

Lyrics

Bado nasimama, bado naendelea
Bado najikaza, nifike kule


Bila nehema na rehema zako, ningekuwa wapi mimi
Bila upendo, na fadhili zako, maisha yangu yangekuwa bure
Kwa wema wako, kanisimamisha
Na imani yangu, ukaiweka salama
Kama si wewe, Mwamba wa wokovu wangu
Nisingeweza. ningeangamia


Nainua macho yangu kwako wewe Baba yangu
Msaada wangu utatoka wapi
Msaada wangu u katika bwana
Hasinzii anilindaye, haniachi mimi niteleze
Anipa nguvu, na uwezo wake
Ili mimi nifike kule
Nifike kule


Bado nasimama, bado naendelea
Bado najikaza, nifike kule (x6)


Still Standing


Video