Japhet Zabron - Acha Yapite Lyrics

Album: Nikumbuke
Released: 19 Mar 2022
iTunes Amazon Music

Lyrics

Amani kuwa ndani ya moyo wako Ni muhimu kuliko maumivu ya moyo Nauona moyo wa hasira Juu yao watu wanao kulipa maovu Inashangaza kuona Ndugu au rafiki wa dhati Wote hawa waweza Kuwa maadui wa safari yako Ule upendo wa dhati Mungu anaotaka tuishi Watu wameuacha Chuki na hasira mioyo ni michafu

Acha yapite (japo kweli wanaudhi) Acha yapite yote (wanakwaza wanakatisha tamaa) Acha yaishe (japo waumia moyo) Acha yaishe (unawaza jinsi gani waonewa) Mimi najua (najua huna hatia hujakosa) Mungu ajua yote’h (hata mungu anajua) Acha yapite (japo kweli wanaudhi, wanakwaza wanakatisha tama) Acha yaishe (japo waumia moyo unawaza jinsi gani waonewa) Mimi najua (najua huna hatia hujakosa hata mungu anajua)

Waona Mengi zaidi ya haya Yakuudhi onewa na kusingiziwa Nauona Wema ndani ya moyo wako Uliwapa watu na sasa hata hawajui Kuwa na Yesu moyoni Bora kuliko vita na watu Moyo uwe huru usiyahesabu maudhi ya watu Ndio upendo wa dhati, mungu anaotaka tuishi Wa kuvumilia wa kuyasamehe na kuyasahau

Acha yapite (japo kweli wanaudhi, wanakwaza wanakatisha tamaa) Acha yapite yote Acha yaishe (japo waumia moyo, unawaza jinsi gani waonewa) Acha yaishe yote Mimi najua’h (najua huna hatia hujakosa, hata mungu anajua) Mungu ajua yote’h Acha yapite (japo kweli wanaudhi, wanakwaza wanakatisha tama) Acha yaishe (japo waumia moyo unawaza jinsi gani waonewa) Mimi najua (najua huna hatia hujakosa hata mungu anajua)

He he he Chanzo cha amani yako (samehe na kusahau) Haijalishi mangapi wamekudhi (yasamehe na kusahau) Chanzo cha amani yako kweli (samehe na kusahau) Haijalishi mangapi wamekudhi (yasamehe na kusahau)

Video

Acha Yapite by Japhet Zabron

Thumbnail for Acha Yapite video
Loading...
In Queue
View Lyrics