Sifa Lyrics

Nijaze by Janet Otieno cover art

Janet Otieno - Nijaze Lyrics

Artist:
Janet Otieno

Lyrics

Roho mtakatifu njoo utawale
Wewe uliye juu ya yote 
Ninakuomba utawale


Nataka nizame ndani na ndani
Zaidi, zaidi ya fahamu zangu
Sura yako iumbike kwangu
Mapenzi yako yatimizwe


Uwepo wako uwe fungu langu
Mi napendezwa sana nawe


Ewe roho wa Mungu
Fanya makao ndani yangu
Ewe pumzi yangu
Fanya makao ndani yangu


Nijaze nijaze
Nijaze bila kukoma
Nijaze nijaze
Nijaze bila kukoma


Mwalimu wa walimu
Nifunze leo nisiwe kikwazo cha uwepo wako
Ziteke hisia zangu ewe roho
Zisiwe kikwazo kwa nguvu zako


Rejesha kiu yako 
Nikutamani zaidi
Fungua sikio langu
Nikusikie zaidi


Maana hakuna kilicho na dhamani zaidi yako
Hakuna aliye na hekima kama yako
Wewe uchunguzaye mawazo ya Mungu
Naomba unijaze leo, ewe ewe


Ewe roho wa Mungu
Fanya makao ndani yangu
Ewe pumzi yangu
Fanya makao ndani yangu


Nijaze nijaze
Nijaze bila kukoma
Nijaze nijaze
Nijaze bila kukoma


Ewe roho wa Mungu
Fanya makao ndani yangu
Ewe pumzi yangu
Fanya makao ndani yangu


Nijaze nijaze
Nijaze bila kukoma
Nijaze nijaze
Nijaze bila kukoma


Video