Sifa Lyrics

Napokea kwako by Christina Shusho + Janet Otieno cover art

Christina Shusho + Janet Otieno - Napokea kwako Lyrics

Artist:
Christina Shusho + Janet Otieno

Lyrics

Maisha magumu sana nimepitia
Nikajaribu kutafuta msaada sikupata
Nikaendea mwanadamu mwisho akanidharau
Kumbe msaada wa mwanadamu unatoka kwa Mungu


Nilijua yapo wenye haki ya kubarikiwa
Kumbe Baraka ni haki ya kila mmoja


Nimebadili wazo langu namwelekea Mungu
Kwake msaada wangu unapatikana


Msaada wa mwanadamu ni wa muda mfupi
Na ni zamu yangu kubarikiwa we


Wakati ni huu wa kubarikiwa
Zamu ni yangu, sasa kupokea
Nimechoshwa na shida za dunia
Napokea kwako, Baba napokea kwako,
Napokea kwako, Baba napokea kwako,
Napokea kwako, Yesu napokea kwako
Napokea kwako, Baba napokea kwako,


Nimeamua kwenda Zaidi na Zaidi
Nimejipanga hadi nione matunda yake


Yale Mungu amewekeza ndani yangu
Najua Mungu yupo kazini kunikamilisha


Akisema nimebarikiwa nimebarikiwa tu
Hata ukipinga leo mimi nimebarikiwa tu


Mlima gani kuu sana usiloung’oa
Jaribu gani kuu sana usiloliweza
Chozi gani zito kwako usilolifuta
Ombi gani kubwa sana usilolijibu


Wakati ni huu wa kubarikiwa
Zamu ni yangu, sasa kupokea
Nimechoshwa na shida za dunia
Napokea kwako, Baba napokea kwako,
Napokea kwako, Baba napokea kwako,
Napokea kwako, Yesu napokea kwako
Napokea kwako, Baba napokea kwako


Wakati ni huu wa kubarikiwa
Zamu ni yangu, sasa kupokea
Nimechoshwa na shida za dunia
Napokea kwako, Baba napokea kwako,
Napokea kwako, Baba napokea kwako,
Napokea kwako, Yesu napokea kwako
Napokea kwako, Baba napokea kwako


Video