Tenda wema nenda zake wee
Usisahau Mungu anaona
Siku kuhukumu kuwa itafika
Mayatima umesomesha sana
Wenye shida umesaidia wote
Wenye njaa umewapa chakula
Nguo zako umepeana zote
Hakuna anayetambua yale umetenda kwote
Sasa naona inakupa worry nakuomba wewe usijali
Aliyekuita anaona yote, tabariki ya siku zote
Tenda wema nenda zako wee
Usisahau Mungu anaona
Siku kuhukumu kuwa itafika
Aliwaponya wagonjwwa wao ni Yesu huyo
Akafufua wafu wao ni Yesu Huyo
Mwisho wakamwita pepo huyo ooh
Na tena wakamwita Belizeburi
Wewe si wa kwanza na hutakuwa wa mwisho
Yesu katukanwa sembuse mwanadamu
Tenda wema nenda zako wee
Usingoje shukurani eeh
Usisahau Mungu anaona
Siku kuhukumu kuwa itafika
Tenda wema nenda zako wee
Usisahau Mungu anaona
Siku kuhukumu kuwa itafika
Utawasomesha wajue kizungu wakutusi
Utawalisha washibe wakupige
Wewe tenda mema, wewe tenda mema tu
Tenda wema nenda zako wee
Usisahau Mungu anaona
Siku kuhukumu kuwa itafika