Mambo ya Walawi 25 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 25 (Swahili) Leviticus 25 (English)

Kisha Bwana akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia, Mambo ya Walawi 25:1

Yahweh said to Moses in Mount Sinai,

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya Bwana. Mambo ya Walawi 25:2

"Speak to the children of Israel, and tell them, 'When you come into the land which I give you, then the land shall keep a Sabbath to Yahweh.

Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake; Mambo ya Walawi 25:3

Six years you shall sow your field, and six years you shall prune your vineyard, and gather in its fruits;

lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu. Mambo ya Walawi 25:4

but in the seventh year there shall be a Sabbath of solemn rest for the land, a Sabbath to Yahweh. You shall not sow your field or prune your vineyard.

Hicho kimeacho chenyewe katika mavuno yako, usikivune, wala zabibu za mizabibu isiyopelewa usizitunde; utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi. Mambo ya Walawi 25:5

What grows of itself in your harvest you shall not reap, and the grapes of your undressed vine you shall not gather. It shall be a year of solemn rest for the land.

Na hiyo Sabato ya nchi itakuwa chakula kwenu; kwako wewe, na kwa mtumwa wako, na kwa mjakazi wako, na kwa mtumishi aliyeajiriwa, na kwa mgeni wako akaaye pamoja nawe; Mambo ya Walawi 25:6

The Sabbath of the land shall be for food for you; for yourself, for your servant, for your maid, for your hired servant, and for your stranger, who lives as a foreigner with you.

na kwa hayawani wako, na kwa wanyama walio katika nchi yako; maongeo yote yatakuwa ni chakula chao. Mambo ya Walawi 25:7

For your cattle also, and for the animals that are in your land, shall all the increase of it be for food.

Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda. Mambo ya Walawi 25:8

"'You shall count off seven Sabbaths of years, seven times seven years; and there shall be to you the days of seven Sabbaths of years, even forty-nine years.

Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. Mambo ya Walawi 25:9

Then you shall sound the loud trumpet on the tenth day of the seventh month. On the Day of Atonement you shall sound the trumpet throughout all your land.

Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake. Mambo ya Walawi 25:10

You shall make the fiftieth year holy, and proclaim liberty throughout the land to all its inhabitants. It shall be a jubilee to you; and each of you shall return to his own property, and each of you shall return to his family.

Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa. Mambo ya Walawi 25:11

That fiftieth year shall be a jubilee to you. In it you shall not sow, neither reap that which grows of itself, nor gather from the undressed vines.

Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani. Mambo ya Walawi 25:12

For it is a jubilee; it shall be holy to you. You shall eat of its increase out of the field.

Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake. Mambo ya Walawi 25:13

"'In this Year of Jubilee each of you shall return to his property.

Tena kama ukimwuzia jirani yako cho chote, au kununua cho chote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe; Mambo ya Walawi 25:14

"'If you sell anything to your neighbor, or buy from your neighbor, you shall not wrong one another.

kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe. Mambo ya Walawi 25:15

According to the number of years after the Jubilee you shall buy from your neighbor. According to the number of years of the crops he shall sell to you.

Kama hesabu ya miaka ilivyo ni nyingi ndivyo utakavyoongeza bei yake, na kama hesabu ya miaka ilivyo ni chache ndivyo utakavyopunguza bei yake; kwani yeye akuuzia mavuno kama hesabu yake ilivyo. Mambo ya Walawi 25:16

According to the length of the years you shall increase the price of it, and according to the shortness of the years you shall diminish the price of it; for he is selling the number of the crops to you.

Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Mambo ya Walawi 25:17

You shall not wrong one another; but you shall fear your God: for I am Yahweh your God.

Kwa sababu hii zitendeni amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzifanya; nanyi mtakaa katika hiyo nchi salama. Mambo ya Walawi 25:18

"'Therefore you shall do my statutes, and keep my ordinances and do them; and you shall dwell in the land in safety.

Nayo nchi itazaa matunda yake, nanyi mtakula na kushiba, na kuketi humo salama. Mambo ya Walawi 25:19

The land shall yield its fruit, and you shall eat your fill, and dwell therein in safety.

Na kama mkisema, Je! Mwaka wa saba tutakula nini? Angalieni hatutapanda mbegu, wala kukusanya maongeo yetu; Mambo ya Walawi 25:20

If you said, "What shall we eat the seventh year? Behold, we shall not sow, nor gather in our increase;"

ndipo nitawaamria baraka yangu iwe juu yenu mwaka wa sita, nayo utazaa matunda hesabu ya miaka mitatu. Mambo ya Walawi 25:21

then I will command my blessing on you in the sixth year, and it shall bring forth fruit for the three years.

Na mwaka wa nane mtapanda mbegu, na kuyala yale matunda, akiba hiyo ya zamani, hata mwaka wa kenda, hata matunda yake yatakapoletwa ndani, mtakula hiyo akiba ya zamani. Mambo ya Walawi 25:22

You shall sow the eighth year, and eat of the fruits, the old store; until the ninth year, until its fruits come in, you shall eat the old store.

Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wasafiri wangu. Mambo ya Walawi 25:23

"'The land shall not be sold in perpetuity, for the land is mine; for you are strangers and live as foreigners with me.

Nanyi mtatoa ukombozi kwa ajili ya nchi, katika nchi yote ya milki yenu. Mambo ya Walawi 25:24

In all the land of your possession you shall grant a redemption for the land.

Kwamba nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye. Mambo ya Walawi 25:25

"'If your brother becomes poor, and sells some of his possessions, then his kinsman who is next to him shall come, and redeem that which his brother has sold.

Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo ya kutosha kuikomboa; Mambo ya Walawi 25:26

If a man has no one to redeem it, and he becomes prosperous and finds sufficient means to redeem it;

ndipo na aihesabu hiyo miaka ya kuuzwa kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua; naye atairejea milki yake. Mambo ya Walawi 25:27

then let him reckon the years since the sale of it, and restore the surplus to the man to whom he sold it; and he shall return to his property.

Lakini asipoweza kujipatia mwenyewe, ndipo hiyo iliyouzwa itakaa mkononi mwake huyo aliyeinunua, hata mwaka wa yubile; na katika yubile itatoka, naye atairejea milki yake. Mambo ya Walawi 25:28

But if he isn't able to get it back for himself, then what he has sold shall remain in the hand of him who has bought it until the Year of Jubilee: and in the Jubilee it shall be released, and he shall return to his propery.

Tena kwamba mtu anauza nyumba ya kukaa, iliyo ndani ya mji wenye kuta, ndipo ana ruhusa kuikomboa katika mwaka mmoja mzima baada ya kuiuza; atakuwa na amri ya kuikomboa muda wa mwaka mzima. Mambo ya Walawi 25:29

"'If a man sells a dwelling house in a walled city, then he may redeem it within a whole year after it has been sold. For a full year he shall have the right of redemption.

Na kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake; nayo haitatoka katika yubile. Mambo ya Walawi 25:30

If it isn't redeemed within the space of a full year, then the house that is in the walled city shall be made sure in perpetuity to him who bought it, throughout his generations. It shall not be released in the Jubilee.

Lakini nyumba za vijiji, ambavyo havikuzingirwa na kuta, zitahesabiwa pamoja na mashamba ya nchi; nazo zina ruhusa ya kukombolewa, nazo zitatoka katika yubile. Mambo ya Walawi 25:31

But the houses of the villages which have no wall round about them shall be reckoned with the fields of the country: they may be redeemed, and they shall be released in the Jubilee.

Pamoja na hayo, miji ya Walawi, nyumba za miji ya milki yao, Walawi wana ruhusa ya kuzikomboa majira yo yote. Mambo ya Walawi 25:32

"'Nevertheless the cities of the Levites, the houses in the cities of their possession, the Levites may redeem at any time.

Tena kama mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa, ndipo nyumba iliyouzwa, na mji wa milki yake, itatoka katika yubile; maana, hizo nyumba za miji ya Walawi ni milki yao kati ya wana wa Israeli. Mambo ya Walawi 25:33

The Levites may redeem the house that was sold, and the city of his possession, and it shall be released in the Jubilee; for the houses of the cities of the Levites are their possession among the children of Israel.

Lakini konde la malisho ya miji yao lisiuzwe kwa kuwa ni milki yao ya daima. Mambo ya Walawi 25:34

But the field of the suburbs of their cities may not be sold; for it is their perpetual possession.

Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri. Mambo ya Walawi 25:35

"'If your brother has become poor, and his hand can't support him among you; then you shall uphold him. As a stranger and a sojourner he shall live with you.

Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe. Mambo ya Walawi 25:36

Take no interest from him or profit, but fear your God; that your brother may live among you.

Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida. Mambo ya Walawi 25:37

You shall not lend him your money at interest, nor give him your food for profit.

Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu. Mambo ya Walawi 25:38

I am Yahweh your God, who brought you forth out of the land of Egypt, to give you the land of Canaan, and to be your God.

Tena kwamba nduguyo amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimtumikishe mfano wa mtumwa; Mambo ya Walawi 25:39

"'If your brother has grown poor among you, and sells himself to you; you shall not make him to serve as a slave.

kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au mfano wa msafiri; naye atatumika kwako hata mwaka wa yubile; Mambo ya Walawi 25:40

As a hired servant, and as a sojourner, he shall be with you; he shall serve with you until the Year of Jubilee:

ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake. Mambo ya Walawi 25:41

then he shall go out from you, he and his children with him, and shall return to his own family, and to the possession of his fathers.

Kwa kuwa hao ni watumishi wangu, niliowaleta watoke nchi ya Misri; wasiuzwe mfano wa watumwa. Mambo ya Walawi 25:42

For they are my servants, whom I brought forth out of the land of Egypt. They shall not be sold as slaves.

Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako. Mambo ya Walawi 25:43

You shall not rule over him with harshness, but shall fear your God.

Tena katika habari za watumwa wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando-kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na wajakazi. Mambo ya Walawi 25:44

"'As for your male and your female slaves, whom you may have; of the nations that are around you, from them you may buy male and female slaves.

Tena katika wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu. Mambo ya Walawi 25:45

Moreover of the children of the strangers who sojourn among you, of them you may buy, and of their families who are with you, which they have conceived in your land; and they will be your property.

Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumwa wenu katika hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana wa Israeli, wenyewe kwa wenyewe. Mambo ya Walawi 25:46

You may make them an inheritance for your children after you, to hold for a possession; of them may you take your slaves forever: but over your brothers the children of Israel you shall not rule, one over another, with harshness.

Tena kama mgeni au mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni; Mambo ya Walawi 25:47

"'If a stranger or sojourner with you becomes rich, and your brother beside him has grown poor, and sells himself to the stranger or foreigner living among you, or to a member of the stranger's family;

baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni mwa ndugu zake ana ruhusa kumkomboa; Mambo ya Walawi 25:48

after he is sold he may be redeemed. One of his brothers may redeem him;

au mjomba wake, au mwana wa mjomba wake, ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu awaye yote aliye karibu naye wa jamaa yake, ana ruhusa ya kumkomboa; au kwamba yeye mwenyewe amepata mali, ana ruhusa ya kujikomboa mwenyewe. Mambo ya Walawi 25:49

or his uncle, or his uncle's son, may redeem him, or any who is a close relative to him of his family may redeem him; or if he has grown rich, he may redeem himself.

Naye atafanya hesabu na huyo aliyemnunua, tangu mwaka huo aliojiuza hata mwaka wa yubile; na ile bei ya kuuzwa kwake itakuwa kama hesabu ya hiyo miaka ilivyo; atakuwa pamoja naye kama majira ya mtumishi aliyeajiriwa yalivyo. Mambo ya Walawi 25:50

He shall reckon with him who bought him from the year that he sold himself to him to the Year of Jubilee: and the price of his sale shall be according to the number of years; according to the time of a hired servant shall he be with him.

Kwamba ikali imesalia miaka mingi, kama hesabu yake ilivyo ndivyo atakavyolipa bei ya ukombozi wake, katika hiyo fedha ambayo alinunuliwa kwayo. Mambo ya Walawi 25:51

If there are yet many years, according to them he shall give back the price of his redemption out of the money that he was bought for.

Tena kwamba imesalia miaka michache tu hata mwaka wa yubile, ndipo atafanya hesabu naye, kama hesabu ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi wake. Mambo ya Walawi 25:52

If there remain but a few years to the year of jubilee, then he shall reckon with him; according to his years of service he shall give back the price of his redemption.

Kama mtumishi aliyeajiriwa mwaka hata mwaka, ndivyo atakavyokuwa pamoja naye; asitawale juu yake kwa nguvu mbele ya macho yako. Mambo ya Walawi 25:53

As a servant hired year by year shall he be with him: he shall not rule with harshness over him in your sight.

Tena kwamba hakukombolewa kwa njia hizi mojawapo, ndipo atatoka katika mwaka wa yubile, yeye, na watoto wake pamoja naye. Mambo ya Walawi 25:54

"'If he isn't redeemed by these means, then he shall be released in the Year of Jubilee, he, and his children with him.

Kwa kuwa wana wa Israeli ni watumishi; ni watumishi wangu niliowaleta watoke katika nchi ya Misri; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Mambo ya Walawi 25:55

For to me the children of Israel are servants; they are my servants whom I brought forth out of the land of Egypt. I am Yahweh your God.