Mambo ya Walawi 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 4 (Swahili) Leviticus 4 (English)

Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 4:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo Bwana amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo; Mambo ya Walawi 4:2

"Speak to the children of Israel, saying, 'If anyone sins unintentionally, in any of the things which Yahweh has commanded not to be done, and does any one of them:

kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa Bwana ng'ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi. Mambo ya Walawi 4:3

if the anointed priest sins so as to bring guilt on the people, then let him offer for his sin, which he has sinned, a young bull without blemish to Yahweh for a sin offering.

Naye atamleta huyo ng'ombe na kumweka mlangoni pa hiyo hema ya kukutania, mbele za Bwana; naye ataweka mkono wake kichwani mwake ng'ombe, na kumchinja huyo ng'ombe mbele za Bwana. Mambo ya Walawi 4:4

He shall bring the bull to the door of the Tent of Meeting before Yahweh; and he shall lay his hand on the head of the bull, and kill the bull before Yahweh.

Kisha huyo kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa baadhi ya damu ya huyo ng'ombe, na kuileta ndani ya hiyo hema ya kukutania; Mambo ya Walawi 4:5

The anointed priest shall take some of the blood of the bull, and bring it to the Tent of Meeting.

kisha kuhani atatia kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza damu mbele ya Bwana mara saba, mbele ya pazia la mahali patakatifu. Mambo ya Walawi 4:6

The priest shall dip his finger in the blood, and sprinkle some of the blood seven times before Yahweh, before the veil of the sanctuary.

Kisha kuhani atatia baadhi ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba mzuri mbele ya Bwana iliyo ndani ya hema ya kukutania; kisha damu yote ya huyo ng'ombe ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyoko mlangoni pa hema ya kukutania. Mambo ya Walawi 4:7

The priest shall put some of the blood on the horns of the altar of sweet incense before Yahweh, which is in the tent of meeting; and he shall pour out all the blood of the bull out at the base of the altar of burnt offering, which is at the door of the Tent of Meeting.

Kisha mafuta yote ya huyo ng'ombe wa sadaka ya dhambi atayaondoa; mafuta yote yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo, Mambo ya Walawi 4:8

He shall take all the fat of the bull of the sin offering off of it; the fat that covers the innards, and all the fat that is on the innards,

na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo, hayo yote atayaondoa, Mambo ya Walawi 4:9

and the two kidneys, and the fat that is on them, which is by the loins, and the cover on the liver, with the kidneys, he shall take away,

vile vile kama yanavyoondolewa katika ng'ombe wa kuchinjwa kwa sadaka za amani; kisha huyo kuhani atayateketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Mambo ya Walawi 4:10

as it is taken off of the ox of the sacrifice of peace offerings. The priest shall burn them on the altar of burnt offering.

Kisha ngozi yake ng'ombe, na nyama yake yote, pamoja na kichwa chake, na pamoja na miguu yake, na matumbo yake, na mavi yake, Mambo ya Walawi 4:11

The bull's skin, all its flesh, with its head, and with its legs, its innards, and its dung,

maana, huyo ng'ombe mzima atamchukua nje ya marago hata mahali safi, hapo wamwagapo majivu, naye atamchoma moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo majivu yamwagwapo. Mambo ya Walawi 4:12

even the whole bull shall he carry forth outside the camp to a clean place, where the ashes are poured out, and burn it on wood with fire. Where the ashes are poured out it shall be burned.

Na kama mkutano mzima wa Israeli ukifanya dhambi, na jambo lenyewe likayafichamania macho ya huo mkutano, nao wamefanya mojawapo katika mambo yaliyozuiliwa na Bwana, kwamba wasiyafanye, nao wamepata hatia; Mambo ya Walawi 4:13

"'If the whole congregation of Israel sins, and the thing is hidden from the eyes of the assembly, and they have done any of the things which Yahweh has commanded not to be done, and are guilty;

hapo itakapojulikana hiyo dhambi waliyoifanya, ndipo mkutano utatoa ng'ombe mume mchanga awe sadaka ya dhambi, na kumleta mbele ya hema ya kukutania. Mambo ya Walawi 4:14

when the sin in which they have sinned is known, then the assembly shall offer a young bull for a sin offering, and bring it before the Tent of Meeting.

Kisha wazee wa mkutano wataweka mikono yao kichwani mwake huyo ng'ombe mbele za Bwana; Mambo ya Walawi 4:15

The elders of the congregation shall lay their hands on the head of the bull before Yahweh; and the bull shall be killed before Yahweh.

kisha ng'ombe atachinjwa mbele za Bwana. Kisha kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa katika damu ya huyo ng'ombe na kuileta ndani ya hema ya kukutania; Mambo ya Walawi 4:16

The anointed priest shall bring of the blood of the bull to the Tent of Meeting:

kisha kuhani atatia kidole chake katika hiyo damu, na kuinyunyiza mbele za Bwana, mbele ya pazia mara saba. Mambo ya Walawi 4:17

and the priest shall dip his finger in the blood, and sprinkle it seven times before Yahweh, before the veil.

Kisha nyingine katika hiyo damu ataitia katika pembe za madhabahu iliyo mbele za Bwana, iliyoko ndani ya hema ya kukutania, kisha damu yote ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo mlangoni pa hema ya kukutania. Mambo ya Walawi 4:18

He shall put some of the blood on the horns of the altar which is before Yahweh, that is in the Tent of Meeting; and the rest of the blood he shall pour out at the base of the altar of burnt offering, which is at the door of the Tent of Meeting.

Kisha atayaondoa mafuta yake yote na kuyateketeza juu ya madhabahu. Mambo ya Walawi 4:19

All its fat he shall take from it, and burn it on the altar.

Ndivyo atakavyomfanyia huyo ng'ombe; kama alivyomfanyia huyo ng'ombe wa sadaka ya dhambi, atamfanyia na huyu vivyo; naye kuhani atawafanyia upatanisho, nao watasamehewa. Mambo ya Walawi 4:20

Thus shall he do with the bull; as he did with the bull of the sin offering, so shall he do with this; and the priest shall make atonement for them, and they shall be forgiven.

Kisha atamchukua huyo ng'ombe nje ya marago, na kumchoma moto vile vile kama alivyomchoma moto ng'ombe wa kwanza; ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mkutano. Mambo ya Walawi 4:21

He shall carry forth the bull outside the camp, and burn it as he burned the first bull. It is the sin offering for the assembly.

Mtawala atakapofanya dhambi, na kutenda pasipo kukusudia neno lo lote katika hayo ambayo Bwana, Mungu wake, aliyazuilia yasifanywe, naye amepata hatia; Mambo ya Walawi 4:22

"'When a ruler sins, and unwittingly does any one of all the things which Yahweh his God has commanded not to be done, and is guilty;

akijulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya, ataleta mbuzi awe matoleo yake, mume, mkamilifu; Mambo ya Walawi 4:23

if his sin, in which he has sinned, is made known to him, he shall bring as his offering a goat, a male without blemish.

kisha ataweka mkono wake kichwani mwake huyo mbuzi, na kumchinja hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa mbele za Bwana; ni sadaka ya dhambi. Mambo ya Walawi 4:24

He shall lay his hand on the head of the goat, and kill it in the place where they kill the burnt offering before Yahweh. It is a sin offering.

Kisha kuhani atatwaa katika damu ya hiyo sadaka ya dhambi kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, nayo damu yake ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya kuteketeza. Mambo ya Walawi 4:25

The priest shall take some of the blood of the sin offering with his finger, and put it on the horns of the altar of burnt offering. He shall pour out the rest of its blood at the base of the altar of burnt offering.

Na mafuta yake yote atayateketeza juu ya madhabahu, kama alivyoyateketeza mafuta ya hizo sadaka za amani; naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa. Mambo ya Walawi 4:26

All its fat he shall burn on the altar, like the fat of the sacrifice of peace offerings; and the priest shall make atonement for him concerning his sin, and he will be forgiven.

Na mtu awaye yote katika watu wa nchi akifanya dhambi pasipo kukusudia, kwa kufanya neno lo lote katika hayo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe, naye akapata hatia; Mambo ya Walawi 4:27

"'If anyone of the common people sins unwittingly, in doing any of the things which Yahweh has commanded not to be done, and is guilty;

akijulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya, ndipo atakapoleta mbuzi mke mkamilifu, awe matoleo yake kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya. Mambo ya Walawi 4:28

if his sin, which he has sinned, is made known to him, then he shall bring for his offering a goat, a female without blemish, for his sin which he has sinned.

Naye ataweka mkono wake kichwani mwake hiyo sadaka ya dhambi, na kumchinja sadaka ya dhambi mahali hapo pa sadaka ya kuteketezwa. Mambo ya Walawi 4:29

He shall lay his hand on the head of the sin offering, and kill the sin offering in the place of burnt offering.

Kisha kuhani atatwaa katika hiyo damu yake kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya kuteketeza na damu yake yote ataimwaga chini ya madhabahu. Mambo ya Walawi 4:30

The priest shall take some of its blood with his finger, and put it on the horns of the altar of burnt offering; and the rest of its blood he shall pour out at the base of the altar.

Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, iwe harufu ya kupendeza kwa Bwana; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa. Mambo ya Walawi 4:31

All its fat he shall take away, like the fat is taken away from off of the sacrifice of peace offerings; and the priest shall burn it on the altar for a sweet savor to Yahweh; and the priest shall make atonement for him, and he will be forgiven.

Naye akileta mwana-kondoo kuwa sadaka ya dhambi, ataleta wa kike mkamilifu. Mambo ya Walawi 4:32

"'If he brings a lamb as his offering for a sin offering, he shall bring a female without blemish.

Naye ataweka mkono wake kichwani mwake sadaka ya dhambi, kisha atamchinja awe sadaka ya dhambi, mahali hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa. Mambo ya Walawi 4:33

He shall lay his hand on the head of the sin offering, and kill it for a sin offering in the place where they kill the burnt offering.

Kisha kuhani atatwaa katika hiyo damu ya sadaka ya kuteketezwa kwa kidole chake na kuitia katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, kisha damu yake yote ataimwaga hapo chini ya madhabahu; Mambo ya Walawi 4:34

The priest shall take some of the blood of the sin offering with his finger, and put it on the horns of the altar of burnt offering; and all the rest of its blood he shall pour out at the base of the altar.

kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama mafuta ya mwana-kondoo yalivyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kwa desturi ya hizo sadaka za Bwana zilizosongezwa kwa njia ya moto; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, naye atasamehewa. Mambo ya Walawi 4:35

All its fat he shall take away, like the fat of the lamb is taken away from the sacrifice of peace offerings; and the priest shall burn them on the altar, on the offerings of Yahweh made by fire; and the priest shall make atonement for him concerning his sin that he has sinned, and he will be forgiven.