Mambo ya Walawi 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 17 (Swahili) Leviticus 17 (English)

Bwana akamwambia Musa, akisema, Mambo ya Walawi 17:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Sema na Haruni, na wanawe, na wana wote wa Israeli, ukawaambie; Neno hili ndilo aliloliamuru Bwana, akisema, Mambo ya Walawi 17:2

"Speak to Aaron, and to his sons, and to all the children of Israel, and say to them: 'This is the thing which Yahweh has commanded,

Mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli atakayechinja ng'ombe, au mwana-kondoo, au mbuzi, ndani ya marago, au atakayemchinja nje ya marago, Mambo ya Walawi 17:3

Whatever man there is of the house of Israel, who kills an ox, or lamb, or goat, in the camp, or who kills it outside the camp,

wala hamleti mlangoni pa hema ya kukutania, ili amtoe kuwa matoleo kwa Bwana mbele ya hema ya Bwana; mtu huyo atahesabiwa kuwa ana hatia ya damu; amemwaga damu; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake; Mambo ya Walawi 17:4

and hasn't brought it to the door of the Tent of Meeting, to offer it as an offering to Yahweh before the tabernacle of Yahweh: blood shall be imputed to that man. He has shed blood; and that man shall be cut off from among his people.

ili kusudi wana wa Israeli walete sadaka zao, wazichinjazo mashambani, naam, wazilete kwa Bwana, mpaka mlango wa hema ya kukutania, kwa huyo kuhani, ili wazichinje ziwe sadaka za amani kwa Bwana. Mambo ya Walawi 17:5

This is to the end that the children of Israel may bring their sacrifices, which they sacrifice in the open field, that they may bring them to Yahweh, to the door of the Tent of Meeting, to the priest, and sacrifice them for sacrifices of peace offerings to Yahweh.

Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya Bwana, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za Bwana. Mambo ya Walawi 17:6

The priest shall sprinkle the blood on the altar of Yahweh at the door of the Tent of Meeting, and burn the fat for a sweet savor to Yahweh.

Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi. Mambo ya Walawi 17:7

They shall no more sacrifice their sacrifices to the goat idols, after which they play the prostitute. This shall be a statute forever to them throughout their generations.'

Nawe utawaambia, Mtu awaye yote katika nyumba ya Israeli, au miongoni mwa wageni, wanaokaa nao, atoaye sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, Mambo ya Walawi 17:8

"You shall say to them, 'Any man there is of the house of Israel, or of the strangers who live as foreigners among them, who offers a burnt offering or sacrifice,

wala haileti mlangoni pa hema ya kukutania, ili aisongeze kwa Bwana basi mtu huyo atatengwa na watu wake. Mambo ya Walawi 17:9

and doesn't bring it to the door of the Tent of Meeting, to sacrifice it to Yahweh; that man shall be cut off from his people.

Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Mambo ya Walawi 17:10

"'Any man of the house of Israel, or of the strangers who live as foreigners among them, who eats any kind of blood, I will set my face against that soul who eats blood, and will cut him off from among his people.

Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. Mambo ya Walawi 17:11

For the life of the flesh is in the blood; and I have given it to you on the altar to make atonement for your souls: for it is the blood that makes atonement by reason of the life.

Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aketiye kati yenu asile damu. Mambo ya Walawi 17:12

Therefore I have said to the children of Israel, "No person among you shall eat blood, neither shall any stranger who lives as a foreigner among you eat blood."

Mtu ye yote aliye wa wana wa Israeli, au wa hao wageni wakaao kati yenu, ambaye amemshika mnyama, au ndege ambaye huliwa, katika kuwinda kwake; atamwaga damu yake, na kuifunika mchanga. Mambo ya Walawi 17:13

"'Whatever man there is of the children of Israel, or of the strangers who live as foreigners among them, who takes in hunting any animal or bird that may be eaten; he shall pour out its blood, and cover it with dust.

Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali. Mambo ya Walawi 17:14

For as to the life of all flesh, its blood is with its life: therefore I said to the children of Israel, "You shall not eat the blood of any kind of flesh; for the life of all flesh is its blood. Whoever eats it shall be cut off."

Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni; ndipo atakapokuwa safi. Mambo ya Walawi 17:15

"'Every person that eats what dies of itself, or that which is torn by animals, whether he is native-born or a foreigner, he shall wash his clothes, and bathe himself in water, and be unclean until the evening: then he shall be clean.

Lakini kwamba hazifui, wala haogi mwili, ndipo atakapochukua uovu wake. Mambo ya Walawi 17:16

But if he doesn't wash them, or bathe his flesh, then he shall bear his iniquity.'"