Mambo ya Walawi 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 11 (Swahili) Leviticus 11 (English)

Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, Mambo ya Walawi 11:1

Yahweh spoke to Moses and to Aaron, saying to them,

Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi. Mambo ya Walawi 11:2

"Speak to the children of Israel, saying, 'These are the living things which you may eat among all the animals that are on the earth.

Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala. Mambo ya Walawi 11:3

Whatever parts the hoof, and is cloven-footed, and chews the cud among the animals, that you may eat.

Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. Mambo ya Walawi 11:4

"'Nevertheless these you shall not eat of those that chew the cud, or of those who part the hoof: the camel, because he chews the cud but doesn't have a parted hoof, he is unclean to you.

Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. Mambo ya Walawi 11:5

The coney, because he chews the cud but doesn't have a parted hoof, he is unclean to you.

Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. Mambo ya Walawi 11:6

The hare, because she chews the cud but doesn't part the hoof, she is unclean to you.

Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. Mambo ya Walawi 11:7

The pig, because he has a split hoof, and is cloven-footed, but doesn't chew the cud, he is unclean to you.

Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu. Mambo ya Walawi 11:8

Of their flesh you shall not eat, and their carcasses you shall not touch; they are unclean to you.

Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao. Mambo ya Walawi 11:9

These you may eat of all that are in the waters: whatever has fins and scales in the waters, in the seas, and in the rivers, that you may eat.

Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu, Mambo ya Walawi 11:10

All that don't have fins and scales in the seas, and in the rivers, of all that move in the waters, and of all the living creatures that are in the waters, they are an abomination to you,

watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu. Mambo ya Walawi 11:11

and you detest them. You shall not eat of their flesh, and you shall detest their carcasses.

Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu. Mambo ya Walawi 11:12

Whatever has no fins nor scales in the waters, that is an abomination to you.

Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu; Mambo ya Walawi 11:13

"'These you shall detest among the birds; they shall not be eaten, they are an abomination: the eagle, and the vulture, and the black vulture,

na mwewe, na kozi kwa aina zake, Mambo ya Walawi 11:14

and the red kite, any kind of black kite,

na kila kunguru kwa aina zake; Mambo ya Walawi 11:15

any kind of raven,

na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; Mambo ya Walawi 11:16

the horned owl, the screech owl, and the gull, any kind of hawk,

na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa; Mambo ya Walawi 11:17

the little owl, the cormorant, the great owl,

na mumbi, na mwari, na mderi; Mambo ya Walawi 11:18

the white owl, the desert owl, the osprey,

na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo. Mambo ya Walawi 11:19

the stork, any kind of heron, the hoopoe, and the bat.

Tena vyote vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, hivi ni machukizo kwenu. Mambo ya Walawi 11:20

"'All flying insects that walk on all fours are an abomination to you.

Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi; Mambo ya Walawi 11:21

Yet you may eat these: of all winged creeping things that go on all fours, which have legs above their feet, with which to hop on the earth.

katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake. Mambo ya Walawi 11:22

Even of these you may eat: any kind of locust, any kind of katydid, any kind of cricket, and any kind of grasshopper.

Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu. Mambo ya Walawi 11:23

But all winged creeping things which have four feet, are an abomination to you.

Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni; Mambo ya Walawi 11:24

"'By these you will become unclean: whoever touches the carcass of them shall be unclean until the evening.

na mtu awaye yote atakayechukua cho chote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni. Mambo ya Walawi 11:25

Whoever carries any part of their carcass shall wash his clothes, and be unclean until the evening.

Kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, naye hana kwato mbili, wala hacheui, huyo ni najisi kwenu; kila agusaye wanyama hao atakuwa ni najisi. Mambo ya Walawi 11:26

"'Every animal which parts the hoof, and is not cloven-footed, nor chews the cud, is unclean to you. Everyone who touches them shall be unclean.

Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni. Mambo ya Walawi 11:27

Whatever goes on its paws, among all animals that go on all fours, they are unclean to you. Whoever touches their carcass shall be unclean until the evening.

Na huyo atakayechukua mzoga wa wanyama hao atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni; hao ni najisi kwenu Mambo ya Walawi 11:28

He who carries their carcass shall wash his clothes, and be unclean until the evening. They are unclean to you.

Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zake, Mambo ya Walawi 11:29

"'These are they which are unclean to you among the creeping things that creep on the earth: the weasel, the rat, any kind of great lizard,

na guruguru na kenge, na mjusi na goromoe, na lumbwi. Mambo ya Walawi 11:30

the gecko, and the monitor lizard, the wall lizard, the skink, and the chameleon.

Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; awaye yote atakayewagusa, wakiisha kufa, atakuwa ni najisi hata jioni. Mambo ya Walawi 11:31

These are they which are unclean to you among all that creep. Whoever touches them when they are dead, shall be unclean until the evening.

Tena kitu cho chote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; kwamba ni chombo cha mti, au nguo, au ngozi, au gunia, chombo cho chote kitakachoangukiwa, ambacho ni chombo cha kufanyia kazi yo yote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hata jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi. Mambo ya Walawi 11:32

On whatever any of them falls when they are dead, it shall be unclean; whether it is any vessel of wood, or clothing, or skin, or sack, whatever vessel it is, with which any work is done, it must be put into water, and it shall be unclean until the evening; then it will be clean.

Na kila chombo cha udongo, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, kila kilichomo ndani yake kitakuwa ni najisi, na hicho chombo kitavunjwa. Mambo ya Walawi 11:33

Every earthen vessel, into which any of them falls, all that is in it shall be unclean, and you shall break it.

Kila chakula kilichomo, ambacho ni kuliwa, hicho ambacho maji hutumiwa juu yake, kitakuwa ni najisi; na kila kinyweo ambacho ni cha kunywewa, kilichomo katika chombo kama hicho, kitakuwa ni najisi. Mambo ya Walawi 11:34

All food which may be eaten, that on which water comes, shall be unclean; and all drink that may be drunk in every such vessel shall be unclean.

Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande cho chote cha mizoga yao kitakuwa najisi; kwamba ni tanuru, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu. Mambo ya Walawi 11:35

Everything whereupon part of their carcass falls shall be unclean; whether oven, or range for pots, it shall be broken in pieces: they are unclean, and shall be unclean to you.

Pamoja na hayo, chemchemi, au shimo, ambamo maji yakusanyika, vitakuwa ni safi; lakini hicho kitakachogusa mizoga yao kitakuwa ni najisi. Mambo ya Walawi 11:36

Nevertheless a spring or a cistern in which water is a gathered shall be clean: but that which touches their carcass shall be unclean.

Na kipande cho chote cha mzoga kikiwa kimeangukia mbegu za kupandwa zitakazopandwa, zitakuwa safi. Mambo ya Walawi 11:37

If part of their carcass falls on any sowing seed which is to be sown, it is clean.

Lakini kwamba hizo mbegu zilitiwa maji na cho chote cha mizoga yao kuziangukia, ni najisi kwenu. Mambo ya Walawi 11:38

But if water is put on the seed, and part of their carcass falls on it, it is unclean to you.

Kama akifa mnyama awaye yote, ambaye mna ruhusa kumla, yeye anayeugusa mzoga wake atakuwa najisi hata jioni. Mambo ya Walawi 11:39

"'If any animal, of which you may eat, dies; he who touches its carcass shall be unclean until the evening.

Na yeye atakayekula nyama ya mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; yeye atakayeuchukua mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni. Mambo ya Walawi 11:40

He who eats of its carcass shall wash his clothes, and be unclean until the evening. He also who carries its carcass shall wash his clothes, and be unclean until the evening.

Na kila kitu kitambaacho juu ya nchi ni machukizo; hakitaliwa. Mambo ya Walawi 11:41

"'Every creeping thing that creeps on the earth is an abomination. It shall not be eaten.

Kila aendaye kwa tumbo lake, na kila aendaye kwa miguu minne, na kila aendaye kwa miguu mingi, maana, ni vyote vyenye kutambaa vitambaavyo juu ya nchi, hamtavila, kwa kuwa ni machukizo. Mambo ya Walawi 11:42

Whatever goes on its belly, and whatever goes on all fours, or whatever has many feet, even all creeping things that creep on the earth, them you shall not eat; for they are an abomination.

Msifanye nafsi zenu kuwa ni chukizo kwa kitu cho chote chenye kutambaa, kitambaacho, wala msifanye nafsi zenu kuwa ni najisi kwa vitu hivyo, mkajipatia uchafu kwa hivyo. Mambo ya Walawi 11:43

You shall not make yourselves abominable with any creeping thing that creeps, neither shall you make yourselves unclean with them, that you should be defiled thereby.

Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi. Mambo ya Walawi 11:44

For I am Yahweh your God. Sanctify yourselves therefore, and be holy; for I am holy: neither shall you defile yourselves with any kind of creeping thing that moves on the earth.

Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu. Mambo ya Walawi 11:45

For I am Yahweh who brought you up out of the land of Egypt, to be your God. You shall therefore be holy, for I am holy.

Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi; Mambo ya Walawi 11:46

"'This is the law of the animal, and of the bird, and of every living creature that moves in the waters, and of every creature that creeps on the earth,

ili kupambanua kati ya hao walio najisi na hao walio safi, na kati ya kiumbe kilicho hai ambacho chaliwa, na hicho kilicho hai ambacho hakiliwi.

Mambo ya Walawi 11:47

to make a distinction between the unclean and the clean, and between the living thing that may be eaten and the living thing that may not be eaten.'"