Mambo ya Walawi 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 3 (Swahili) Leviticus 3 (English)

Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng'ombe, mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya Bwana. Mambo ya Walawi 3:1

"'If his offering is a sacrifice of peace offerings; if he offers it from the herd, whether male or female, he shall offer it without blemish before Yahweh.

Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. Mambo ya Walawi 3:2

He shall lay his hand on the head of his offering, and kill it at the door of the tent of meeting: and Aaron's sons the priests shall sprinkle the blood on the altar round about.

Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo, Mambo ya Walawi 3:3

He shall offer of the sacrifice of peace offerings an offering made by fire to Yahweh; the fat that covers the innards, and all the fat that is on the innards,

na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno, na hicho kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa. Mambo ya Walawi 3:4

and the two kidneys, and the fat that is on them, which is by the loins, and the cover on the liver, with the kidneys, he shall take away.

Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana. Mambo ya Walawi 3:5

Aaron's sons shall burn it on the altar on the burnt offering, which is on the wood that is on the fire: it is an offering made by fire, of a sweet savor to Yahweh.

Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia Bwana, kwamba ni katika kundi la kondoo; mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu. Mambo ya Walawi 3:6

"'If his offering for a sacrifice of peace offerings to Yahweh is from the flock; male or female, he shall offer it without blemish.

Kama akimtoa mwana-kondoo kuwa matoleo yake, ndipo atakapomtolea Bwana; Mambo ya Walawi 3:7

If he offers a lamb for his offering, then he shall offer it before Yahweh;

naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemsongeza, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. Mambo ya Walawi 3:8

and he shall lay his hand on the head of his offering, and kill it before the tent of meeting: and Aaron's sons shall sprinkle its blood on the altar round about.

Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani dhabihu kwa Bwana, itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yake, na mkia wenye mafuta mzima, atauondoa kwa kuukata hapo karibu na mfupa wa maungoni; na mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo, Mambo ya Walawi 3:9

He shall offer from the sacrifice of peace offerings an offering made by fire to Yahweh; its fat, the entire tail fat, he shall take away close to the backbone; and the fat that covers the inwards, and all the fat that is on the inwards,

na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa. Mambo ya Walawi 3:10

and the two kidneys, and the fat that is on them, which is by the loins, and the cover on the liver, with the kidneys, he shall take away.

Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. Mambo ya Walawi 3:11

The priest shall burn it on the altar: it is the food of the offering made by fire to Yahweh.

Na matoleo yake, kwamba ni mbuzi, ndipo atakapomtoa mbele za Bwana; Mambo ya Walawi 3:12

"'If his offering is a goat, then he shall offer it before Yahweh:

naye ataweka mkono wake kichwani mwake, na kumchinja hapo mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. Mambo ya Walawi 3:13

and he shall lay his hand on its head, and kill it before the tent of meeting; and the sons of Aaron shall sprinkle its blood on the altar round about.

Naye atasongeza katika sadaka hiyo matoleo yake, dhabihu kwa Bwana kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo, Mambo ya Walawi 3:14

He shall offer from it as his offering, an offering made by fire to Yahweh; the fat that covers the innards, and all the fat that is on the innards,

na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini pamoja na hizo figo mbili; hayo yote atayaondoa. Mambo ya Walawi 3:15

and the two kidneys, and the fat that is on them, which is by the loins, and the cover on the liver, with the kidneys, he shall take away.

Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya Bwana. Mambo ya Walawi 3:16

The priest shall burn them on the altar: it is the food of the offering made by fire, for a sweet savor; all the fat is Yahweh's.

Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.

Mambo ya Walawi 3:17

"'It shall be a perpetual statute throughout your generations in all your dwellings, that you shall eat neither fat nor blood.'"