Mambo ya Walawi 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 2 (Swahili) Leviticus 2 (English)

Na mtu atakapomtolea Bwana matoleo ya sadaka ya unga, matoleo yake yatakuwa ya unga mwembamba; naye ataumiminia mafuta, na kutia na ubani juu yake; Mambo ya Walawi 2:1

"'When anyone offers an offering of a meal offering to Yahweh, his offering shall be of fine flour; and he shall pour oil on it, and put frankincense on it.

kisha atauleta kwa wana wa Haruni, hao makuhani; naye atatwaa konzi moja katika huo unga mwembamba, na katika mafuta yake, na huo ubani wote; kisha kuhani atauteketeza kuwa ndio ukumbusho wake juu ya madhabahu, ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana; Mambo ya Walawi 2:2

He shall bring it to Aaron's sons the priests; and he shall take his handful of its fine flour, and of its oil, with all its frankincense; and the priest shall burn the memorial of it on the altar, an offering made by fire, of a sweet savor to Yahweh.

na huo uliosalia wa ile sadaka ya unga utakuwa ni wa Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. Mambo ya Walawi 2:3

That which is left of the meal offering shall be Aaron's and his sons'. It is a most holy thing of the offerings of Yahweh made by fire.

Tena, utakapotoa matoleo ya sadaka ya unga uliookwa tanuuni, yatakuwa mikate isiyotiwa chachu, ya unga mwembamba uliokandwa na mafuta, au maandazi yasiyochachwa yaliyopakwa mafuta. Mambo ya Walawi 2:4

"'When you offer an offering of a meal offering baked in the oven, it shall be unleavened cakes of fine flour mixed with oil, or unleavened wafers anointed with oil.

Tena matoleo yako kwamba ni sadaka ya unga wa kaangoni, yatakuwa ya unga mwembamba usiotiwa chachu, uliokandwa na mafuta. Mambo ya Walawi 2:5

If your offering is a meal offering of the baking pan, it shall be of unleavened fine flour, mixed with oil.

Utaukata-kata vipande, na kutia mafuta juu yake; ni sadaka ya unga. Mambo ya Walawi 2:6

You shall cut it in pieces, and pour oil on it. It is a meal offering.

Tena matoleo yako kwamba ni sadaka ya unga ya chunguni, yataandaliwa kwa unga mwembamba pamoja na mafuta. Mambo ya Walawi 2:7

If your offering is a meal offering of the frying pan, it shall be made of fine flour with oil.

Nawe utamletea Bwana sadaka ya unga iliyofanywa ya vitu hivyo; nayo italetwa kwa kuhani, naye ndiye atakayeisongeza madhabahuni. Mambo ya Walawi 2:8

You shall bring the meal offering that is made of these things to Yahweh: and it shall be presented to the priest, and he shall bring it to the altar.

Kisha kuhani atatwaa humo huo ukumbusho wa sadaka ya unga, naye atauteketeza juu ya madhabahu; ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana. Mambo ya Walawi 2:9

The priest shall take from the meal offering its memorial, and shall burn it on the altar, an offering made by fire, of a sweet savor to Yahweh.

Na hicho kitakachosalia katika sadaka ya unga kitakuwa cha Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. Mambo ya Walawi 2:10

That which is left of the meal offering shall be Aaron's and his sons'. It is a thing most holy of the offerings of Yahweh made by fire.

Sadaka ya unga iwayo yote itakayosongezwa kwa Bwana isitiwe chachu kabisa; kwa kuwa hamtateketeza chachu, wala asali iwayo yote, kuwa ni sadaka ya kusongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. Mambo ya Walawi 2:11

"'No meal offering, which you shall offer to Yahweh, shall be made with yeast; for you shall burn no yeast, nor any honey, as an offering made by fire to Yahweh.

Vitu hivyo mtavisongeza kwa Bwana kuwa ni malimbuko; lakini visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza. Mambo ya Walawi 2:12

As an offering of firstfruits you shall offer them to Yahweh: but they shall not come up for a sweet savor on the altar.

Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote. Mambo ya Walawi 2:13

Every offering of your meal offering you shall season with salt; neither shall you allow the salt of the covenant of your God to be lacking from your meal offering. With all your offerings you shall offer salt.

Nawe kwamba wamtolea Bwana sadaka ya unga ya malimbuko, utatoa hiyo ngano katika masuke yake iliyochomwa motoni, ngano iliyopondwa ya masuke mabichi, ndiyo utakayoleta kuwa sadaka ya unga ya malimbuko yako. Mambo ya Walawi 2:14

"'If you offer a meal offering of first fruits to Yahweh, you shall offer for the meal offering of your first fruits grain in the ear parched with fire, bruised grain of the fresh ear.

Nawe utatia mafuta juu yake, na kuweka ubani juu yake; ni sadaka ya unga. Mambo ya Walawi 2:15

You shall put oil on it, and lay frankincense on it: it is a meal offering.

Huyo kuhani atauteketeza ukumbusho wake, yaani, sehemu ya ngano iliyopondwa ya hiyo sadaka, na sehemu ya mafuta yake, pamoja na ule ubani wake wote; ni kafara ya kusongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto.

Mambo ya Walawi 2:16

The priest shall burn as its memorial, part of its bruised grain, and part of its oil, along with all its frankincense: it is an offering made by fire to Yahweh.