Mambo ya Walawi 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 6 (Swahili) Leviticus 6 (English)

Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 6:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Mtu awaye yote akifanya dhambi, na kuasi juu ya Bwana, akamdanganya mwenziwe katika jambo la amana, au la mapatano, au la kunyang'anya, au kumwonea mwenziwe; Mambo ya Walawi 6:2

"If anyone sins, and commits a trespass against Yahweh, and deals falsely with his neighbor in a matter of deposit, or of bargain, or of robbery, or has oppressed his neighbor,

au kuzumbua kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo; Mambo ya Walawi 6:3

or has found that which was lost, and dealt falsely therein, and swearing to a lie; in any of all these things that a man does, sinning therein;

ndipo itakapokuwa, akiwa amefanya dhambi, na kupata hatia, atarudisha hicho alichokipata kwa kunyang'anya, au kitu kile alichokipata kwa kuonea, au ile amana aliyowekewa, au kitu kile kilichopotea alichokizumbua yeye, Mambo ya Walawi 6:4

then it shall be, if he has sinned, and is guilty, he shall restore that which he took by robbery, or the thing which he has gotten by oppression, or the deposit which was committed to him, or the lost thing which he found,

au kitu cho chote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia. Mambo ya Walawi 6:5

or any thing about which he has sworn falsely; he shall restore it even in full, and shall add a fifth part more to it. To him to whom it belongs he shall give it, in the day of his being found guilty.

Kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa Bwana, ni kondoo mume wa katika kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani; Mambo ya Walawi 6:6

He shall bring his trespass offering to Yahweh, a ram without blemish from the flock, according to your estimation, for a trespass offering, to the priest.

na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana, naye atasamehewa; katika jambo lo lote alifanyalo hata akapata kuwa mwenye hatia kwalo. Mambo ya Walawi 6:7

The priest shall make atonement for him before Yahweh, and he will be forgiven concerning whatever he does to become guilty."

Bwana akanena na Musa na kumwambia, Mambo ya Walawi 6:8

Yahweh spoke to Moses, saying,

Haya, mwagize Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya sadaka ya kuteketezwa ni hii; hiyo sadaka ya kuteketezwa itakuwa pale motoni juu ya madhabahu usiku wote hata asubuhi; na huo moto wa madhabahu utawaka juu yake usizimike. Mambo ya Walawi 6:9

"Command Aaron and his sons, saying, 'This is the law of the burnt offering: the burnt offering shall be on the hearth on the altar all night until the morning; and the fire of the altar shall be kept burning on it.

Naye kuhani atavaa nguo yake ya kitani, na suruali zake za kitani atazivaa mwilini mwake; naye atayazoa majivu ambayo huo moto umeiteketezea sadaka juu ya madhabahu, kisha atayaweka kando ya madhabahu. Mambo ya Walawi 6:10

The priest shall put on his linen garment, and he shall put on his linen breeches upon his body; and he shall remove the ashes from where the fire has consumed the burnt offering on the altar, and he shall put them beside the altar.

Kisha atayavua mavazi yake, na kuvaa mavazi mengine, kisha atayachukua yale majivu kwenda nayo nje ya marago hata mahali safi. Mambo ya Walawi 6:11

He shall take off his garments, and put on other garments, and carry the ashes outside the camp to a clean place.

Na huo moto ulio madhabahuni atautunza uwake daima juu yake, usizimike; naye kuhani atateketeza kuni katika moto huo kila siku asubuhi; naye ataipanga sadaka ya kuteketezwa juu yake, naye atayateketeza mafuta ya sadaka za amani juu yake. Mambo ya Walawi 6:12

The fire on the altar shall be kept burning on it, it shall not go out; and the priest shall burn wood on it every morning: and he shall lay the burnt offering in order upon it, and shall burn on it the fat of the peace offerings.

Moto utatunzwa uwake juu ya madhabahu daima; usizimike. Mambo ya Walawi 6:13

Fire shall be kept burning on the altar continually; it shall not go out.

Na amri ya hiyo sadaka ya unga ni hii; wana wa Haruni wataisongeza mbele za Bwana, mbele ya madhabahu. Mambo ya Walawi 6:14

"'This is the law of the meal offering: the sons of Aaron shall offer it before Yahweh, before the altar.

Naye atatwaa konzi yake katika huo unga, katika huo unga mwembamba wa sadaka ya unga, na katika mafuta yake, na ubani wote ulio juu ya sadaka ya unga, kisha atauteketeza juu ya madhabahu kuwa harufu ya kupendeza, kuwa ukumbusho wake kwa Bwana. Mambo ya Walawi 6:15

He shall take from there his handful of the fine flour of the meal offering, and of its oil, and all the frankincense which is on the meal offering, and shall burn it on the altar for a sweet savor, as its memorial, to Yahweh.

Na unga uliosalia Haruni na wanawe wataula; utaliwa pasipo kutiwa chachu, katika mahali patakatifu; katika ua wa hema ya kukutania ndipo watakapoula. Mambo ya Walawi 6:16

That which is left of it Aaron and his sons shall eat. It shall be eaten without yeast in a holy place. They shall eat it in the court of the Tent of Meeting

Hautaokwa na chachu. Nimewapa kuwa sehemu yao katika matoleo yangu yasongezwayo kwa njia ya moto; ni kitu kitakatifu sana, kama hiyo sadaka ya dhambi, na kama hiyo sadaka ya hatia. Mambo ya Walawi 6:17

It shall not be baked with yeast. I have given it as their portion of my offerings made by fire. It is most holy, as the sin offering, and as the trespass offering.

Kila mwana mume miongoni mwa wana wa Haruni atakula katika huo, kuwa ni haki yao milele katika vizazi vyenu, katika matoleo ya Bwana yasongezwayo kwa njia ya moto; mtu awaye yote atakayevigusa atakuwa ni mtakatifu Mambo ya Walawi 6:18

Every male among the children of Aaron shall eat of it, as their portion forever throughout your generations, from the offerings of Yahweh made by fire. Whoever touches them shall be holy.'"

Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 6:19

Yahweh spoke to Moses, saying,

Matoleo ya Haruni na wanawe watakayomtolea Bwana, katika siku atakayotiwa mafuta, ni haya; sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga daima, nusu yake asubuhi, na nusu yake jioni. Mambo ya Walawi 6:20

"This is the offering of Aaron and of his sons, which they shall offer to Yahweh in the day when he is anointed: the tenth part of an ephah of fine flour for a meal offering perpetually, half of it in the morning, and half of it in the evening.

Utaandaliwa kaangoni pamoja na mafuta; ukisha kulowama utauleta ndani; utasongeza hiyo sadaka ya unga vipande vilivyookwa, iwe harufu ya kupendeza kwa Bwana. Mambo ya Walawi 6:21

It shall be made with oil in a baking pan. When it is soaked, you shall bring it in. You shall offer the meal offering in baked pieces for a sweet savor to Yahweh.

Na huyo kuhani aliyetiwa mafuta badala yake katika hao wanawe ataisongeza; itateketezwa kabisa kwa Bwana kwa amri ya milele. Mambo ya Walawi 6:22

The anointed priest that will be in his place from among his sons shall offer it. By a statute forever, it shall be wholly burnt to Yahweh.

Tena kila sadaka ya unga ya kuhani itateketezwa kabisa; isiliwe. Mambo ya Walawi 6:23

Every meal offering of a priest shall be wholly burned. It shall not be eaten."

Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 6:24

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya hiyo sadaka ya dhambi ni hii; mahali hapo pachinjwapo sadaka ya kuteketezwa ndipo itakapochinjwa sadaka ya dhambi, mbele za Bwana; ni takatifu sana. Mambo ya Walawi 6:25

"Speak to Aaron and to his sons, saying, 'This is the law of the sin offering: in the place where the burnt offering is killed, the sin offering shall be killed before Yahweh. It is most holy.

Huyo kuhani atakayeisongeza kwa ajili ya dhambi ndiye atakayeila; italiwa katika mahali patakatifu, katika ua wa hema ya kukutania. Mambo ya Walawi 6:26

The priest who offers it for sin shall eat it. It shall be eaten in a holy place, in the court of the Tent of Meeting.

Kila kitu kitakachoigusa nyama ya sadaka hiyo kitakuwa kitakatifu; tena itakapomwagika damu yake yo yote katika nguo yo yote, utaifua nguo hiyo iliyomwagiwa, katika mahali patakatifu. Mambo ya Walawi 6:27

Whatever shall touch its flesh shall be holy. When there is any of its blood sprinkled on a garment, you shall wash that on which it was sprinkled in a holy place.

Lakini hicho chombo cha udongo ambacho hiyo nyama ilipikwa ndani yake kitavunjwa; na kama ikipikwa katika chombo cha shaba, kitasuguliwa, na kuoshwa kwa maji. Mambo ya Walawi 6:28

But the earthen vessel in which it is boiled shall be broken; and if it is boiled in a brazen vessel, it shall be scoured, and rinsed in water.

Kila mwana mume miongoni mwa makuhani atakula katika hiyo; ni takatifu sana. Mambo ya Walawi 6:29

Every male among the priests shall eat of it: it is most holy.

Wala haitaliwa sadaka ya dhambi yo yote, ambayo damu yake yo yote ililetwa ndani ya hema ya kukutania, ili kufanya upatanisho katika mahali patakatifu; itachomwa moto.

Mambo ya Walawi 6:30

No sin offering, of which any of the blood is brought into the Tent of Meeting to make atonement in the Holy Place, shall be eaten: it shall be burned with fire.