Mambo ya Walawi 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 1 (Swahili) Leviticus 1 (English)

Bwana akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia, Mambo ya Walawi 1:1

Yahweh called to Moses, and spoke to him out of the Tent of Meeting, saying,

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea Bwana matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng'ombe na katika kondoo. Mambo ya Walawi 1:2

"Speak to the children of Israel, and tell them, 'When anyone of you offers an offering to Yahweh, you shall offer your offering of the cattle, from the herd and from the flock.

Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe mume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya Bwana. Mambo ya Walawi 1:3

"'If his offering is a burnt offering from the herd, he shall offer a male without blemish. He shall offer it at the door of the Tent of Meeting, that he may be accepted before Yahweh.

Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake. Mambo ya Walawi 1:4

He shall lay his hand on the head of the burnt offering, and it shall be accepted for him to make atonement for him.

Naye atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Bwana; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kando-kando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania Mambo ya Walawi 1:5

He shall kill the bull before Yahweh. Aaron's sons, the priests, shall present the blood and sprinkle the blood around on the altar that is at the door of the Tent of Meeting.

Kisha atachuna sadaka ya kuteketeza na kuikata vipande vyake. Mambo ya Walawi 1:6

He shall flay the burnt offering, and cut it into pieces.

Kisha wana wa Haruni, watatia moto juu ya madhabahu, na kuzipanga kuni juu ya moto, Mambo ya Walawi 1:7

The sons of Aaron the priest shall put fire on the altar, and lay wood in order on the fire;

kisha wana wa Haruni, makuhani, watazipanga kuni zilizo juu ya moto uliopo juu ya madhabahu; Mambo ya Walawi 1:8

and Aaron's sons, the priests, shall lay the pieces, the head, and the fat in order on the wood that is on the fire which is on the altar;

lakini matumbo yake, na miguu yake, ataiosha kwa maji; na huyo kuhani ataviteketeza vyote juu ya madhabahu, ili iwe sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana. Mambo ya Walawi 1:9

but its innards and its legs he shall wash with water. The priest shall burn the whole on the altar, for a burnt offering, an offering made by fire, of a sweet savor to Yahweh.

Na matoleo yake kwamba ni katika kundi, katika kondoo, au katika mbuzi, kuwa sadaka ya kuteketezwa; atatoa mume mkamilifu. Mambo ya Walawi 1:10

"'If his offering is from the flock, from the sheep, or from the goats, for a burnt offering, he shall offer a male without blemish.

Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za Bwana; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote. Mambo ya Walawi 1:11

He shall kill it on the north side of the altar before Yahweh. Aaron's sons, the priests, shall sprinkle its blood around on the altar.

Kisha atamkata vipande vyake, pamoja na kichwa chake, na mafuta yake; kisha atavipanga vile vipande juu ya kuni zilizo juu ya madhabahu; Mambo ya Walawi 1:12

He shall cut it into its pieces, with its head and its fat. The priest shall lay them in order on the wood that is on the fire which is on the altar,

lakini matumbo yake, na miguu yake, ataosha kwa maji; na huyo kuhani atavisongeza vyote na kuviteketeza juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana. Mambo ya Walawi 1:13

but the innards and the legs he shall wash with water. The priest shall offer the whole, and burn it on the altar. It is a burnt offering, an offering made by fire, of a sweet savor to Yahweh.

Na matoleo yake atakayomtolea Bwana kuwa sadaka ya kuteketezwa, kwamba ni katika ndege, ndipo atakapoleta matoleo yake katika hua au katika makinda ya njiwa. Mambo ya Walawi 1:14

"'If his offering to Yahweh is a burnt offering of birds, then he shall offer his offering of turtledoves, or of young pigeons.

Kisha kuhani atamleta karibu na madhabahu, naye atamkongonyoa kichwa, na kumteketeza kwa moto juu ya madhabahu; na damu yake itachuruzishwa kando ya madhabahu; Mambo ya Walawi 1:15

The priest shall bring it to the altar, and wring off its head, and burn it on the altar; and its blood shall be drained out on the side of the altar;

kisha atakiondoa kile kibofu chake, pamoja na taka zake, na kukitupa kando ya madhabahu upande wa mashariki, mahali pa majivu; Mambo ya Walawi 1:16

and he shall take away its crop with its filth, and cast it beside the altar on the east part, in the place of the ashes.

kisha atampasua na mabawa yake, lakini asimkate vipande viwili; kisha kuhani atamteketeza juu ya madhabahu, juu ya kuni zilizo juu ya moto; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.

Mambo ya Walawi 1:17

He shall tear it by its wings, but shall not divide it apart. The priest shall burn it on the altar, on the wood that is on the fire. It is a burnt offering, an offering made by fire, of a sweet savor to Yahweh.