Mambo ya Walawi 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 8 (Swahili) Leviticus 8 (English)

Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 8:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Mtwae Haruni, na wanawe pamoja naye, na yale mavazi, na mafuta ya kutia, na ng'ombe mume wa sadaka ya dhambi, na kondoo waume wawili, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu; Mambo ya Walawi 8:2

"Take Aaron and his sons with him, and the garments, and the anointing oil, and the bull of the sin offering, and the two rams, and the basket of unleavened bread;

kisha ukutanishe mkutano wote hapo mlangoni pa hema ya kukutania. Mambo ya Walawi 8:3

and assemble all the congregation at the door of the Tent of Meeting."

Basi Musa akafanya kama alivyoambiwa na Bwana; na huo mkutano ulikutanishwa mlangoni pa hema ya kukutania. Mambo ya Walawi 8:4

Moses did as Yahweh commanded him; and the congregation was assembled at the door of the Tent of Meeting.

Musa akawaambia mkutano, Neno aliloliagiza Bwana kwamba lifanywe, ni hili. Mambo ya Walawi 8:5

Moses said to the congregation, "This is the thing which Yahweh has commanded to be done."

Basi Musa akawaleta Haruni na wanawe, akawaosha kwa maji. Mambo ya Walawi 8:6

Moses brought Aaron and his sons, and washed them with water.

Kisha akamvika Haruni ile kanzu, na kumfunga mshipi, na kumvika joho, na kumvika naivera, na kumfunga huo mshipi wa kazi ya mstadi wa naivera na kumfunga naivera kwa huo mshipi. Mambo ya Walawi 8:7

He put the coat on him, tied the sash on him, clothed him with the robe, put the ephod on him, and he tied the skillfully woven band of the ephod on him, and fastened it to him with it.

Kisha akamtia kile kifuko cha kifuani; akatia hizo Urimu na Thumimu katika hicho kifuko cha kifuani. Mambo ya Walawi 8:8

He placed the breastplate on him; and in the breastplate he put the Urim and the Thummim.

Akamvika na kile kilemba kichwani mwake; na juu ya kilemba, upande wa mbele, akakitia kile kipande cha dhahabu, hiyo taji takatifu; kama Bwana alivyomwagiza Musa. Mambo ya Walawi 8:9

He set the turban on his head; and on the turban, in front, he set the golden plate, the holy crown; as Yahweh commanded Moses.

Kisha Musa akatwaa hayo mafuta matakatifu ya kutia, akatia mafuta maskani, na vyote vilivyokuwamo, na kuvitakasa. Mambo ya Walawi 8:10

Moses took the anointing oil, and anointed the tabernacle and all that was in it, and sanctified them.

Kisha akanyunyiza hayo mafuta juu ya madhabahu mara saba, na kuitia mafuta madhabahu na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake, ili kuvitakasa. Mambo ya Walawi 8:11

He sprinkled it on the altar seven times, and anointed the altar and all its vessels, and the basin and its base, to sanctify them.

Kisha akamimina mafuta hayo ya kutia kichwani mwake Haruni, na kumtia mafuta, ili amtakase. Mambo ya Walawi 8:12

He poured some of the anointing oil on Aaron's head, and anointed him, to sanctify him.

Kisha Musa akawaleta wana wa Haruni, na kuwavika kanzu, na kuwafunga mishipi, na kuwavika vilemba; kama Bwana alivyomwagiza Musa. Mambo ya Walawi 8:13

Moses brought Aaron's sons, and clothed them with coats, and tied sashes on them, and put headbands on them; as Yahweh commanded Moses.

Kisha akamleta yule ng'ombe mume wa sadaka ya dhambi; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao katika kichwa cha huyo ng'ombe wa sadaka ya dhambi. Mambo ya Walawi 8:14

He brought the bull of the sin offering, and Aaron and his sons laid their hands on the head of the bull of the sin offering.

Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake. Mambo ya Walawi 8:15

He killed it; and Moses took the blood, and put it on the horns of the altar round about with his finger, and purified the altar, and poured out the blood at the base of the altar, and sanctified it, to make atonement for it.

Kisha akayatwaa mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo yake, na kitambi kilichokuwa katika ini, na figo zake mbili, na mafuta yake, na Musa akayateketeza juu ya madhabahu. Mambo ya Walawi 8:16

He took all the fat that was on the innards, and the cover of the liver, and the two kidneys, and their fat; and Moses burned it on the altar.

Lakini huyo ng'ombe mwenyewe, na ngozi yake, na nyama yake, na mavi yake, akayachoma moto nje ya marago; vile vile kama Bwana alivyomwagiza Musa. Mambo ya Walawi 8:17

But the bull, and its skin, and its flesh, and its dung, he burned with fire outside the camp; as Yahweh commanded Moses.

Kisha akamsongeza yule kondoo mume wa sadaka ya kuteketezwa; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao kichwani mwa huyo kondoo. Mambo ya Walawi 8:18

He presented the ram of the burnt offering: and Aaron and his sons laid their hands on the head of the ram.

Kisha akamchinja; na Musa akainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. Mambo ya Walawi 8:19

He killed it; and Moses sprinkled the blood on the altar round about.

Kisha akamkata kondoo vipande vyake; na Musa akateketeza kichwa, na vile vipande, na mafuta. Mambo ya Walawi 8:20

He cut the ram into its pieces; and Moses burned the head, and the pieces, and the fat.

Kisha akayaosha matumbo na miguu yake kwa maji; na Musa akamteketeza huyo kondoo wote juu ya madhabahu; ilikuwa ni sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza; ilikuwa ni sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto; kama Bwana alivyomwagiza Musa. Mambo ya Walawi 8:21

He washed the innards and the legs with water; and Moses burned the whole ram on the altar. It was a burnt offering for a sweet savor. It was an offering made by fire to Yahweh; as Yahweh commanded Moses.

Kisha akamsongeza kondoo mume wa pili, huyo kondoo wa kuwaweka wakfu; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao kichwani mwa huyo kondoo. Mambo ya Walawi 8:22

He presented the other ram, the ram of consecration: and Aaron and his sons laid their hands on the head of the ram.

Kisha akamchinja; na Musa akatwaa katika damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la kuume la Haruni, na katika chanda chake cha gumba cha mkono wake wa kuume, na katika kidole cha gumba cha guu lake la kuume. Mambo ya Walawi 8:23

He killed it; and Moses took some of its blood, and put it on the tip of Aaron's right ear, and on the thumb of his right hand, and on the great toe of his right foot.

Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya kuume, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vya gumba vya maguu yao ya kuume; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote. Mambo ya Walawi 8:24

He brought Aaron's sons; and Moses put some of the blood on the tip of their right ear, and on the thumb of their right hand, and on the great toe of their right foot; and Moses sprinkled the blood on the altar round about.

Kisha akayatwaa hayo mafuta, na mkia wenye mafuta, na mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo, na kitambi cha ini, na figo mbili, na mafuta yake, na mguu wa nyuma wa upande wa kuume; Mambo ya Walawi 8:25

He took the fat, and the fat tail, and all the fat that was on the innards, and the cover of the liver, and the two kidneys, and their fat, and the right thigh;

kisha katika kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, kilichokuwa pale mbele za Bwana, akatwaa mkate mmoja usiochachwa, na mkate mmoja ulioandaliwa na mafuta na kaki moja nyembamba, akaiweka juu ya mafuta, na juu ya huo mguu wa nyuma wa upande wa kuume; Mambo ya Walawi 8:26

and out of the basket of unleavened bread, that was before Yahweh, he took one unleavened cake, and one cake of oiled bread, and one wafer, and placed them on the fat, and on the right thigh.

kisha akaweka vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe, na kuvitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana. Mambo ya Walawi 8:27

He put all these in Aaron's hands and in his sons' hands, and waved them for a wave offering before Yahweh.

Kisha Musa akavitwaa tena mikononi mwao, na kuviteketeza juu ya madhabahu, juu ya hiyo sadaka ya kuteketezwa vilikuwa vya kuwaweka wakfu, ni harufu nzuri; ilikuwa dhabihu iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto. Mambo ya Walawi 8:28

Moses took them from their hands, and burned them on the altar on the burnt offering. They were a consecration for a sweet savor. It was an offering made by fire to Yahweh.

Kisha Musa akakitwaa kile kidari, akakitikisa huku na huku, kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana; ni sehemu ya Musa katika huyo kondoo mume wa kuwaweka wakfu; kama Bwana alivyomwagiza Musa. Mambo ya Walawi 8:29

Moses took the breast, and waved it for a wave offering before Yahweh. It was Moses' portion of the ram of consecration, as Yahweh commanded Moses.

Kisha Musa akatwaa baadhi ya mafuta ya kutia, na ya damu iliyokuwa pale juu ya madhabahu, na kumnyunyizia Haruni, katika mavazi yake, na wanawe, katika mavazi yao, pamoja naye; akamtakasa Haruni, na mavazi yake, na wanawe, na mavazi ya wanawe, pamoja naye. Mambo ya Walawi 8:30

Moses took some of the anointing oil, and some of the blood which was on the altar, and sprinkled it on Aaron, on his garments, and on his sons, and on his sons' garments with him, and sanctified Aaron, his garments, and his sons, and his sons' garments with him.

Kisha Musa akawaambia huyo Haruni na wanawe, Tokoseni hiyo nyama mlangoni pa hema ya kukutania; mkaile pale pale, na hiyo mikate iliyo katika kile kikapu cha kuwaweka wakfu, kama nilivyoagizwa kusema, Haruni na wanawe wataila. Mambo ya Walawi 8:31

Moses said to Aaron and to his sons, "Boil the flesh at the door of the Tent of Meeting, and there eat it and the bread that is in the basket of consecration, as I commanded, saying, 'Aaron and his sons shall eat it.'

Nacho kitakachosalia katika hiyo nyama na mikate mtakichoma moto. Mambo ya Walawi 8:32

What remains of the flesh and of the bread you shall burn with fire.

Wala msitoke nje mlangoni pa hema ya kukutania muda wa siku saba, hata siku za kuwekwa wakfu kwenu zitakapotimia; kwa kuwa atawaweka muda wa siku saba. Mambo ya Walawi 8:33

You shall not go out from the door of the Tent of Meeting seven days, until the days of your consecration are fulfilled: for he shall consecrate you seven days.

Vile vile kama vilivyotendeka siku ya leo, ni vivyo Bwana alivyoagiza kufanywa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Mambo ya Walawi 8:34

What has been done this day, so Yahweh has commanded to do, to make atonement for you.

Nanyi mtakaa mlangoni pa hema ya kukutania muda wa siku saba mchana na usiku, na kuulinda ulinzi wa Bwana ili kwamba msife; kwani ndivyo nilivyoagizwa. Mambo ya Walawi 8:35

At the door of the Tent of Meeting you shall stay day and night seven days, and keep the charge of Yahweh, that you don't die: for so I am commanded."

Basi Haruni na wanawe wakafanya mambo hayo yote Bwana aliyoyaagiza kwa mkono wa Musa.

Mambo ya Walawi 8:36

Aaron and his sons did all the things which Yahweh commanded by Moses.