Ezekieli 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezekieli 3 (Swahili) Ezekiel 3 (English)

Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli. Ezekieli 3:1

He said to me, Son of man, eat that which you find; eat this scroll, and go, speak to the house of Israel.

Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. Ezekieli 3:2

So I opened my mouth, and he caused me to eat the scroll.

Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali. Ezekieli 3:3

He said to me, Son of man, cause your belly to eat, and fill your bowels with this scroll that I give you. Then did I eat it; and it was in my mouth as honey for sweetness.

Akaniambia, Mwanadamu, haya! Waendee wana wa Israeli ukawaambie maneno yangu. Ezekieli 3:4

He said to me, Son of man, go, get you to the house of Israel, and speak with my words to them.

Maana wewe hukutumwa kwa watu wa maneno mageni, ama wa lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli; Ezekieli 3:5

For you are not sent to a people of a strange speech and of a hard language, but to the house of Israel;

si kwa watu wa kabila nyingi wenye maneno mageni, na lugha ngumu, ambao huwezi kufahamu maneno yao. Bila shaka, kama ningekutuma kwa watu hao, wangekusikiliza. Ezekieli 3:6

not to many peoples of a strange speech and of a hard language, whose words you can not understand. Surely, if I sent you to them, they would listen to you.

Bali nyumba ya Israeli hawatakusikiliza wewe; kwa kuwa hawanisikilizi mimi; maana nyumba yote ya Israeli wana vipaji vigumu, na mioyo yenye ukaidi. Ezekieli 3:7

But the house of Israel will not listen to you; for they will not listen to me: for all the house of Israel are of hard forehead and of a stiff heart.

Tazama, nimeufanya uso wako kuwa mgumu juu ya nyuso zao, na kipaji cha uso chako kuwa kigumu juu ya vipaji vya nyuso vyao. Ezekieli 3:8

Behold, I have made your face hard against their faces, and your forehead hard against their foreheads.

Kama almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji chako; usiwaogope, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi. Ezekieli 3:9

As an adamant harder than flint have I made your forehead: don't be afraid of them, neither be dismayed at their looks, though they are a rebellious house.

Tena akaniambia, Mwanadamu, maneno yangu yote nitakayokuambia, yapokee moyoni mwako, na kuyasikia kwa masikio yako. Ezekieli 3:10

Moreover he said to me, Son of man, all my words that I shall speak to you receive in your heart, and hear with your ears.

Haya! Enenda uwafikilie watu hao waliohamishwa, kwa wana wa watu wako, ukaseme nao, na kuwaambia, Bwana MUNGU asema hivi; kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia. Ezekieli 3:11

Go, get you to them of the captivity, to the children of your people, and speak to them, and tell them, Thus says the Lord Yahweh; whether they will hear, or whether they will forbear.

Ndipo roho ikaniinua, nami nikasikia nyuma yangu sauti kama mshindo wa radi kuu, ikisema, Na uhimidiwe utukufu wa Bwana tokea mahali pake. Ezekieli 3:12

Then the Spirit lifted me up, and I heard behind me the voice of a great rushing, [saying], Blessed be the glory of Yahweh from his place.

Nikasikia mshindo wa mabawa ya vile viumbe hai, walipogusana, na mshindo wa yale magurudumu kando yao, mshindo wa radi kuu. Ezekieli 3:13

[I heard] the noise of the wings of the living creatures as they touched one another, and the noise of the wheels beside them, even the noise of a great rushing.

Basi roho ikaniinua, ikanichukua mahali pengine; nami nikaenda kwa uchungu, na hasira kali rohoni mwangu, na mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu kwa nguvu. Ezekieli 3:14

So the Spirit lifted me up, and took me away; and I went in bitterness, in the heat of my spirit; and the hand of Yahweh was strong on me.

Ndipo nikawafikia watu waliohamishwa, huko Tel-abibu, waliokuwa wakikaa karibu na mto Kebari, nikafika huko walikokuwa wakikaa; nikaketi huko miongoni mwao muda wa siku saba, katika hali ya ushangao mwingi. Ezekieli 3:15

Then I came to them of the captivity at Tel Aviv, that lived by the river Chebar, and to where they lived; and I sat there overwhelmed among them seven days.

Hata ikawa, mwisho wa siku saba, neno la Bwana likanijia, kusema, Ezekieli 3:16

It happened at the end of seven days, that the word of Yahweh came to me, saying,

Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu. Ezekieli 3:17

Son of man, I have made you a watchman to the house of Israel: therefore hear the word at my mouth, and give them warning from me.

Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Ezekieli 3:18

When I tell the wicked, You shall surely die; and you give him no warning, nor speak to warn the wicked from his wicked way, to save his life; the same wicked man shall die in his iniquity; but his blood will I require at your hand.

Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako. Ezekieli 3:19

Yet if you warn the wicked, and he doesn't turn from his wickedness, nor from his wicked way, he shall die in his iniquity; but you have delivered your soul.

Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Ezekieli 3:20

Again, when a righteous man does turn from his righteousness, and commit iniquity, and I lay a stumbling block before him, he shall die: because you have not given him warning, he shall die in his sin, and his righteous deeds which he has done shall not be remembered; but his blood will I require at your hand.

Bali ukimwonya mwenye haki, kwamba yule mwenye haki asitende dhambi, tena ikiwa yeye hatendi dhambi, hakika ataishi, kwa sababu alikubali kuonywa; nawe umejiokoa roho yako. Ezekieli 3:21

Nevertheless if you warn the righteous man, that the righteous not sin, and he does not sin, he shall surely live, because he took warning; and you have delivered your soul.

Na mkono wa Bwana ulikuwako juu yangu huko; akaniambia, Ondoka, enenda uwandani; nami nitasema nawe huko. Ezekieli 3:22

The hand of Yahweh was there on me; and he said to me, Arise, go forth into the plain, and I will there talk with you.

Basi, nikaondoka, nikaenda uwandani, na tazama, utukufu wa Bwana ulisimama huko, kama utukufu ule niliouona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi. Ezekieli 3:23

Then I arose, and went forth into the plain: and, behold, the glory of Yahweh stood there, as the glory which I saw by the river Chebar; and I fell on my face.

Ndipo roho ile ikaniingia, ikanisimamisha kwa miguu yangu; akasema nami, akaniambia, Enenda ukajifungie nyumbani mwako. Ezekieli 3:24

Then the Spirit entered into me, and set me on my feet; and he spoke with me, and said to me, Go, shut yourself within your house.

Lakini wewe, mwanadamu, tazama, watakutia pingu, nao watakufunga kwazo, wala hutakwenda nje kati yao; Ezekieli 3:25

But you, son of man, behold, they shall lay bands on you, and shall bind you with them, and you shall not go out among them:

nami nitaufanya ulimi wako ugandamane na kaakaa lako, hata utakuwa bubu, wala hutakuwa mwonyaji kwao; kwa kuwa wao ni nyumba yenye kuasi. Ezekieli 3:26

and I will make your tongue cleave to the roof of your mouth, that you shall be mute, and shall not be to them a reprover; for they are a rebellious house.

Lakini hapo nitakaposema nawe, nitafumbua kinywa chako, nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi. Yeye asikiaye na asikie; naye akataaye na akatae; maana wao ni nyumba yenye kuasi. Ezekieli 3:27

But when I speak with you, I will open your mouth, and you shall tell them, Thus says the Lord Yahweh: He who hears, let him hear; and he who forbears, let him forbear: for they are a rebellious house.