Ezekieli 24 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezekieli 24 (Swahili) Ezekiel 24 (English)

Tena, katika mwaka wa kenda, mwezi wa kumi, siku ya kumi ya mwezi, neno la Bwana likanijia, kusema, Ezekieli 24:1

Again, in the ninth year, in the tenth month, in the tenth [day] of the month, the word of Yahweh came to me, saying,

Mwanadamu, liandike jina la siku hii, naam, la siku ii hii; mfalme wa Babeli ameukaribia Yerusalemu siku iyo hiyo. Ezekieli 24:2

Son of man, write you the name of the day, [even] of this same day: the king of Babylon drew close to Jerusalem this same day.

Ukawatungie mithali nyumba ya kuasi, ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Teleka sufuria, liteleke; ukatie maji ndani yake; Ezekieli 24:3

Utter a parable to the rebellious house, and tell them, Thus says the Lord Yahweh, Set on the caldron, set it on, and also pour water into it:

vikusanye vipande vyake ndani yake, naam, kila kipande chema, paja na bega; lijaze mifupa iliyochaguliwa. Ezekieli 24:4

gather the pieces of it into it, even every good piece, the thigh, and the shoulder; fill it with the choice bones.

Uwatwae wateule wa kundi la kondoo, ukafanye chungu ya mifupa chini yake; ukalitokose sana; naam, mifupa yake itokoswe ndani yake. Ezekieli 24:5

Take the choice of the flock, and also a pile [of wood] for the bones under [the caldron]; make it boil well; yes, let the bones of it be boiled in the midst of it.

Basi Bwana MUNGU asema hivi; Ole wake mji wa damu! Hilo sufuria ambalo kutu yake i ndani yake, ambalo kutu yake haikulitoka; litoe kipande kipande; hapana kura iliyoanguka juu yake. Ezekieli 24:6

Therefore thus says the Lord Yahweh: Woe to the bloody city, to the caldron whose rust is therein, and whose rust is not gone out of it! take out of it piece after piece; No lot is fallen on it.

Maana damu yake imo ndani yake; aliiweka juu ya jabali lililo wazi; hakuimwaga juu ya nchi, apate kuifunika kwa mavumbi; Ezekieli 24:7

For her blood is in the midst of her; she set it on the bare rock; she didn't pour it on the ground, to cover it with dust.

ili ipandishe ghadhabu ya kulipa kisasi, nimeiweka damu yake juu ya jabali lililo wazi, isipate kufunikwa. Ezekieli 24:8

That it may cause wrath to come up to take vengeance, I have set her blood on the bare rock, that it should not be covered.

Basi Bwana MUNGU asema hivi; Ole wake mji wa damu! Mimi nami nitaiongeza chungu. Ezekieli 24:9

Therefore thus says the Lord Yahweh: Woe to the bloody city! I also will make the pile great.

Tia kuni nyingi, uchochee moto, itokose nyama sana, fanyiza mchuzi mzito, mifupa ikateketee. Ezekieli 24:10

Heap on the wood, make the fire hot, boil well the flesh, and make thick the broth, and let the bones be burned.

Kisha litie juu ya makaa yake, tupu, lipate moto, na shaba yake iteketee, uchafu wake uyeyushwe, na kutu yake iteketee. Ezekieli 24:11

Then set it empty on the coals of it, that it may be hot, and the brass of it may burn, and that the filthiness of it may be molten in it, that the rust of it may be consumed.

Amejidhoofisha kwa taabu, lakini kutu yake nyingi haikumtoka; kutu yake haitoki kwa moto. Ezekieli 24:12

She has wearied [herself] with toil; yet her great rust doesn't go forth out of her; her rust doesn't [go forth] by fire.

Katika uchafu wako mna uasherati, kwa maana nimekusafisha, ila wewe hukusafika; hutasafishwa tena uchafu wako ukutoke, hata nitakapokuwa nimeituliza hasira yangu kwako. Ezekieli 24:13

In your filthiness is lewdness: because I have cleansed you and you weren't cleansed, you shall not be cleansed from your filthiness any more, until I have caused my wrath toward you to rest.

Mimi, Bwana, nimenena neno hili, nalo litakuwa; nami nitalifanya; sitaachilia, wala sitahurumia, wala sitajuta; sawasawa na njia zako, na sawasawa na matendo yako, ndivyo watakavyokuhukumu, asema Bwana MUNGU. Ezekieli 24:14

I, Yahweh, have spoken it: it shall happen, and I will do it: I will not go back, neither will I spare, neither will I repent; according to your ways, and according to your doings, shall they judge you, says the Lord Yahweh.

Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Ezekieli 24:15

Also the word of Yahweh came to me, saying,

Mwanadamu, tazama, ninakuondolea kwa pigo moja tunu, mteule wa macho yako; walakini hutaomboleza wala kulia, wala yasichuruzike machozi yako. Ezekieli 24:16

Son of man, behold, I take away from you the desire of your eyes with a stroke: yet you shall neither mourn nor weep, neither shall your tears run down.

Ugua lakini si kwa sauti ya kusikiwa; usifanye matanga kwa ajili yake yeye aliyekufa; jipige kilemba chako, ukavae viatu vyako, wala usiifunike midomo yako, wala usile chakula cha watu. Ezekieli 24:17

Sigh, but not aloud, make no mourning for the dead; bind your headdress on you, and put your shoes on your feet, and don't cover your lips, and don't eat men's bread.

Basi nalisema na watu asubuhi, na jioni mke wangu akafa; nami nalifanya asubuhi kama nilivyoagizwa. Ezekieli 24:18

So I spoke to the people in the morning; and at even my wife died; and I did in the morning as I was commanded.

Watu hao wakaniambia, Je! Hutaki kutuambia maana ya mambo haya kwetu, hata umefanya kama vile ufanyavyo. Ezekieli 24:19

The people said to me, Won't you tell us what these things are to us, that you do so?

Nikawaambia, Neno la Bwana lilinijia, kusema, Ezekieli 24:20

Then I said to them, The word of Yahweh came to me, saying,

Uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahali pa kutamaniwa na macho yenu, ambapo roho zenu zinapahurumia na wana wenu na binti zenu, mliowaacha nyuma, wataanguka kwa upanga. Ezekieli 24:21

Speak to the house of Israel, Thus says the Lord Yahweh: Behold, I will profane my sanctuary, the pride of your power, the desire of your eyes, and that which your soul pities; and your sons and your daughters whom you have left behind shall fall by the sword.

Nanyi mtafanya kama mimi nilivyofanya; hamtaifunika midomo yenu, wala kula chakula cha watu. Ezekieli 24:22

You shall do as I have done: you shall not cover your lips, nor eat the bread of men.

Na vilemba vyenu vitakuwa juu ya vichwa vyenu, na viatu vyenu miguuni mwenu; hamtaomboleza wala kulia; lakini mtafifia katika maovu yenu, na kuugua kila mtu pamoja na mwenziwe. Ezekieli 24:23

Your tires shall be on your heads, and your shoes on your feet: you shall not mourn nor weep; but you shall pine away in your iniquities, and moan one toward another.

Basi ndivyo Ezekielii atakavyokuwa ishara kwenu; ninyi mtatenda sawasawa na yote aliyoyatenda yeye; litakapokuja jambo hili, ndipo mtakapojua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU. Ezekieli 24:24

Thus shall Ezekiel be to you a sign; according to all that he has done shall you do: when this comes, then shall you know that I am the Lord Yahweh.

Nawe, mwanadamu, je! Haitakuwa hivi katika siku hiyo nitakapowaondolea nguvu zao, na furaha ya utukufu wao, na kilichotamaniwa na macho yao, ambacho walikiinulia mioyo yao, wana wao na binti zao, Ezekieli 24:25

You, son of man, shall it not be in the day when I take from them their strength, the joy of their glory, the desire of their eyes, and that whereupon they set their heart, their sons and their daughters,

kwamba katika siku iyo hiyo yeye atakayeokoka atakuja kwako, akusikize jambo hili kwa masikio yako? Ezekieli 24:26

that in that day he who escapes shall come to you, to cause you to hear it with your ears?

Siku hiyo kinywa chako kitafumbuliwa kwake aliyeokoka, nawe utasema; hutakuwa bubu tena; ndivyo utakavyokuwa ishara kwao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Ezekieli 24:27

In that day shall your mouth be opened to him who is escaped, and you shall speak, and be no more mute: so shall you be a sign to them; and they shall know that I am Yahweh.