Ezekieli 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezekieli 12 (Swahili) Ezekiel 12 (English)

Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Ezekieli 12:1

The word of Yahweh also came to me, saying,

Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi. Ezekieli 12:2

Son of man, you dwell in the midst of the rebellious house, who have eyes to see, and don't see, who have ears to hear, and don't hear; for they are a rebellious house.

Basi, mwanadamu, funga tayari vyombo kwa uhamisho, ukahame wakati wa mchana mbele ya macho yao; nawe utahama toka mahali pako hapa mpaka mahali pengine mbele ya macho yao; labda watafahamu, wajapokuwa ni nyumba iliyoasi. Ezekieli 12:3

Therefore, you son of man, prepare you stuff for removing, and remove by day in their sight; and you shall remove from your place to another place in their sight: it may be they will consider, though they are a rebellious house.

Nawe utatoa vyombo vyako, wakati wa mchana, mbele ya macho yao, kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa; nawe mwenyewe utatoka, wakati wa jioni, mbele ya macho yao, kama watu watokavyo katika kuhamishwa. Ezekieli 12:4

You shall bring forth your stuff by day in their sight, as stuff for removing; and you shall go forth yourself at even in their sight, as when men go forth into exile.

Toboa mahali ukutani mbele ya macho yao, ukachukue vitu kwa kuvipitisha pale. Ezekieli 12:5

Dig you through the wall in their sight, and carry out thereby.

Mbele ya macho yao utajitwika begani pako, na kuvichukua nje gizani; utafunika uso wako, hata usiione nchi; kwa maana nimekuweka uwe ishara kwa nyumba ya Israeli. Ezekieli 12:6

In their sight shall you bear it on your shoulder, and carry it forth in the dark; you shall cover your face, that you don't see the land: for I have set you for a sign to the house of Israel.

Nikafanya vile vile kama nilivyoamriwa; nalitoa vyombo vyangu wakati wa mchana kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa, na wakati wa jioni nikautoboa ukuta kwa mkono wangu; nikavitoa gizani, nikavichukua begani, mbele ya macho yao. Ezekieli 12:7

I did so as I was commanded: I brought forth my stuff by day, as stuff for removing, and in the even I dug through the wall with my hand; I brought it forth in the dark, and bore it on my shoulder in their sight.

Asubuhi neno la Bwana likanijia, kusema, Ezekieli 12:8

In the morning came the word of Yahweh to me, saying,

Mwanadamu, nyumba ya Israeli, je! Nyumba ile iliyoasi, hawakukuambia, Unafanya nini wewe? Ezekieli 12:9

Son of man, has not the house of Israel, the rebellious house, said to you, What do you?

Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Ufunuo huu wamhusu mkuu wa Yerusalemu, na nyumba yote ya Israeli walio kati yao. Ezekieli 12:10

Say you to them, Thus says the Lord Yahweh: This burden [concerns] the prince in Jerusalem, and all the house of Israel among whom they are.

Sema, Mimi ni ishara kwenu; kama mimi nilivyotenda, wao nao watatendwa vile vile; watahamishwa, watakwenda kufungwa. Ezekieli 12:11

Say, I am your sign: like as I have done, so shall it be done to them; they shall go into exile, into captivity.

Naye mkuu aliye kati yao atachukua begani katika giza; naye atatoka kwenda zake; watatoboa mahali ukutani, wapate kuvichukua vyombo vyao nje; atafunika uso wake, kwa sababu hataiona nchi kwa macho yake. Ezekieli 12:12

The prince who is among them shall bear on his shoulder in the dark, and shall go forth: they shall dig through the wall to carry out thereby: he shall cover his face, because he shall not see the land with his eyes.

Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; lakini hataiona, angawa atakufa huko. Ezekieli 12:13

My net also will I spread on him, and he shall be taken in my snare; and I will bring him to Babylon to the land of the Chaldeans; yet shall he not see it, though he shall die there.

Nami nitawatawanya kwa pepo zote wote wamzungukao ili wamsaidie, na vikosi vyake vyote; nami nitaufuta upanga nyuma yao. Ezekieli 12:14

I will scatter toward every wind all who are round about him to help him, and all his bands; and I will draw out the sword after them.

Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; nitakapowatawanya kati ya mataifa, na kuwatupa-tupa katika nchi zote. Ezekieli 12:15

They shall know that I am Yahweh, when I shall disperse them among the nations, and scatter them through the countries.

Lakini nitawasaza watu wachache miongoni mwao na kuwaokoa na upanga, na njaa, na tauni ili watangaze habari ya machukizo yao yote, kati ya mataifa huko waendako; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Ezekieli 12:16

But I will leave a few men of them from the sword, from the famine, and from the pestilence; that they may declare all their abominations among the nations where they come; and they shall know that I am Yahweh.

Tena neno la Bwana likanijia, kusema, Ezekieli 12:17

Moreover the word of Yahweh came to me, saying,

Mwanadamu, ule chakula chako kwa matetemo, ukanywe maji yako kwa kutetemeka na kwa kuyatunza sana; Ezekieli 12:18

Son of man, eat your bread with quaking, and drink your water with trembling and with fearfulness;

ukawaambie watu wa nchi, Bwana MUNGU asema hivi, katika habari zao wakaao Yerusalemu, na katika nchi ya Israeli; Watakula chakula chao kwa kukitunza sana, na maji yao watayanywa kwa ushangao, nchi yao iwe ukiwa, kwa kukosa vitu vyote viijazavyo, kwa sababu ya udhalimu wao wote wakaao ndani yake. Ezekieli 12:19

and tell the people of the land, Thus says the Lord Yahweh concerning the inhabitants of Jerusalem, and the land of Israel: They shall eat their bread with fearfulness, and drink their water in dismay, that her land may be desolate, [and despoiled] of all that is therein, because of the violence of all those who dwell therein.

Na miji yote yenye watu itakuwa maganjo, nayo nchi itakuwa ukiwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Ezekieli 12:20

The cities that are inhabited shall be laid waste, and the land shall be a desolation; and you shall know that I am Yahweh.

Neno la Bwana likanijia, kusema, Ezekieli 12:21

The word of Yahweh came to me, saying,

Mwanadamu, ni mithali gani hii mliyo nayo katika nchi ya Israeli, mkisema, Siku hizo zinakawia na maono yote hayatimizwi. Ezekieli 12:22

Son of man, what is this proverb that you have in the land of Israel, saying, The days are prolonged, and every vision fails?

Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Nitaikomesha mithali hii, wasiitumie tena kama mithali katika Israeli; lakini uwaambie, Siku hizo ni karibu, na utimilizo wa maono yote. Ezekieli 12:23

Tell them therefore, Thus says the Lord Yahweh: I will make this proverb to cease, and they shall no more use it as a proverb in Israel; but tell them, The days are at hand, and the fulfillment of every vision.

Kwa maana hayatakuwapo tena maono yo yote ya ubatili, wala ubashiri wa kujipendekeza, katika nyumba ya Israeli. Ezekieli 12:24

For there shall be no more any false vision nor flattering divination within the house of Israel.

Maana mimi ni Bwana; mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala halitakawilishwa tena; maana katika siku zenu, Ewe nyumba iliyoasi, nitalinena neno hilo na kulitimiza, asema Bwana MUNGU. Ezekieli 12:25

For I am Yahweh; I will speak, and the word that I shall speak shall be performed; it shall be no more deferred: for in your days, rebellious house, will I speak the word, and will perform it, says the Lord Yahweh.

Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Ezekieli 12:26

Again the word of Yahweh came to me, saying,

Mwanadamu, tazama, hao wa nyumba ya Israeli husema, Maono hayo ayaonayo ni ya siku nyingi zijazo, naye anatabiri habari ya nyakati zilizo mbali sana. Ezekieli 12:27

Son of man, behold, they of the house of Israel say, The vision that he sees is for many day to come, and he prophesies of times that are far off.

Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Maneno yangu hayatakawilishwa tena hata moja, bali neno nitakalolinena litatimizwa, asema Bwana MUNGU. Ezekieli 12:28

Therefore tell them, Thus says the Lord Yahweh: There shall none of my words be deferred any more, but the word which I shall speak shall be performed, says the Lord Yahweh.