Ezekieli 26 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezekieli 26 (Swahili) Ezekiel 26 (English)

Ikawa katika mwaka wa kumi na mmoja, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana likanijia, kusema, Ezekieli 26:1

It happened in the eleventh year, in the first [day] of the month, that the word of Yahweh came to me, saying,

Mwanadamu, Kwa sababu Tiro amesema juu ya Yerusalemu, Aha! Yeye amevunjika aliyekuwa lango la kabila za watu; amenigeukia; nitajazwa kwa kuwa sasa ameharibika; Ezekieli 26:2

Son of man, because Tyre has said against Jerusalem, Aha, she is broken: the gate of the peoples; she is turned to me; I shall be replenished, now that she is laid waste:

basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee Tiro, nami nitaleta mataifa mengi kupigana nawe, kama bahari iinuavyo mawimbi yake. Ezekieli 26:3

therefore thus says the Lord Yahweh, Behold, I am against you, Tyre, and will cause many nations to come up against you, as the sea causes its waves to come up.

Nao wataziharibu kuta za Tiro, na kuibomoa minara yake; tena nitakwangua hata mavumbi yake yamtoke, na kumfanya kuwa jabali tupu. Ezekieli 26:4

They shall destroy the walls of Tyre, and break down her towers: I will also scrape her dust from her, and make her a bare rock.

Naye atakuwa mahali pa kutandazia nyavu za wavuvi kati ya bahari; maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU; naye atakuwa mateka ya mataifa. Ezekieli 26:5

She shall be a place for the spreading of nets in the midst of the sea; for I have spoken it, says the Lord Yahweh; and she shall become a spoil to the nations.

Na binti zake walio katika mashamba watauawa kwa upanga; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Ezekieli 26:6

Her daughters who are in the field shall be slain with the sword: and they shall know that I am Yahweh.

Maana Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitamleta Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mfalme wa wafalme, juu ya Tiro toka kaskazini, pamoja na farasi, na magari ya vita, na wapanda farasi, na jeshi, na watu wengi. Ezekieli 26:7

For thus says the Lord Yahweh: Behold, I will bring on Tyre Nebuchadrezzar king of Babylon, king of kings, from the north, with horses, and with chariots, and with horsemen, and a company, and much people.

Atawaua binti zako kwa upanga katika mashamba; naye atafanya ngome juu yako, na kufanya maboma juu yako, na kuiinua ngao juu yako. Ezekieli 26:8

He shall kill with the sword your daughters in the field; and he shall make forts against you, and cast up a mound against you, and raise up the buckler against you.

Naye ataweka vyombo vyake vya kubomolea mbele za kuta zako, na kwa mashoka yake ataiangusha chini minara yako. Ezekieli 26:9

He shall set his battering engines against your walls, and with his axes he shall break down your towers.

Kwa sababu wingi wa farasi zake, mavumbi yao yatakufunika; kuta zako zitatetemeka kwa sababu ya mshindo wa wapanda farasi, na wa magurudumu, na wa magari ya vita, atakapoingia katika malango yako, kama watu waingiavyo katika mji uliobomolewa mahali. Ezekieli 26:10

By reason of the abundance of his horses their dust shall cover you: your walls shall shake at the noise of the horsemen, and of the wagons, and of the chariots, when he shall enter into your gates, as men enter into a city in which is made a breach.

Kwa kwato za farasi zake atazikanyaga njia zako zote; atawaua watu wako kwa upanga, na minara ya nguvu zako itashuka hata nchi. Ezekieli 26:11

With the hoofs of his horses shall he tread down all your streets; he shall kill your people with the sword; and the pillars of your strength shall go down to the ground.

Nao wataufanya utajiri wako kuwa mateka, na bidhaa yako kuwa mawindo; nao watazibomoa kuta zako, na kuziharibu nyumba zako zipendezazo; nao wataweka mawe yako, na miti yako, na mavumbi yako, kati ya maji. Ezekieli 26:12

They shall make a spoil of your riches, and make a prey of your merchandise; and they shall break down your walls, and destroy your pleasant houses; and they shall lay your stones and your timber and your dust in the midst of the waters.

Nami nitaikomesha sauti ya nyimbo zako, wala sauti ya vinubi vyako haitasikiwa tena. Ezekieli 26:13

I will cause the noise of your songs to cease; and the sound of your harps shall be no more heard.

Nami nitakufanya kuwa jabali tupu; utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za wavuvi; hutajengwa tena; maana mimi, Bwana, nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU. Ezekieli 26:14

I will make you a bare rock; you shall be a place for the spreading of nets; you shall be built no more: for I Yahweh have spoken it, says the Lord Yahweh.

Bwana MUNGU amwambia Tiro neno hili; Je! Visiwa havitatikisika kwa mshindo wa kuanguka kwako, watakapougua waliojeruhiwa, yatakapofanyika machinjo kati yako. Ezekieli 26:15

Thus says the Lord Yahweh to Tyre: shall not the isles shake at the sound of your fall, when the wounded groan, when the slaughter is made in the midst of you?

Ndipo wakuu wote wa bahari watashuka kutoka viti vyao vya enzi, na kuweka upande mavazi yao, na kuvua nguo zao zilizotiwa taraza; watajivika matetemeko; wataketi na kutetemeka kila dakika, na kukustaajabia, Ezekieli 26:16

Then all the princes of the sea shall come down from their thrones, and lay aside their robes, and strip off their embroidered garments: they shall clothe themselves with trembling; they shall sit on the ground, and shall tremble every moment, and be astonished at you.

Nao watakufanyia maombolezo, na kukuambia, Imekuwaje wewe kuharibika, wewe uliyekaliwa na wana-maji, mji wenye sifa, uliyekuwa na nguvu katika bahari, mji huo, na hao waliokaa ndani yake, waliowatia hofu wote waliokaa ndani yake! Ezekieli 26:17

They shall take up a lamentation over you, and tell you, How are you destroyed, who were inhabited by seafaring men, the renowned city, who was strong in the sea, she and her inhabitants, who caused their terror to be on all who lived there!

Sasa visiwa vitatetemeka katika siku ya kuanguka kwako; naam, visiwa vilivyo katika bahari vitafadhaika, kwa sababu ya kuondoka kwako. Ezekieli 26:18

Now shall the isles tremble in the day of your fall; yes, the isles that are in the sea shall be dismayed at your departure.

Maana Bwana MUNGU asema hivi; Nitakapokufanya kuwa mji wa ukiwa, kama miji isiyokaliwa na watu; nitakapoleta vilindi vya bahari juu yako, na maji makuu yatakapokufunika; Ezekieli 26:19

For thus says the Lord Yahweh: When I shall make you a desolate city, like the cities that are not inhabited; when I shall bring up the deep on you, and the great waters shall cover you;

ndipo nitakapokushusha pamoja nao washukao shimoni, uende kwa watu wa kale; nami nitakukalisha pande za chini za nchi; mahali palipokuwa ukiwa tangu zamani, pamoja nao washukao shimoni; ili usikaliwe na watu, wala usiweke utukufu wako katika nchi yao walio hai. Ezekieli 26:20

then will I bring you down with those who descend into the pit, to the people of old time, and will make you to dwell in the lower parts of the earth, in the places that are desolate of old, with those who go down to the pit, that you be not inhabited; and I will set glory in the land of the living:

Nitakufanya kuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwako tena; ujapotafutwa, lakini hutaonekana tena kabisa, asema Bwana MUNGU. Ezekieli 26:21

I will make you a terror, and you shall no more have any being; though you are sought for, yet shall you never be found again, says the Lord Yahweh.