Ezekieli 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ezekieli 17 (Swahili) Ezekiel 17 (English)

Neno la Bwana likanijia, kusema, Ezekieli 17:1

The word of Yahweh came to me, saying,

Mwanadamu, tega kitendawili, ukawaambie nyumba ya Israeli mithali; Ezekieli 17:2

Son of man, put forth a riddle, and speak a parable to the house of Israel;

useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tai mkubwa, mwenye mabawa makubwa na manyoya marefu katika mabawa, mwenye kujaa manyoya, yaliyo ya rangi mbalimbali, alifika Lebanoni, akakitwaa kilele cha mwerezi; Ezekieli 17:3

and say, Thus says the Lord Yahweh: A great eagle with great wings and long feathers, full of feathers, which had various colors, came to Lebanon, and took the top of the cedar:

akakikata kitawi kilicho juu katika vitawi vyake, akakichukua mpaka nchi ya biashara, akakiweka katika mji wa wachuuzi. Ezekieli 17:4

he cropped off the topmost of the young twigs of it, and carried it to a land of traffic; he set it in a city of merchants.

Akatwaa tena mbegu katika mbegu za nchi hiyo, akaipanda katika udongo uzaao sana, akaiweka kando ya maji mengi; aliipandikiza kama mti ukuao karibu na mto. Ezekieli 17:5

He took also of the seed of the land, and planted it in a fruitful soil; he placed it beside many waters; he set it as a willow tree.

Ikakua, ikawa mzabibu wenye kuenea sana, wa kimo kifupi, ambao matawi yake yalimgeukia, na mizizi yake ilikuwa chini yake; basi ukawa mzabibu, ukatoa matawi, ukachipuza vichipuko. Ezekieli 17:6

It grew, and became a spreading vine of low stature, whose branches turned toward him, and the roots of it were under him: so it became a vine, and brought forth branches, and shot forth sprigs.

Kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa makubwa na manyoya mengi; na tazama, mzabibu huo ukapinda mizizi yake imwelekee yeye, ukachipuza matawi yake yamwelekee yeye, toka matuta yake ulipopandwa; ili yeye apate kuunywesha. Ezekieli 17:7

There was also another great eagle with great wings and many feathers: and, behold, this vine did bend its roots toward him, and shot forth its branches toward him, from the beds of its plantation, that he might water it.

Ulikuwa umepandwa katika udongo mwema, kando ya maji mengi, upate kutoa matawi, na kuzaa matunda, uwe mzabibu mzuri. Ezekieli 17:8

It was planted in a good soil by many waters, that it might bring forth branches, and that it might bear fruit, that it might be a goodly vine.

Basi nena wewe, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Huo utafanikiwa? Yeye hataing'oa mizizi yake na kuyakata matunda yake, ili ukauke? Kwamba majani mabichi yake yote yachipukayo yakauke, hata ikiwa hana nguvu nyingi, wala watu wengi wa kuung'oa na mizizi yake? Ezekieli 17:9

Say you, Thus says the Lord Yahweh: Shall it prosper? shall he not pull up the roots of it, and cut off the fruit of it, that it may wither; that all its fresh springing leaves may wither? and not by a strong arm or much people can it be raised from the roots of it.

Naam, tazama, ingawa umepandwa, je! Utafanikiwa? Hautakauka kabisa, upepo wa mashariki utakapoupiga? Naam, utakauka katika matuta hapo ulipopandwa. Ezekieli 17:10

Yes, behold, being planted, shall it prosper? shall it not utterly wither, when the east wind touches it? it shall wither in the beds where it grew.

Tena neno la Bwana likanijia, kusema, Ezekieli 17:11

Moreover the word of Yahweh came to me, saying,

Waambie sasa nyumba hii iliyoasi, Hamjui maana ya mambo haya? Waambie, Tazama, mfalme wa Babeli alifika Yerusalemu, akamtwaa mfalme wake, na wakuu wake, akawachukua pamoja naye mpaka Babeli; Ezekieli 17:12

Say now to the rebellious house, Don't you know what these things mean? tell them, Behold, the king of Babylon came to Jerusalem, and took the king of it, and the princes of it, and brought them to him to Babylon:

akawatwaa baadhi ya wazao wa kifalme; kisha akafanya agano naye, akamwapisha; akawaondoa watu wa nchi wenye nguvu; Ezekieli 17:13

and he took of the seed royal, and made a covenant with him; he also brought him under an oath, and took away the mighty of the land;

ili ufalme huo uwe duni usijiinue, lakini usimame kwa kulishika agano lake. Ezekieli 17:14

that the kingdom might be base, that it might not lift itself up, but that by keeping his covenant it might stand.

Lakini alimwasi kwa kupeleka wajumbe huko Misri, wampe farasi na watu wengi. Je! Atafanikiwa? Afanyaye mambo hayo ataokoka? Atalivunja agano, kisha akaokoka? Ezekieli 17:15

But he rebelled against him in sending his ambassadors into Egypt, that they might give him horses and much people. Shall he prosper? shall he escape who does such things? shall he break the covenant, and yet escape?

Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika mahali pale akaapo mfalme aliyemmilikisha, ambaye alikidharau kiapo chake, na kulivunja agano lake, ndipo atakapokufa pamoja naye kati ya Babeli. Ezekieli 17:16

As I live, says the Lord Yahweh, surely in the place where the king dwells who made him king, whose oath he despised, and whose covenant he broke, even with him in the midst of Babylon he shall die.

Wala Farao na jeshi lake kubwa, na kusanyiko lake kuu la watu, hawatamfaa kitu vitani, watakapofanya maboma, na kujenga ngome, ili kukatilia mbali watu wengi. Ezekieli 17:17

Neither shall Pharaoh with his mighty army and great company help him in the war, when they cast up mounds and build forts, to cut off many persons.

Kwa maana amekidharau kiapo kwa kulivunja agano; na tazama, ametia mkono wake, na pamoja na hayo ameyatenda mambo hayo yote; hataokoka. Ezekieli 17:18

For he has despised the oath by breaking the covenant; and behold, he had given his hand, and yet has done all these things; he shall not escape.

Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mimi niishivyo, hakika kiapo changu alichokidharau, na agano langu alilolivunja, nitampatiliza kichwani pake. Ezekieli 17:19

Therefore thus says the Lord Yahweh: As I live, surely my oath that he has despised, and my covenant that he has broken, I will even bring it on his own head.

Nami nitatandika wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu, nami nitamleta hata Babeli; nami nitateta naye huko kwa sababu ya kosa lake alilonikosa. Ezekieli 17:20

I will spread my net on him, and he shall be taken in my snare, and I will bring him to Babylon, and will enter into judgment with him there for his trespass that he has trespassed against me.

Na wakimbizi wake wote wa vikosi vyake vyote wataanguka kwa upanga, na hao watakaosalia watatawanyika kwenye kila upepo; nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimenena neno hili. Ezekieli 17:21

All his fugitives in all his bands shall fall by the sword, and those who remain shall be scattered toward every wind: and you shall know that I, Yahweh, have spoken it.

Bwana MUNGU asema hivi; Mimi nami nitakitwaa kilele kirefu cha mwerezi, na kukipandikiza mahali; na katika vitawi vyake vilivyo juu nitatwaa kitawi kimoja kilicho chororo, nami nitakipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana; Ezekieli 17:22

Thus says the Lord Yahweh: I will also take of the lofty top of the cedar, and will set it; I will crop off from the topmost of its young twigs a tender one, and I will plant it on a high and lofty mountain:

juu ya mlima wa mahali palipoinuka pa Israeli nitakipanda; nacho kitatoa matawi, na kuzaa matunda, nao utakuwa mwerezi mzuri; na chini yake watakaa ndege wa kila namna ya mbawa; katika uvuli wa matawi yake watakaa. Ezekieli 17:23

in the mountain of the height of Israel will I plant it; and it shall bring forth boughs, and bear fruit, and be a goodly cedar: and under it shall dwell all birds of every wing; in the shade of the branches of it shall they dwell.

Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, Bwana, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, Bwana, nimenena, nami nimelitenda jambo hili. Ezekieli 17:24

All the trees of the field shall know that I, Yahweh, have brought down the high tree, have exalted the low tree, have dried up the green tree, and have made the dry tree to flourish; I, Yahweh, have spoken and have done it.