2 Wafalme 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 7 (Swahili) 2nd Kings 7 (English)

Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. 2 Wafalme 7:1

Elisha said, Hear you the word of Yahweh: thus says Yahweh, Tomorrow about this time shall a measure of fine flour be [sold] for a shekel, and two measures of barley for a shekel, in the gate of Samaria.

Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula. 2 Wafalme 7:2

Then the captain on whose hand the king leaned answered the man of God, and said, Behold, if Yahweh should make windows in heaven, might this thing be? He said, Behold, you shall see it with your eyes, but shall not eat of it.

Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? 2 Wafalme 7:3

Now there were four leprous men at the entrance of the gate: and they said one to another, Why sit we here until we die?

Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. 2 Wafalme 7:4

If we say, We will enter into the city, then the famine is in the city, and we shall die there; and if we sit still here, we die also. Now therefore come, and let us fall to the host of the Syrians: if they save us alive, we shall live; and if they kill us, we shall but die.

Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. 2 Wafalme 7:5

They rose up in the twilight, to go to the camp of the Syrians; and when they were come to the outermost part of the camp of the Syrians, behold, there was no man there.

Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. 2 Wafalme 7:6

For the Lord had made the host of the Syrians to hear a noise of chariots, and a noise of horses, even the noise of a great host: and they said one to another, Behold, the king of Israel has hired against us the kings of the Hittites, and the kings of the Egyptians, to come on us.

Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. 2 Wafalme 7:7

Therefore they arose and fled in the twilight, and left their tents, and their horses, and their donkeys, even the camp as it was, and fled for their life.

Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. 2 Wafalme 7:8

When these lepers came to the outermost part of the camp, they went into one tent, and ate and drink, and carried there silver, and gold, and clothing, and went and hid it; and they came back, and entered into another tent, and carried there also, and went and hid it.

Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. 2 Wafalme 7:9

Then they said one to another, We aren't doing right. This day is a day of good news, and we hold our peace: if we wait until the morning light, punishment will overtake us; now therefore come, let us go and tell the king's household.

Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. 2 Wafalme 7:10

So they came and called to the porter of the city; and they told them, saying, We came to the camp of the Syrians, and, behold, there was no man there, neither voice of man, but the horses tied, and the donkeys tied, and the tents as they were.

Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme. 2 Wafalme 7:11

He called the porters; and they told it to the king's household within.

Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonyesha ninyi walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha kondeni, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini. 2 Wafalme 7:12

The king arose in the night, and said to his servants, I will now show you what the Syrians have done to us. They know that we are hungry; therefore are they gone out of the camp to hide themselves in the field, saying, When they come out of the city, we shall take them alive, and get into the city.

Na mmojawapo wa watumishi wake akajibu, akasema, Kunradhi; baadhi ya watu na watwae farasi watano katika hao waliosalia, waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli waliobaki ndani yake; tazama, wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli walioangamia), tukawapeleke tukaone. 2 Wafalme 7:13

One of his servants answered, Please let some take five of the horses that remain, which are left in the city (behold, they are as all the multitude of Israel who are left in it; behold, they are as all the multitude of Israel who are consumed); and let us send and see.

Basi wakatwaa magari mawili na farasi zake; mfalme akawatuma kuwafuata Washami, akasema, Enendeni, mkaangalie. 2 Wafalme 7:14

They took therefore two chariots with horses; and the king sent after the host of the Syrians, saying, Go and see.

Wakawafuata mpaka Yordani; na kumbe! Njia yote ilikuwa imejaa mavazi na vyombo, walivyovitupa Washami, wapate kukimbia upesi. Watu wale waliotumwa wakarudi, wakamwambia mfalme. 2 Wafalme 7:15

They went after them to the Jordan: and, behold, all the way was full of garments and vessels, which the Syrians had cast away in their haste. The messengers returned, and told the king.

Basi watu wakatoka, wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, sawasawa na neno la Bwana. 2 Wafalme 7:16

The people went out, and plundered the camp of the Syrians. So a measure of fine flour was [sold] for a shekel, and two measures of barley for a shekel, according to the word of Yahweh.

Naye mfalme akamweka yule akida, ambaye alitegemea mkono wake, awasimamie watu langoni; na watu wakamkanyaga langoni, akafa; kama alivyosema yule mtu wa Mungu, aliyenena hapo mfalme alipomshukia. 2 Wafalme 7:17

The king appointed the captain on whose hand he leaned to have the charge of the gate: and the people trod on him in the gate, and he died as the man of God had said, who spoke when the king came down to him.

Ikatukia kama vile yule mtu wa Mungu alivyomwambia mfalme, Vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, na kipimo cha unga mzuri kwa shekeli, ndivyo vitakavyokuwa kesho, panapo saa hii, katika lango la Samaria; 2 Wafalme 7:18

It happened, as the man of God had spoken to the king, saying, Two measures of barley for a shekel, and a measure of fine flour for a shekel, shall be tomorrow about this time in the gate of Samaria;

na yule akida akamjibu mtu wa Mungu, akasema, Sasa tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akasema, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula. 2 Wafalme 7:19

and that captain answered the man of God, and said, Now, behold, if Yahweh should make windows in heaven, might such a thing be? and he said, Behold, you shall see it with your eyes, but shall not eat of it:

Ikampata vivyo hivyo, kwa kuwa watu wakamkanyaga langoni, akafa. 2 Wafalme 7:20

it happened even so to him; for the people trod on him in the gate, and he died.