2 Wafalme 22 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 22 (Swahili) 2nd Kings 22 (English)

Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; akatawala miaka thelathini na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Yedida, binti Adaya wa Bozkathi. 2 Wafalme 22:1

Josiah was eight years old when he began to reign; and he reigned thirty-one years in Jerusalem: and his mother's name was Jedidah the daughter of Adaiah of Bozkath.

Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, akaenda katika njia yote ya Daudi baba yake, wala hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto. 2 Wafalme 22:2

He did that which was right in the eyes of Yahweh, and walked in all the way of David his father, and didn't turn aside to the right hand or to the left.

Ikawa, katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yosia, mfalme akamtuma Shafani, mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, mwandishi, nyumbani kwa Bwana, akisema, 2 Wafalme 22:3

It happened in the eighteenth year of king Josiah, that the king sent Shaphan, the son of Azaliah the son of Meshullam, the scribe, to the house of Yahweh, saying,

Enenda kwa Hilkia, kuhani mkuu, ili aihesabu fedha yote inayoletwa nyumbani mwa Bwana, ambayo mabawabu wameipokea kwa watu; 2 Wafalme 22:4

Go up to Hilkiah the high priest, that he may sum the money which is brought into the house of Yahweh, which the keepers of the threshold have gathered of the people:

tena waitie ile fedha katika mikono ya wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya Bwana; wakapewe wafanya kazi waliomo ndani ya nyumba ya Bwana, ili wapate kupatengeneza mahali palipobomoka ndani ya nyumba; 2 Wafalme 22:5

and let them deliver it into the hand of the workmen who have the oversight of the house of Yahweh; and let them give it to the workmen who are in the house of Yahweh, to repair the breaches of the house,

wapewe maseremala, na wajenzi, na waashi; ili kununua miti na mawe yaliyochongwa wapate kuitengeneza nyumba. 2 Wafalme 22:6

to the carpenters, and to the builders, and to the masons, and for buying timber and hewn stone to repair the house.

Lakini hawakuulizwa habari za ile fedha waliyokabidhiwa; maana walitenda kazi kwa uaminifu. 2 Wafalme 22:7

However there was no reckoning made with them of the money that was delivered into their hand; for they dealt faithfully.

Naye Hilkia, kuhani mkuu, akamwambia Shafani, mwandishi, Nimekiona kitabu cha torati katika nyumba ya Bwana. Hilkia akampa Shafani kile kitabu, naye akakisoma. 2 Wafalme 22:8

Hilkiah the high priest said to Shaphan the scribe, I have found the book of the law in the house of Yahweh. Hilkiah delivered the book to Shaphan, and he read it.

Shafani mwandishi akamwendea mfalme, akamletea mfalme habari tena, akasema, Watumishi wako wamezitoa zile fedha zilizoonekana ndani ya nyumba, nao wamewakabidhi wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya Bwana. 2 Wafalme 22:9

Shaphan the scribe came to the king, and brought the king word again, and said, Your servants have emptied out the money that was found in the house, and have delivered it into the hand of the workmen who have the oversight of the house of Yahweh.

Kisha Shafani mwandishi akamwambia mfalme, akasema, Hilkia kuhani amenipa kitabu. Shafani akakisoma mbele ya mfalme. 2 Wafalme 22:10

Shaphan the scribe told the king, saying, Hilkiah the priest has delivered me a book. Shaphan read it before the king.

Ikawa, mfalme alipokwisha kuyasikia maneno ya kitabu hicho cha torati, alirarua nguo zake. 2 Wafalme 22:11

It happened, when the king had heard the words of the book of the law, that he tore his clothes.

Mfalme akamwamuru Hilkia kuhani, na Ahikamu, mwana wa Shafani, na Akbori, mwana wa Mikaya, na Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wa mfalme akasema, 2 Wafalme 22:12

The king commanded Hilkiah the priest, and Ahikam the son of Shaphan, and Achbor the son of Micaiah, and Shaphan the scribe, and Asaiah the king's servant, saying,

Enendeni, mkamwulize Bwana kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu hawa, na kwa ajili ya Yuda yote, katika habari za maneno ya kitabu hiki kilichoonekana; kwa kuwa hasira ya Bwana ni kubwa aliyotukasirikia, kwa sababu baba zetu hawakuyaangalia maneno ya kitabu hiki, kufanya kama hayo yote tuliyoandikiwa. 2 Wafalme 22:13

Go you, inquire of Yahweh for me, and for the people, and for all Judah, concerning the words of this book that is found; for great is the wrath of Yahweh that is kindled against us, because our fathers have not listened to the words of this book, to do according to all that which is written concerning us.

Basi Hilkia kuhani, na Ahikamu, na Akbori, na Shafani, na Asaya, wakamwendea Hulda, nabii mke, mkewe Shalumu, mwana wa Tikva, mwana wa Harhasi, mtunza mavazi ya mfalme; (naye alikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili;) wakasema naye. 2 Wafalme 22:14

So Hilkiah the priest, and Ahikam, and Achbor, and Shaphan, and Asaiah, went to Huldah the prophetess, the wife of Shallum the son of Tikvah, the son of Harhas, keeper of the wardrobe (now she lived in Jerusalem in the second quarter); and they talked with her.

Akawaambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi; Mwambieni mtu yule aliyewatuma ninyi kwangu, 2 Wafalme 22:15

She said to them, Thus says Yahweh, the God of Israel: Tell you the man who sent you to me,

Bwana asema hivi, Tazama, mimi nitaleta uovu juu ya mahali hapa, na juu yao wakaao hapa, naam, maneno yote ya kitabu alichokisoma mfalme wa Yuda; 2 Wafalme 22:16

Thus says Yahweh, Behold, I will bring evil on this place, and on the inhabitants of it, even all the words of the book which the king of Judah has read.

kwa sababu wameniacha mimi, wameifukizia uvumba miungu mingine, ili wapate kunikasirisha kwa kazi yote ya mikono yao; kwa hiyo hasira yangu itawaka juu ya mahali hapa, isizimike. 2 Wafalme 22:17

Because they have forsaken me, and have burned incense to other gods, that they might provoke me to anger with all the work of their hands, therefore my wrath shall be kindled against this place, and it shall not be quenched.

Lakini yule mfalme wa Yuda, aliyewatuma ninyi kumwuliza Bwana, mtamwambia hivi, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa habari ya maneno yale uliyoyasikia, 2 Wafalme 22:18

But to the king of Judah, who sent you to inquire of Yahweh, thus shall you tell him, Thus says Yahweh, the God of Israel: As touching the words which you have heard,

kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe ukajinyenyekesha mbele za Bwana, hapo ulipoyasikia maneno niliyoyanena juu ya mahali hapa, na juu ya wenyeji wake, ya kwamba watakuwa ukiwa na laana, nawe ulizirarua nguo zako, ukalia mbele zangu; basi, mimi nami nimekusikia wewe, asema Bwana. 2 Wafalme 22:19

because your heart was tender, and you did humble yourself before Yahweh, when you heard what I spoke against this place, and against the inhabitants of it, that they should become a desolation and a curse, and have torn your clothes, and wept before me; I also have heard you, says Yahweh.

Kwa hiyo tazama, nitakukusanya pamoja na baba zako, nawe utawekwa kaburini mwako kwa amani; wala macho yako hayatauona uovu huo wote nitakaouleta juu ya mahali hapa. Basi wakamletea mfalme habari tena. 2 Wafalme 22:20

Therefore, behold, I will gather you to your fathers, and you shall be gathered to your grave in peace, neither shall your eyes see all the evil which I will bring on this place. They brought the king word again.