2 Wafalme 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 5 (Swahili) 2nd Kings 5 (English)

Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake Bwana alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma. 2 Wafalme 5:1

Now Naaman, captain of the host of the king of Syria, was a great man with his master, and honorable, because by him Yahweh had given victory to Syria: he was also a mighty man of valor, [but he was] a leper.

Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani. 2 Wafalme 5:2

The Syrians had gone out in bands, and had brought away captive out of the land of Israel a little maiden; and she waited on Naaman's wife.

Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake. 2 Wafalme 5:3

She said to her mistress, Would that my lord were with the prophet who is in Samaria! then would he recover him of his leprosy.

Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi. 2 Wafalme 5:4

One went in, and told his lord, saying, Thus and thus said the maiden who is of the land of Israel.

Mfalme wa Shamu akasema, Haya! Basi, mimi nitampelekea mfalme wa Israeli waraka. Basi akaenda zake, akachukua mikononi mwake talanta kumi za fedha, na vipande vya dhahabu elfu sita, na mavazi kumi. 2 Wafalme 5:5

The king of Syria said, Go now, and I will send a letter to the king of Israel. He departed, and took with him ten talents of silver, and six thousand [pieces] of gold, and ten changes of clothing.

Akampelekea mfalme wa Israeli waraka ule, kusema, Waraka huu utakapokuwasilia, tazama, nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, ili upate kumponya ukoma wake. 2 Wafalme 5:6

He brought the letter to the king of Israel, saying, Now when this letter is come to you, behold, I have sent Naaman my servant to you, that you may recover him of his leprosy.

Ikawa, mfalme wa Israeli alipousoma waraka, alirarua mavazi yake, akasema, Je! Mimi ni Mungu, niue na kuhuisha, hata mtu huyu akanipelekea mtu nimponye ukoma wake? Fahamuni, basi, nakusihini, mwone ya kuwa mtu huyu anataka kugombana nami. 2 Wafalme 5:7

It happened, when the king of Israel had read the letter, that he tore his clothes, and said, Am I God, to kill and to make alive, that this man does send to me to recover a man of his leprosy? but consider, I pray you, and see how he seeks a quarrel against me.

Ikawa, Elisha, yule mtu wa Mungu, aliposikia kwamba mfalme wa Israeli ameyararua mavazi yake, ndipo akatuma mtu kwa mfalme, akisema, Mbona umeyararua mavazi yako? Na aje sasa kwangu mimi, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli. 2 Wafalme 5:8

It was so, when Elisha the man of God heard that the king of Israel had torn his clothes, that he sent to the king, saying, Why have you torn your clothes? let him come now to me, and he shall know that there is a prophet in Israel.

Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake, akasimama mlangoni pa nyumba ya Elisha. 2 Wafalme 5:9

So Naaman came with his horses and with his chariots, and stood at the door of the house of Elisha.

Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi. 2 Wafalme 5:10

Elisha sent a messenger to him, saying, Go and wash in the Jordan seven times, and your flesh shall come again to you, and you shall be clean.

Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma. 2 Wafalme 5:11

But Naaman was angry, and went away, and said, Behold, I thought, He will surely come out to me, and stand, and call on the name of Yahweh his God, and wave his hand over the place, and recover the leper.

Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira. 2 Wafalme 5:12

Aren't Abanah and Pharpar, the rivers of Damascus, better than all the waters of Israel? may I not wash in them, and be clean? So he turned and went away in a rage.

Watumishi wake wakamkaribia, wakamwambia, wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi? 2 Wafalme 5:13

His servants came near, and spoke to him, and said, My father, if the prophet had bid you do some great thing, wouldn't you have done it? how much rather then, when he says to you, Wash, and be clean?

Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi. 2 Wafalme 5:14

Then went he down, and dipped [himself] seven times in the Jordan, according to the saying of the man of God; and his flesh came again like the flesh of a little child, and he was clean.

Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako. 2 Wafalme 5:15

He returned to the man of God, he and all his company, and came, and stood before him; and he said, See now, I know that there is no God in all the earth, but in Israel: now therefore, please take a present from your servant.

Lakini akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa. 2 Wafalme 5:16

But he said, As Yahweh lives, before whom I stand, I will receive none. He urged him to take it; but he refused.

Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana. 2 Wafalme 5:17

Naaman said, If not, yet, please let there be given to your servant two mules' burden of earth; for your servant will henceforth offer neither burnt offering nor sacrifice to other gods, but to Yahweh.

Jambo hili Bwana amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, Bwana amwachilie mtumwa wako jambo hili. 2 Wafalme 5:18

In this thing Yahweh pardon your servant: when my master goes into the house of Rimmon to worship there, and he leans on my hand, and I bow myself in the house of Rimmon, when I bow myself in the house of Rimmon, Yahweh pardon your servant in this thing.

Akamwambia, Enenda kwa amani Basi akamwondokea mbali kidogo. 2 Wafalme 5:19

He said to him, Go in peace. So he departed from him a little way.

Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake. 2 Wafalme 5:20

But Gehazi the servant of Elisha the man of God, said, Behold, my master has spared this Naaman the Syrian, in not receiving at his hands that which he brought: as Yahweh lives, I will run after him, and take somewhat of him.

Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani? 2 Wafalme 5:21

So Gehazi followed after Naaman. When Naaman saw one running after him, he alighted from the chariot to meet him, and said, Is all well?

Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili. 2 Wafalme 5:22

He said, All is well. My master has sent me, saying, Behold, even now there are come to me from the hill-country of Ephraim two young men of the sons of the prophets; please give them a talent of silver, and two changes of clothing.

Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake. 2 Wafalme 5:23

Naaman said, Be pleased to take two talents. He urged him, and bound two talents of silver in two bags, with two changes of clothing, and laid them on two of his servants; and they bore them before him.

Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao. 2 Wafalme 5:24

When he came to the hill, he took them from their hand, and bestowed them in the house; and he let the men go, and they departed.

Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali. 2 Wafalme 5:25

But he went in, and stood before his master. Elisha said to him, Whence come you, Gehazi? He said, Your servant went no where.

Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi? 2 Wafalme 5:26

He said to him, Didn't my heart go with you, when the man turned from his chariot to meet you? Is it a time to receive money, and to receive garments, and olive groves and vineyards, and sheep and oxen, and men-servants and maid-servants?

Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.

2 Wafalme 5:27

The leprosy therefore of Naaman shall cleave to you, and to your seed forever. He went out from his presence a leper [as white] as snow.