2 Wafalme 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 6 (Swahili) 2nd Kings 6 (English)

Kisha, wana wa manabii wakamwambia Elisha, Angalia basi, mahali tukaapo mbele yako ni padogo kwetu. 2 Wafalme 6:1

The sons of the prophets said to Elisha, See now, the place where we dwell before you is too strait for us.

Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni. 2 Wafalme 6:2

Let us go, we pray you, to the Jordan, and take there every man a beam, and let us make us a place there, where we may dwell. He answered, Go you.

Mmoja wao akasema, Uwe radhi, basi nakusihi, uende pamoja na watumishi wako. Akajibu, Nitakwenda. 2 Wafalme 6:3

One said, Be pleased, I pray you, to go with your servants. He answered, I will go.

Basi, akaenda pamoja nao. Nao walipofika Yordani, wakakata miti. 2 Wafalme 6:4

So he went with them. When they came to the Jordan, they cut down wood.

Lakini mmojawapo alipokuwa katika kukata boriti, chuma cha shoka kikaanguka majini; akalia, akasema, Ole wangu! Bwana wangu, kwani kiliazimiwa kile. 2 Wafalme 6:5

But as one was felling a beam, the axe head fell into the water; and he cried, and said, Alas, my master! for it was borrowed.

Mtu wa Mungu akasema, Kilianguka wapi? Akamwonyesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea. 2 Wafalme 6:6

The man of God said, Where fell it? He shown him the place. He cut down a stick, and cast it in there, and made the iron to swim.

Akasema, Kiokote. Basi akanyosha mkono, akakitwaa. 2 Wafalme 6:7

He said, Take it up to you. So he put out his hand, and took it.

Basi, mfalme wa Shamu alikuwa akifanya vita na Israeli. Akafanya mashauri na watumishi wake, akasema, Kituo changu kitakuwapo mahali fulani. 2 Wafalme 6:8

Now the king of Syria was warring against Israel; and he took counsel with his servants, saying, In such and such a place shall be my camp.

Yule mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, kusema, Jihadhari, usipite mahali fulani; kwa sababu ndiko wanakoshukia Washami. 2 Wafalme 6:9

The man of God sent to the king of Israel, saying, Beware that you not pass such a place; for there the Syrians are coming down.

Mfalme wa Israeli akapeleka watu mpaka mahali pale alipoambiwa na yule mtu wa Mungu, na kuhadharishwa; akajiokoa nafsi yake, si mara moja, wala si mara mbili. 2 Wafalme 6:10

The king of Israel sent to the place which the man of God told him and warned him of; and he saved himself there, not once nor twice.

Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionyesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli? 2 Wafalme 6:11

The heart of the king of Syria was sore troubled for this thing; and he called his servants, and said to them, Won't you show me which of us is for the king of Israel?

Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala. 2 Wafalme 6:12

One of his servants said, No, my lord, O king; but Elisha, the prophet who is in Israel, tells the king of Israel the words that you speak in your bedchamber.

Akasema, Enendeni, mkamwangalie aliko, nipate kupeleka watu kwenda kumchukua. Akaambiwa ya kwamba, Tazama, yuko Dothani. 2 Wafalme 6:13

He said, Go and see where he is, that I may send and get him. It was told him, saying, Behold, he is in Dothan.

Kwa hiyo akapeleka huko farasi, na magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku, wakauzingira mji ule pande zote. 2 Wafalme 6:14

Therefore sent he there horses, and chariots, and a great host: and they came by night, and surrounded the city.

Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje? 2 Wafalme 6:15

When the servant of the man of God was risen early, and gone forth, behold, a host with horses and chariots was round about the city. His servant said to him, Alas, my master! how shall we do?

Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. 2 Wafalme 6:16

He answered, Don't be afraid; for those who are with us are more than those who are with them.

Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote. 2 Wafalme 6:17

Elisha prayed, and said, Yahweh, Please open his eyes, that he may see. Yahweh opened the eyes of the young man; and he saw: and, behold, the mountain was full of horses and chariots of fire round about Elisha.

Na walipomtelemkia Elisha akamwomba Bwana, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha. 2 Wafalme 6:18

When they came down to him, Elisha prayed to Yahweh, and said, Please smite this people with blindness. He struck them with blindness according to the word of Elisha.

Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria. 2 Wafalme 6:19

Elisha said to them, This is not the way, neither is this the city: follow me, and I will bring you to the man whom you seek. He led them to Samaria.

Hata walipokwisha kuingia Samaria, Elisha akasema, Bwana wafumbue macho watu hawa, wapate kuona. Bwana akawafumbua macho wakaona; kumbe! Walikuwa katikati ya Samaria. 2 Wafalme 6:20

It happened, when they were come into Samaria, that Elisha said, Yahweh, open the eyes of these men, that they may see. Yahweh opened their eyes, and they saw; and, behold, they were in the midst of Samaria.

Naye mfalme wa Israeli alipowaona, akamwambia Elisha, Ee baba yangu, niwapige? Niwapige? 2 Wafalme 6:21

The king of Israel said to Elisha, when he saw them, My father, shall I strike them? shall I strike them?

Akamjibu, Usiwapige; je! Ungetaka kuwapiga watu ambao umewatwaa mateka kwa upanga wako na uta wako? Weka chakula na maji mbele yao, wapate kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao. 2 Wafalme 6:22

He answered, You shall not strike them: would you strike those whom you have taken captive with your sword and with your bow? set bread and water before them, that they may eat and drink, and go to their master.

Basi akawaandalia chakula tele; nao walipokwisha kula na kunywa, akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikosi vya Shamu havikuja tena katika nchi ya Israeli. 2 Wafalme 6:23

He prepared great provision for them; and when they had eaten and drunk, he sent them away, and they went to their master. The bands of Syria came no more into the land of Israel.

Ikawa baada ya hayo, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya majeshi yake yote, akakwea akauhusuru Samaria. 2 Wafalme 6:24

It happened after this, that Benhadad king of Syria gathered all his host, and went up, and besieged Samaria.

Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha. 2 Wafalme 6:25

There was a great famine in Samaria: and, behold, they besieged it, until a donkey's head was sold for eighty [pieces] of silver, and the fourth part of a kab of dove's dung for five [pieces] of silver.

Ikawa mfalme wa Israeli alipokuwa akipita ukutani, mwanamke mmoja akamwita akisema, Unisaidie, bwana wangu, mfalme. 2 Wafalme 6:26

As the king of Israel was passing by on the wall, there cried a woman to him, saying, Help, my lord, O king.

Akasema, Bwana asipokusaidia, nikusaidieje mimi? Ya sakafuni, au ya shinikizoni? 2 Wafalme 6:27

He said, If Yahweh doesn't help you, whence shall I help you? out of the threshing floor, or out of the winepress?

Mfalme akamwambia, Una nini? Akajibu, Mwanamke huyu aliniambia, Mtoe mtoto wako, tumle leo, na mtoto wangu tutamla kesho. 2 Wafalme 6:28

The king said to her, What ails you? She answered, This woman said to me, Give your son, that we may eat him today, and we will eat my son tomorrow.

Basi, tukamtokosa mtoto wangu, tukamla; nikamwambia siku ya pili, Mtoe mtoto wako, tumle; naye amemficha mtoto wake. 2 Wafalme 6:29

So we boiled my son, and ate him: and I said to her on the next day, Give your son, that we may eat him; and she has hid her son.

Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya huyo mwanamke, aliyararua mavazi yake; (naye alikuwa akipita juu ya ukuta;) na watu wakaona, na tazama, alikuwa amevaa magunia ndani mwilini mwake. 2 Wafalme 6:30

It happened, when the king heard the words of the woman, that he tore his clothes (now he was passing by on the wall); and the people looked, and, behold, he had sackcloth within on his flesh.

Ndipo akasema, Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, kikimbakia kichwa Elisha mwana wa Shafati juu yake leo. 2 Wafalme 6:31

Then he said, God do so to me, and more also, if the head of Elisha the son of Shaphat shall stand on him this day.

Lakini Elisha alikuwa akikaa nyumbani mwake, na wazee wakikaa pamoja naye; na mfalme akamtuma mtu wa mbele yake; lakini hata kabla ya kufika kwake yule aliyetumwa, akawaambia wazee, Je! Mwaona jinsi huyu mwana wa mwuaji alivyotuma aniondolee kichwa changu? Angalieni, huyo aliyetumwa akifika, fungeni mlango, mkamzuie mlangoni; je! Sauti ya miguu ya bwana wake haiko nyuma yake? 2 Wafalme 6:32

But Elisha was sitting in his house, and the elders were sitting with him; and [the king] sent a man from before him: but before the messenger came to him, he said to the elders, See you how this son of a murderer has sent to take away my head? behold, when the messenger comes, shut the door, and hold the door fast against him: isn't the sound of his master's feet behind him?

Hata alipokuwa katika kusema nao, tazama, yule aliyetumwa akamshukia; naye akasema, Angalia, mabaya haya yatoka kwa Bwana; kwani mimi kumngojea Bwana tena? 2 Wafalme 6:33

While he was yet talking with them, behold, the messenger came down to him: and he said, Behold, this evil is of Yahweh; why should I wait for Yahweh any longer?