2 Wafalme 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 19 (Swahili) 2nd Kings 19 (English)

Ikawa mfalme Hezekia aliposikia hayo, alizirarua nguo zake, akajivika nguo za magunia, akaingia katika nyumba ya Bwana. 2 Wafalme 19:1

It happened, when king Hezekiah heard it, that he tore his clothes, and covered himself with sackcloth, and went into the house of Yahweh.

Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wamevikwa nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi. 2 Wafalme 19:2

He sent Eliakim, who was over the household, and Shebna the scribe, and the elders of the priests, covered with sackcloth, to Isaiah the prophet the son of Amoz.

Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wa tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa. 2 Wafalme 19:3

They said to him, Thus says Hezekiah, This day is a day of trouble, and of rebuke, and of rejection; for the children are come to the birth, and there is not strength to bring forth.

Yamkini Bwana, Mungu wako, atayasikia maneno yote ya amiri huyu, ambaye mfalme wa Ashuru ,bwana wake,amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai,naye atayakemea hayo maneno aliyoyasikia BWANA ,Mungu wako;kwa sababu hii inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia. 2 Wafalme 19:4

It may be Yahweh your God will hear all the words of Rabshakeh, whom the king of Assyria his master has sent to defy the living God, and will rebuke the words which Yahweh your God has heard. Therefore lift up your prayer for the remnant that is left.

Basi watumishi wa mfalme Hezekia wakamwendea Isaya. 2 Wafalme 19:5

So the servants of king Hezekiah came to Isaiah.

Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu maneno haya; Bwana asema hivi, Usiyaogope maneno hayo uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana. 2 Wafalme 19:6

Isaiah said to them, Thus shall you tell your master, Thus says Yahweh, Don't be afraid of the words that you have heard, with which the servants of the king of Assyria have blasphemed me.

Tazama, nitatia roho ya hofu ndani yake, naye atasikia kivumi, na kuirudia nchi yake mwenyewe; nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe. 2 Wafalme 19:7

Behold, I will put a spirit in him, and he shall hear news, and shall return to his own land; and I will cause him to fall by the sword in his own land.

Basi yule amiri akarudi, akamkuta mfalme wa Ashuru, anapigana na Libna; maana alikuwa amesikia ya kwamba ameondoka, akaacha Lakishi. 2 Wafalme 19:8

So Rabshakeh returned, and found the king of Assyria warring against Libnah; for he had heard that he was departed from Lachish.

Na aliposikia habari ya Tirhaka mfalme wa Kushi, ya kwamba, Tazama, ametoka ili kupigana nawe; alituma wajumbe kwa Hezekia mara ya pili, kusema, 2 Wafalme 19:9

When he heard say of Tirhakah king of Ethiopia, Behold, he is come out to fight against you, he sent messengers again to Hezekiah, saying,

Mwambieni Hezekia, mfalme wa Yuda, maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema, Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru. 2 Wafalme 19:10

Thus shall you speak to Hezekiah king of Judah, saying, Don't let your God in whom you trust deceive you, saying, Jerusalem shall not be given into the hand of the king of Assyria.

Tazama, umesikia ni mambo gani wafalme wa Ashuru waliyozitenda nchi zote, kwa kuziangamiza kabisa; je! Utaokoka wewe? 2 Wafalme 19:11

Behold, you have heard what the kings of Assyria have done to all lands, by destroying them utterly: and shall you be delivered?

Je! Miungu ya mataifa wale, ambao baba zangu waliwaangamiza, imewaokoa? Yaani, Gozani, na Harani, na Resefu, na wana wa Adini waliokuwa katika Telasari? 2 Wafalme 19:12

Have the gods of the nations delivered them, which my fathers have destroyed, Gozan, and Haran, and Rezeph, and the children of Eden that were in Telassar?

Yuko wapi mfalme wa Hamathi, na mfalme wa Arpadi, na mfalme wa mji wa Sefarvaimu, na wa Hena, na wa Iva? 2 Wafalme 19:13

Where is the king of Hamath, and the king of Arpad, and the king of the city of Sepharvaim, of Hena, and Ivvah?

Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya Bwana, akaukunjua mbele za Bwana. 2 Wafalme 19:14

Hezekiah received the letter from the hand of the messengers, and read it; and Hezekiah went up to the house of Yahweh, and spread it before Yahweh.

Naye Hezekia akaomba mbele za Bwana, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia; wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi. 2 Wafalme 19:15

Hezekiah prayed before Yahweh, and said, Yahweh, the God of Israel, who sit [above] the cherubim, you are the God, even you alone, of all the kingdoms of the earth; you have made heaven and earth.

Tega sikio lako, Ee Bwana, usikie; fumbua macho yako, Ee Bwana, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, ambayo amemtuma mtu aje nayo ili kumtukana Mungu aliye hai. 2 Wafalme 19:16

Incline your ear, Yahweh, and hear; open your eyes, Yahweh, and see; and hear the words of Sennacherib, with which he has sent him to defy the living God.

Ni kweli, Bwana, wafalme wa Ashuru wamewaharibu mataifa na nchi zao, 2 Wafalme 19:17

Of a truth, Yahweh, the kings of Assyria have laid waste the nations and their lands,

na kuitupa miungu yao motoni; kwa maana haikuwa miungu, bali ni kazi ya mikono ya wanadamu; ilikuwa miti na mawe tu, ndiyo sababu wakaiharibu. 2 Wafalme 19:18

and have cast their gods into the fire; for they were no gods, but the work of men's hands, wood and stone; therefore they have destroyed them.

Basi sasa, Ee Bwana, Mungu wetu, utuokoe na mkono wake, nakusihi, ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe Bwana Mungu, wewe peke yako. 2 Wafalme 19:19

Now therefore, Yahweh our God, save you us, I beg you, out of his hand, that all the kingdoms of the earth may know that you Yahweh are God alone.

Ndipo Isaya, mwana wa Amozi, akapeleka ujumbe kwa Hezekia, akisema, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa kuwa umeniomba juu ya Senakeribu, mfalme wa Ashuru, mimi nimekusikia. 2 Wafalme 19:20

Then Isaiah the son of Amoz sent to Hezekiah, saying, Thus says Yahweh, the God of Israel, Whereas you have prayed to me against Sennacherib king of Assyria, I have heard [you].

Tamko alilolitamka Bwana katika habari zake ndilo hili, Bikira, binti Sayuni, amekudharau, na kukudhihaki sana; binti Yerusalemu ametikisa kichwa chake juu yako. 2 Wafalme 19:21

This is the word that Yahweh has spoken concerning him: The virgin daughter of Zion has despised you and ridiculed you; the daughter of Jerusalem has shaken her head at you.

Ni nani uliyemshutumu na kumtukana? Umeinua sauti yako juu ya nani, na kuinua macho yako juu? Juu ya Mtakatifu wa Israeli. 2 Wafalme 19:22

Whom have you defied and blasphemed? and against whom have you exalted your voice and lifted up your eyes on high? [even] against the Holy One of Israel.

Kwa vinywa vya wajumbe wako umemshutumu Bwana, ukasema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani pa Lebanoni. Nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misunobari yake mizuri; nami nitaingia ndani ya makazi yake yaliyo mbali sana, na msitu wa shamba lake lizaalo sana. 2 Wafalme 19:23

By your messengers you have defied the Lord, and have said, With the multitude of my chariots am I come up to the height of the mountains, to the innermost parts of Lebanon; and I will cut down the tall cedars of it, and the choice fir trees of it; and I will enter into his farthest lodging-place, the forest of his fruitful field.

Nimechimba na kunywa maji mageni, na kwa nyayo za miguu yangu nitaikausha mito yote ya Misri. 2 Wafalme 19:24

I have dug and drunk strange waters, and with the sole of my feet will I dry up all the rivers of Egypt.

Je! Hukusikia wewe ya kuwa mimi ndimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale? Sasa mimi nimelitimiza jambo hili, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, hata ikawe chungu na magofu. 2 Wafalme 19:25

Haven't you heard how I have done it long ago, and formed it of ancient times? now have I brought it to pass, that it should be yours to lay waste fortified cities into ruinous heaps.

Ndiyo sababu wenyeji wao walikuwa na nguvu chache, wakafadhaika, na kuhangaika; wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, na kama ngano iliyokaushwa kabla haijaiva. 2 Wafalme 19:26

Therefore their inhabitants were of small power, they were dismayed and confounded; they were as the grass of the field, and as the green herb, as the grass on the housetops, and as grain blasted before it is grown up.

Lakini nakujua, kuketi kwako, na kutoka kwako, na kuingia kwako; na ghadhabu yako unayonighadhibikia. 2 Wafalme 19:27

But I know your sitting down, and your going out, and your coming in, and your raging against me.

Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu; kwa sababu hiyo nitatia kulabu yangu puani mwako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijia. 2 Wafalme 19:28

Because of your raging against me, and because your arrogance is come up into my ears, therefore will I put my hook in your nose, and my bridle in your lips, and I will turn you back by the way by which you came.

Na kwako wewe hii ndiyo dalili; mwaka huu mtakula vitu viotavyo vyenyewe; na mwaka wa pili mtakula mazao ya vitu hivyo; na mwaka wa tatu pandeni mbegu, kavuneni; mkapande mashamba ya mizabibu, mkale matunda yake. 2 Wafalme 19:29

This shall be the sign to you: You shall eat this year that which grows of itself, and in the second year that which springs of the same; and in the third year sow you, and reap, and plant vineyards, and eat the fruit of it.

Na mabaki yaliyookoka ya nyumba ya Yuda yatatia mizizi chini, na kuzaa matunda juu. 2 Wafalme 19:30

The remnant that has escaped of the house of Judah shall again take root downward, and bear fruit upward.

Maana mabaki yatatoka katika Yerusalemu, na wao watakaookoka katika mlima wa Sayuni wivu wa Bwana utatimiza jambo hilo. 2 Wafalme 19:31

For out of Jerusalem shall go forth a remnant, and out of Mount Zion those who shall escape: the zeal of Yahweh shall perform this.

Basi Bwana asema hivi katika habari za mfalme wa Ashuru, Yeye hatauingia mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake. 2 Wafalme 19:32

Therefore thus says Yahweh concerning the king of Assyria, He shall not come to this city, nor shoot an arrow there, neither shall he come before it with shield, nor cast up a mound against it.

Njia ile ile aliyojia, kwa njia iyo hiyo atarudi zake, wala hataingia ndani ya mji huu, asema Bwana. 2 Wafalme 19:33

By the way that he came, by the same shall he return, and he shall not come to this city, says Yahweh.

Maana nitaulinda mji huu, niuokoe, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu. 2 Wafalme 19:34

For I will defend this city to save it, for my own sake, and for my servant David's sake.

Ikawa usiku uo huo malaika wa Bwana alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano elfu. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia. 2 Wafalme 19:35

It happened that night, that the angel of Yahweh went forth, and struck in the camp of the Assyrians one hundred eighty-five thousand: and when men arose early in the morning, behold, these were all dead bodies.

Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akaondoka, akaenda zake, akarudi akakaa Ninawi. 2 Wafalme 19:36

So Sennacherib king of Assyria departed, and went and returned, and lived at Nineveh.

Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake. 2 Wafalme 19:37

It happened, as he was worshipping in the house of Nisroch his god, that Adrammelech and Sharezer struck him with the sword: and they escaped into the land of Ararat. Esar Haddon his son reigned in his place.