2 Wafalme 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 2 (Swahili) 2nd Kings 2 (English)

Ikawa, hapo Bwana alipopenda kumpandisha Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha. 2 Wafalme 2:1

It happened, when Yahweh would take up Elijah by a whirlwind into heaven, that Elijah went with Elisha from Gilgal.

Eliya akamwambia Elisha, Tafadhali, kaa hapa; maana Bwana amenituma niende mpaka Betheli. 2 Wafalme 2:2

Elijah said to Elisha, Please wait here, for Yahweh has sent me as far as Bethel. Elisha said, As Yahweh lives, and as your soul lives, I will not leave you. So they went down to Bethel.

Elisha akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha, Basi wakashuka mpaka Betheli. Basi wana wa manabii, waliokuwako Betheli, wakatoka kuonana na Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa Bwana atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akasema, Naam, najua; nyamazeni. 2 Wafalme 2:3

The sons of the prophets who were at Bethel came forth to Elisha, and said to him, "Do you know that Yahweh will take away your master from your head today?" He said, "Yes, I know it; hold your peace."

Eliya akamwambia, Tafadhali, kaa hapa, Elisha; maana Bwana amenituma niende mpaka Yeriko. Akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Nao wakafika Yeriko. 2 Wafalme 2:4

Elijah said to him, Elisha, please wait here, for Yahweh has sent me to Jericho. He said, As Yahweh lives, and as your soul lives, I will not leave you. So they came to Jericho.

Basi wana wa manabii, waliokuwako Yeriko, wakamkaribia Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa Bwana atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akajibu, Naam, najua, nyamazeni. 2 Wafalme 2:5

The sons of the prophets who were at Jericho came near to Elisha, and said to him, "Do you know that Yahweh will take away your master from your head today?" He answered, "Yes, I know it. Hold your peace."

Eliya akamwambia, Tafadhali kaa hapa; maana Bwana amenituma niende mpaka Yordani. Akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Wakaendelea mbele wote wawili. 2 Wafalme 2:6

Elijah said to him, "Please wait here, for Yahweh has sent me to the Jordan." He said, "As Yahweh lives, and as your soul lives, I will not leave you." They two went on.

Basi watu hamsini wa wale wana wa manabii wakaenda wakasimama, kuwakabili kwa mbali; na hao wawili wakasimama karibu na Yordani. 2 Wafalme 2:7

Fifty men of the sons of the prophets went, and stood over against them afar off: and they two stood by the Jordan.

Eliya akalitwaa vazi lake la juu, akalikunja, akayapiga maji, yakagawanyika huku na huku, na hao wawili wakavuka pakavu. 2 Wafalme 2:8

Elijah took his mantle, and wrapped it together, and struck the waters, and they were divided here and there, so that they two went over on dry ground.

Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu. 2 Wafalme 2:9

It happened, when they had gone over, that Elijah said to Elisha, Ask what I shall do for you, before I am taken from you. Elisha said, please let a double portion of your spirit be on me.

Akasema, Umeomba neno gumu; lakini, ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la hukuniona, hulipati. 2 Wafalme 2:10

He said, You have asked a hard thing: [nevertheless], if you see me when I am taken from you, it shall be so to you; but if not, it shall not be so.

Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli. 2 Wafalme 2:11

It happened, as they still went on, and talked, that behold, [there appeared] a chariot of fire, and horses of fire, which parted them both apart; and Elijah went up by a whirlwind into heaven.

Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa; akashika mavazi yake mwenyewe, akayararua vipande viwili. 2 Wafalme 2:12

Elisha saw it, and he cried, My father, my father, the chariots of Israel and the horsemen of it! He saw him no more: and he took hold of his own clothes, and tore them in two pieces.

Kisha akaliokota lile vazi la Eliya lililomwangukia, akarudi, akasimama katika ukingo wa Yordani. 2 Wafalme 2:13

He took up also the mantle of Elijah that fell from him, and went back, and stood by the bank of the Jordan.

Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka. 2 Wafalme 2:14

He took the mantle of Elijah that fell from him, and struck the waters, and said, Where is Yahweh, the God of Elijah? and when he also had struck the waters, they were divided here and there; and Elisha went over.

Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake. 2 Wafalme 2:15

When the sons of the prophets who were at Jericho over against him saw him, they said, The spirit of Elijah does rest on Elisha. They came to meet him, and bowed themselves to the ground before him.

Wakamwambia, Angalia, wako hapa pamoja nasi watumishi wako watu hamsini walio hodari; waende, twakuomba, wamtafute bwana wako; isiwe labda roho ya Bwana imemtwaa na kumtupa juu ya mlima mmoja, au katika bonde moja. Akasema, Msiwatume. 2 Wafalme 2:16

They said to him, See now, there are with your servants fifty strong men; let them go, we pray you, and seek your master, lest the Spirit of Yahweh has taken him up, and cast him on some mountain, or into some valley. He said, You shall not send.

Wakamsisitiza hata akaona haya, akasema, Haya! Watumeni. Basi wakatuma watu hamsini; nao wakatafuta siku tatu, wasimwone. 2 Wafalme 2:17

When they urged him until he was ashamed, he said, Send. They sent therefore fifty men; and they sought three days, but didn't find him.

Wakamrudia, alipokuwa anakawia Yeriko; akawaambia, Je! Mimi sikuwaambia, Msiende? 2 Wafalme 2:18

They came back to him, while he stayed at Jericho; and he said to them, "Didn't I tell you, 'Don't go?'"

Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. 2 Wafalme 2:19

The men of the city said to Elisha, Behold, we pray you, the situation of this city is pleasant, as my lord sees: but the water is bad, and the land miscarries.

Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. 2 Wafalme 2:20

He said, Bring me a new jar, and put salt therein. They brought it to him.

Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. 2 Wafalme 2:21

He went forth to the spring of the waters, and cast salt therein, and said, Thus says Yahweh, I have healed these waters; there shall not be from there any more death or miscarrying.

Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena. 2 Wafalme 2:22

So the waters were healed to this day, according to the word of Elisha which he spoke.

Akakwea kutoka huko mpaka Betheli; naye alipokuwa akienda njiani, wakatoka vijana katika mji, wakamfanyizia mzaha, wakamwambia, Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa! 2 Wafalme 2:23

He went up from there to Bethel; and as he was going up by the way, there came forth young lads out of the city, and mocked him, and said to him, Go up, you baldy; go up, you baldhead.

Akatazama nyuma akawaona, akawalaani kwa jina la Bwana. Wakatoka dubu wawili wa kike mwituni, wakawararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao. 2 Wafalme 2:24

He looked behind him and saw them, and cursed them in the name of Yahweh. There came forth two she-bears out of the wood, and mauled forty-two lads of them.

Akatoka huko akaenda mlima wa Karmeli, na toka huko akarudi mpaka Samaria. 2 Wafalme 2:25

He went from there to Mount Carmel, and from there he returned to Samaria.