2 Wafalme 24 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 24 (Swahili) 2nd Kings 24 (English)

Katika siku zake akakwea Nebukadreza, mfalme wa Babeli na Yehoyakimu akawa mtumishi wake muda wa miaka mitatu;kisha ,akageuka,akamwasi. 2 Wafalme 24:1

In his days Nebuchadnezzar king of Babylon came up, and Jehoiakim became his servant three years: then he turned and rebelled against him.

Naye Bwana akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii. 2 Wafalme 24:2

Yahweh sent against him bands of the Chaldeans, and bands of the Syrians, and bands of the Moabites, and bands of the children of Ammon, and sent them against Judah to destroy it, according to the word of Yahweh, which he spoke by his servants the prophets.

Hakika kwa amri ya Bwana mambo hayo yalimpata Yuda, ili waondoshwe kutoka machoni pake, kwa sababu ya dhambi zake Manase, kadiri ya yote aliyoyafanya; 2 Wafalme 24:3

Surely at the commandment of Yahweh came this on Judah, to remove them out of his sight, for the sins of Manasseh, according to all that he did,

tena kwa ajili ya damu zisizo na hatia alizozimwaga; kwani aliujaza Yerusalemu damu zisizo na hatia; wala Bwana hakukubali kusamehe. 2 Wafalme 24:4

and also for the innocent blood that he shed; for he filled Jerusalem with innocent blood: and Yahweh would not pardon.

Basi mambo yote ya Yehoyakimu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? 2 Wafalme 24:5

Now the rest of the acts of Jehoiakim, and all that he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah?

Yehoyakimu akalala na babaze; na mwanawe Yekonia akatawala mahali pake. 2 Wafalme 24:6

So Jehoiakim slept with his fathers; and Jehoiachin his son reigned in his place.

Basi mfalme wa Misri hakuja tena kutoka nchi yake; kwa kuwa mfalme wa Babeli alikuwa amemnyang'anya nchi, tangu kijito cha Misri mpaka mto wa Frati, yote aliyokuwa nayo mfalme wa Misri. 2 Wafalme 24:7

The king of Egypt didn't come again out of his land any more; for the king of Babylon had taken, from the brook of Egypt to the river Euphrates, all that pertained to the king of Egypt.

Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala miezi mitatu katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani wa Yerusalemu. 2 Wafalme 24:8

Jehoiachin was eighteen years old when he began to reign; and he reigned in Jerusalem three months: and his mother's name was Nehushta the daughter of Elnathan of Jerusalem.

Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, mfano wa yote aliyoyafanya baba yake. 2 Wafalme 24:9

He did that which was evil in the sight of Yahweh, according to all that his father had done.

Wakati ule watumishi wa Nebukadreza mfalme wa Babeli wakakwea kwenda Yerusalemu, na mji ukahusuriwa. 2 Wafalme 24:10

At that time the servants of Nebuchadnezzar king of Babylon came up to Jerusalem, and the city was besieged.

Na Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akaufikilia huo mji, hapo watumishi wake walipokuwa wakiuhusuru. 2 Wafalme 24:11

Nebuchadnezzar king of Babylon came to the city, while his servants were besieging it;

Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maakida wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake. 2 Wafalme 24:12

and Jehoiachin the king of Judah went out to the king of Babylon, he, and his mother, and his servants, and his princes, and his officers: and the king of Babylon took him in the eighth year of his reign.

Akatoa huko hazina zote za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme, akavikata-kata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani, mfalme wa Israeli, alivifanya katika hekalu la Bwana, kama Bwana alivyosema. 2 Wafalme 24:13

He carried out there all the treasures of the house of Yahweh, and the treasures of the king's house, and cut in pieces all the vessels of gold, which Solomon king of Israel had made in the temple of Yahweh, as Yahweh had said.

Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi. 2 Wafalme 24:14

He carried away all Jerusalem, and all the princes, and all the mighty men of valor, even ten thousand captives, and all the craftsmen and the smiths; none remained, save the poorest sort of the people of the land.

Akamchukua Yekonia mpaka Babeli; na mama yake mfalme, na wake zake mfalme, na maakida wake, na wakuu wa nchi, aliwachukua mateka toka Yerusalemu mpaka Babeli. 2 Wafalme 24:15

He carried away Jehoiachin to Babylon; and the king's mother, and the king's wives, and his officers, and the chief men of the land, carried he into captivity from Jerusalem to Babylon.

Na mashujaa wote, watu elfu saba, na mafundi na wafua chuma elfu moja, wote pia wenye nguvu, tayari kwa vita, hao wote mfalme wa Babeli aliwachukua mateka mpaka Babeli. 2 Wafalme 24:16

All the men of might, even seven thousand, and the craftsmen and the smiths one thousand, all of them strong and apt for war, even them the king of Babylon brought captive to Babylon.

Mfalme wa Babeli akamtawaza Matania, ndugu ya baba yake, awe mfalme badala yake, akalibadili jina lake, akamwita Sedekia. 2 Wafalme 24:17

The king of Babylon made Mattaniah, [Jehoiachin's] father's brother, king is his place, and changed his name to Zedekiah.

Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Hamutali, binti Yeremia wa Libna. 2 Wafalme 24:18

Zedekiah was twenty-one years old when he began to reign; and he reigned eleven years in Jerusalem: and his mother's name was Hamutal the daughter of Jeremiah of Libnah.

Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Yehoyakimu. 2 Wafalme 24:19

He did that which was evil in the sight of Yahweh, according to all that Jehoiakim had done.

Maana kwa sababu ya hasira ya Bwana mambo hayo yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata alipokuwa amewaondosha wasiwe mbele ya uso wake; naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.

2 Wafalme 24:20

For through the anger of Yahweh did it happen in Jerusalem and Judah, until he had cast them out from his presence. Zedekiah rebelled against the king of Babylon.